Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,583
- 13,270
Dar es Salaam. Unaweza kusema hafla ya uwekaji jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam umewakutanisha wanachama wa CCM na Chadema.
Wanachama hao wakiwa wamevalia sare za vyama vyao wamejitokeza kwa wingi leo Jumatano Desemba 19, 2018 kushiriki hafla hiyo inayofanyika eneo la Kimara Stop Over huku wakiwa wameketi pamoja.
Si kila mmoja kuvaa sare za chama chake, pia baadhi walionekana kuimba na kutabasamu ili mradi tu kufurahia tukio hilo.
Wakati wanachama wa CCM wakiimba nyimbo za chama hicho, wa Chadema wameonekana wakinyoosha mikono juu na kuonyesha vidole viwili ishara inayotumiwa na chama chao huku wakiwa na baadhi ya wanachama wa CUF.
Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika naye ni miongoni mwa waliojitokeza katika uzinduzi huo na kuketi sambamba na mbunge wa Kinondoni (CCM), Maulid Mtulia. Awali Mtulia alikuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF.
Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara ambaye awali alikuwa mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya Chadema kabla ya kuhamia CCM na kupitishwa kuwania ubunge na baadaye kuteuliwa kuwa naibu waziri, naye amehudhuria hafla hiyo na ameonekana akisalimiana kwa bashasha na Mnyika.
Rais John Magufuli ndiye atakayeweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara hiyo ambayo leo kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana imefungwa kuanzia eneo la Kimara Stop Over hadi Kimara Temboni.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 19.2 kutoka Kimara hadi Kibaha ikikamilika itakuwa na njia nane.
Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni waliokuwa wenyeviti wa CCM wa mikoa na wilaya ambao jana Halmashauri Kuu ya chama hicho tawala ilitangaza kuwasamehe na kuwarejeshea uanachama wao wakiwemo Ramadhan Madabida na Salum Madenge.
UPDATES;
JOHN MNYIKA ANASEMA
Mhe. Rais kwa niaba ya wananchi, tunakushukuru kwamba umeamua kodi za walipa kodi wa Tanzania ziweze kujenga barabara ya njia nane asante sana.
"Naamini Watanzania wamekuombea usiwe na kiburi, Wananchi wana malalamiko juu ya Bomoabomoa nakuomba kwa kutanguliza utu, Mwl. Nyerere alisema maendeleo ni ya vitu lakini maendeleo zaidi ni ya watu tafakari kuwalipia fidia Wananchi waliopisha ujenzi huu"
"Demokrasia na Maendeleo ni mapacha, tunakuomba Rais unapofanya kazi za Miradi ya Maendeleo vilevile ukatumia fursa hii kuzungumzia kuondoa vikwazo vinavyoikabili Demokrasia ya Nchi ambayo tunaamini vitasaidia Nchi kusonga".
"Kuna mambo matano yanatoka kwa Mbowe ambayo anawaomba Watanzania na wewe Rais muyatafakari tunapoingia mwaka 2019". Mheshimiwa rais ntakukabidhi.
"Rais umepiga marufuku kuzungumzia kauli ya vyuma kukaza lakini ukweli vyuma vimekaza, vyuma havijakaza kwa Mafisadi peke yake, vyuma vimekaza kwa Wananchi wa kawaida"
"Ukisikia Wafanyakazi wa Umma wanalilia kikokotoo, wengine wamepandishwa madaraja hawajapandishwa mishahara, Wafanyabiashara wanalia Mtaani, Rais ukipata nafasi ya kuzungumza pamoja na uzinduzi utatoa matumaini ya Taifa kwa 2019 na 2020"
"Juhudi zote za ujenzi wa barabara, ukuaji wa uchumi tunaziunga mkono kwa 200%, Mnyika kaeleza Wananchi wana malalamiko kutokana na fidia ya maeneo waliokuwa wanaishi" Kubenea
PAUL MAKONDA ANASEMA
Mkuu wa Dar Paul Makonda: "Hivi niwaulize watani zangu wa CHADEMA, mnapompinga Rais Magufuli, mnapinga kwa kosa lipi? Kosa lake ni kujenga flyover, kosa lake ni kutoa elimu bure? kosa lake ni kujenga barabara 8 mpite? Cha ajabu nyie ofisi yenu pale Kinondoni mmeshindwa hata kuijenga."
Mkuu wa Dar Paul Makonda: "CHADEMA walikataa kuje kwenye uzinduzi wa Mfugale Flyover, lakini walipoenda #Zanzibar, sijui walikuwa wanafanya nini huko, waliona raha kupita juu ya barabara ile. Sasa mnampinga Rais Magufuli kwa lipi?"
