Kwa wanaoamini uchawi wanaweza kusema uongozi wa timu kubwa Valencia inayoshiriki ligi kuu ya Spain ulipigwa juju kiasi cha kupofushwa akili na kumpa kazi mtu asiye na uwezo wowote wa kufundisha soka .
wako wadau wa soka walioenda mbali zaidi na kuona ni afadhali kazi hiyo angepewa Sunday Kayuni kuliko Neville ambaye pamoja na mambo mengine ameleta aibu kubwa sana valencia baada ya timu yake kupigwa mabao 7 na barca kwenye kombe la mfalme.
chini ya kocha wa muda palco ayestaran timu imechupa hadi nafasi ya 8 kutoka nafasi za chini kabisa za kushuka daraja , ikiwa na points 43 baada ya jana kuivurumisha Eibar 4 - 0.
ushauri kwa vilabu vya soka hakikisheni kwanza uwezo wa kocha mpya kabla hamjampa kazi , kosa kama hili ilifanya timu ya simba juzijuzi kwa kumpa ukocha mbeba jezi , eti kisa katokea uingereza , yaliyotokea mmeyaona .