PATRICK MFUGALE ANASEMA
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Patrick Mfugale: "Katika barabara nane zitakazokuwa kati ya Kimara ya Kibaha, mabasi yatatumia barabara za katikati, huku magari madogo na magari makubwa ya mizigo yakitumia barabara za pembeni."-
ISACK KAMWELE ANASEMA
Waziri wa Ujenzi, Isack Aloyce Kamwelwe: "Mheshimiwa Rais kuna mfanyabiashara mmoja anaitwa Fastjet, juzi alitubipu, na sisi tumempigia." "Kati ya ndege mpya mbili za ATCL zitakazokuja mwezi huu, ndege moja itaanza safari Disemba 26 (Boxing Day)."-
RAIS MAGUFULI ANASEMA
Rais Magufuli: Nashukuru kualikwa kuja kuzindua barabara hii yenye urefu wa Kilometa 19.2
- Sijawahi kufanya mkutano wa hadhara ila nilisimama hapa wakati wa kampeni za kumtafuta Diwani wa Kata na nikawaomba mchague CCM na haya ndio matunda
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Mwaka 1997 barabara zilizokuwepo hapa zilikuwa hazitoshi kwa msongamano wa magari
- Palikuwepo na umuhimun wa kupanua barabara hii na wakati huo mimi nilikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Tulizungumza na Seriklai ya Denmark kutuzaidia kupanua barabara iliyokuwepo iliyokuwa imekweisha
- Wakati tukitaka kupanua, Wataalamu wanaojua sheria wakiongozwa na Prof. Mgongofimbo Mwalimu wa UDSM wakaishtaki Serikali
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Kwa wale wanaotaka kwenda kuangalia na najua Mheshimiwa Mnyika amesoma sheria waaende wakaangalie kesi namba 39 ya mwaka 1997 iliyofunguliwa Mahakama Kuu
- Mshtakiwa alikuwa Mwanasheria Mkuu na Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Serikali ilishinda kesi hiyo na aliyekuwa Mtetezi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu alikuwa Mheshimiwa Welema
- Baada ya kushinda kesi, Wizara ya ujenzi tukaanza kubomoa nyumba na kuanza ujenzi wa mradi uliosimamiwa na Denmark
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Serikali imeingia gharama za kuweka mpaka wa barabara Tanzania nzima ili kuwajulisha Watanzania kuwa hapa ndio mpaka
- Kwa bahati mbaya sana baadhi ya Watanzania ama kwa kurubuniwa na baadhi ya Wasiasa ili kupata kura, hawakusikia
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Wanasiasa walishindwa kuwaambia ukweli kuwa kwenye kesi iliyosimamiwa na Prof. Mgongofimbo Mwalimu wa Chuo Kikuu, Serikali ilishinda
- Wananchi wa Ubungo kuna mtu aliwachangisha hela kwamba watafungua kesi, mwisho wakatapeliwa
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Nawaambia nikiwa Rais kwamba ukisogelea barabara hasa Road Reserve madhara yake ni umaskini
- Nataka niwaambie Wananchi, waliobomoleshwa kwenye nyumba hizi wamo ndungu zangu. Mfano ni marehemu Msabila na wamebaki watoto wake watatu
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Ndugu zangu fidia hakuna, hata uwende wapi huwezi kusinda kesi hii ilishaamuliwa na Mahakama Kuu
- Lengo ni kutengeneza miundombinu tena tumejenga barabara hii hapa kwenye jimbo la wapinzani kwa kuwa maendelo haya chama
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Barabara hii ilikuwa ifadhiliwe na baadhi wa development partners wetu, tukaona tunacheleweshwa kwa sababu ya masharti
- Tukasema kwa nchi inayojitambua hawezi kuchelewa kwa sababu ya misaa, mtaji wa maskini nin nguvu zake mwenyewe
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Ndugu zangu fidia hakuna, hata uwende wapi huwezi kushinda kesi hii ilishaamuliwa na Mahakama Kuu
- Lengo ni kutengeneza miundombinu tena tumejenga barabara hii hapa kwenye jimbo la wapinzani kwa kuwa maendelo hayana chama
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Wafadhili waliahidi kujenga njia nne lakini tukasema tujiongeze zaidi kwa sababu uamuzi na fedha ni zetu
- Ndio maana tumejenga njia nane na sehemu nyingine kutakuwa na njia hadi 12
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Tumetumia nguvu zetu kujenga barabara na mtu anaweza kusema ni kodi zetu, ni kweli. Kwani miaka ya nyuma mlikuwa hamlipi kodi? Mbona hazikujengwa?
- Sema tu Magufuli umesimamia kodi na tunaiona inatengeneza barabara, tunakushukuru
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Kwa Dar hapa miradi ya barabara tunatengeneza zaidi ya Kilometa 212 kwenye miradi ya thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 660. Haijawahi kutokea
- Na ndio maana kila kona mnaona kuna Wakandarasi wanaendelea na shughuli
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Tungekuwa wabaya sisi CCM tusingeweka Dar kwa sababau hata Mstahiki Meya sio wa CCM ila namshukuru maana anajua kabisa huku ndio kutekeleza ilani ya CCM
- Watu wanatukataa lakini bado tunawaletea maendeleo lakini bado hawaridhiki
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Kelele nyingi za Mnyika katika jimbo lake ilikuwa maji na napongeza kwa kulalamikia maji lakini Serikali imetekeleza miradi ya mabilioni
- Nilitegemea aliposimama hapa angesema asanteni sana niliwaambia maji mmetekeleza, Asante CCM
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Mnyika aliposimama hapa kazungumzia Demokrasia sijui demokrasia gani anataka
- Tumekaa hapa CCM, CHADEMA na CUF, ameitwa kwenye mkutano ambao Rais ni Mwenyekiti wa CCM anazungumza sijui anataka demokrasia gani. Demoktasia sio fujo
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Hizi fedha zinazotengeneza barabara siku za nyuma zilikuwa hazitumiki kwenye barabara
- Tulipoingia madarakani tuliamua kuhakikisha nchi inakusanya kodi na kodi ikaongezeka kutoka Bilioni 850 hadi Trilioni 1.3
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Tulibadilisha hata mwelekeo wa bajeti ya Serikali badala ya kupeleka asilima 20 kwenye miradi ya maendeleo tukapeleka asilimia 40
- Ndio maana tukatoa elimu bure, kwa kutenga Bilioni 23.8 kila mwezi. Tumelenga kutoa elimu bure
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
MWITA WAITARA ANASEMA
"Leo ni mara ya kwanza nimesimama mbele yako Rais tangu nilipoachana na kile chama ambacho hakina shukrani hata mbele za Mungu. Nilikuwa upinzani kwa miaka 10, lakini kwa vile hakukuwa na shukrani nikaondoka, wewe chapa kazi, hizi kelele zisikusumbue."
Rais Magufuli: Watanzania wote wa vyama vyote tunawajibu wa kujipongeza kwa kuwa tunafanya makubwa
- Tanzania kwa sasa ni miongoni mwa nchi 5 kwa Afrika ambazo uchumi unakua, inflation imeshuka kutoka 12 hadi 3
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Siasa za kubembelezana zimapitwa na wakati kwa kuwa zinatuchelewesha, mimi nawaambia ukweli
- 'Hakuna mtu atakayekufa na njaa' mimi nawaambia upofanyakazi utakufa na njaa kwa kuwa hakuna wa kukulimia chakula ili ile wewe
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Haiingi akili unakuta mtu anafanya kazi ya mradi haya haifiki Milioni 4 ananyang'anywa, mama nauza chakula ananyang'awa halafu mgambo anakula
- Hili ni marufuku, Tanzania hii ni ya wote wa hali ya juu, chini na katikati
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Hili la vyuma vimebana ni siasa tu na Watanzania wanaelewa sana ndio maana wengine waliamua kutoka huko walipokuwa
- Kuna Mheshimiwa Mwita hapa, zamani alikuwa anazungumza hivyo hivyo ila sasa hivi anasema 'CCM hoyee'
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Nimuombe Mkandarasi aakamilishe barabara hii kwa wakati tena kwa viwango vinavyotakiwa
- Ikiwezekana afanye kazi uziku na mchana kwa kuwa Watanzania wanaihitaji barabara hii
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Niwaombe vijana wa maeneo haya msilalamike vyuma vimebana ni wakati wa kuomnba kazi hata kwa Mkandarasi huyu
- Kama utapewa ya kuchimba mtaro au kundesha greda ama kukusanya kokoto chuma hakiwezi kubana, utakibanua
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Inawezekana watu hawaelewi historia ya huu mpango wa kujenga barabara kwa fedha zetu ila uliasisiwa na Mzee Mkapa
- Baada ya mvua za Elnino za mwaka 1997, barabara zilikuwa mbaya zinapitika kwa shida...inawezwekana watu wamesahau
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Namshukuru Spika na Bunge kwa ujumla maana kwa kipindi hiki limepitisha sheria zenye manufaa kwa nchi yetu
- Nawashukuru madiwani katika maeneo yao wakuwa wasimamizi wazuri wa Rasilimali. Pia nawashuru Wanahabari, ukiacha wachache
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Rais Magufuli: Nawashukuru Wabunge wote nasema kwa dhati bila kubagua vyama wote
- Najua Mnyika unanipenda, Kubenea unanipenda na ndio maana mmekaa pamoja. Mnapokaa ninyi najua mnazungumza ukweli kwamba lakini kajamaa kanatutwanga
#JFLeo #UzinduziBarabaraKimara
Habari zaidi....
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 19 Desemba, 2018 ameweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Morogoro Jijini Dar es Salaam katika sehemu ya kuanzia Kimara hadi Kibaha yenye urefu wa Kilometa 19.2.
Upanuzi huo utahusisha kuongeza njia za magari kutoka 2 zilizopo sasa hadi 8, kujenga madaraja 6 na makalavati 36, na kujenga barabara ya juu (Flyover) katika eneo la Kibamba CCM kwenye makutano ya barabara inayotokea Bunju na barabara ya kwenda hospitali ya Mloganzila.
Sherehe za uwekaji jiwe la msingi la mradi huo zimefanyika katika eneo la Kimara Stopover na kuhudhuriwa na Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri, Wabunge, viongozi wa Dini, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Makonda.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema barabara ya Morogoro ni lango kuu la usafiri kati ya Jiji la Dar es Salaam lenye bandari kuu na mikoa mingi ya Tanzania Bara na nchi jirani, na kwamba upanuzi wake utasaidia kupunguza msongamano mkubwa wa magari takribani 50,000 yanayopita katika barabara hiyo kwa siku na utaokoa muda kutoka saa tatu zinazotumika kupita eneo hilo kwa sasa hadi nusu saa.
Amebainisha kuwa upanuzi wa barabara hiyo utafanyika kwa muda wa miezi 30 kuanzia tarehe 21 Julai 2018 na utagharimu shilingi Bilioni 141.56, fedha zote zinatolewa na Serikali ya Tanzania.
Akizungumza katika sherehe hizo Mhe. Rais Magufuli amewapongeza wananchi wa Dar es Salaam kwa kupatiwa mradi huo mkubwa na kubainisha kuwa pamoja na barabara hiyo Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea kuboresha miundombinu ya Dar es Salaam ambapo barabara zenye jumla ya kilometa 212 zinajengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 660.
Kuhusu fidia kwa nyumba zilizovunjwa wakati wa upanuzi wa barabara hiyo Mhe. Rais Magufuli amewataka wanasiasa kuacha kuwapotosha wananchi kuwa watalipwa fidia, na amesema Serikali haitalipa fidia kwa mtu yeyote aliyejenga katika eneo la hifadhi ya barabara kwa mujibu wa sheria.
“Kuna wanasiasa wanataka waonekane wao ndio wanawatetea wananchi na wanasema Serikali itoe fidia, nataka niwaambie ndugu ukivamia barabara unatafuta umasikini, fidia haipo, fidia haipo, narudia fidia haipo” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli na kuwataka Watanzania kote nchini kuacha kuvamia maeneo ya hifadhi ya barabara na kujenga makazi.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kulipa kodi na kwamba Serikali itaendelea kuhakikisha kodi inayokusanywa inasimamiwa vizuri kwa kuelekezwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, kuendeleza elimu, afya na kuboresha upatikanaji wa maji ukiwemo mkoa wa Dar es Salaam ambao kwa sasa unapata maji kwa asilimia 75.
Mhe. Rais Magufuli amewaonya Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam waliokuwa wakichelewesha kuanza kwa ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi kutokana na kubishana juu ya mkandarasi wa kukijenga na kubainisha kuwa “Nilikuwa nawafuatilia jinsi mnavyobishana na leo mngekuwa bado mnabishana nilipanga nitangaze kuondoa fedha hizo (shilingi Bilioni 50) na kupeleka mahali pengine, ndugu zangu viongozi naomba tutangulize maslahi ya wananchi, sio maslahi yetu binafsi”.
Mapema Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa namna Serikali inavyosimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kumhakikishia kuwa Bunge litaendelea kuunga mkono juhudi hizo zenye maslahi makubwa kwa Taifa.
Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika Mkoa huo ikiwemo kutatua tatizo la maji, kuimarisha miundombinu ya barabara na reli, kununua ndege na kuboresha uwanja wa ndege na kuboresha huduma za afya na elimu.
Wakati huo huo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema Serikali itaanza kutekeleza sheria ya kudhibiti uzito wa magari barabarani kuanzia Januari 2019 ili kuokoa uharibifu mkubwa wa barabara unaojitokeza katika barabara nyingi hivi sasa.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Desemba, 2018