Uzi wa kuelezea matukio ya kutisha uliyowahi kukumbana nayo maishani, either ya kichawi,anything scary

ngebo

JF-Expert Member
Sep 8, 2017
1,684
2,127
Wenyewe habarini za mchana ,this thread pls tuelezee matukio ya kutisha ambayo wewe binafsi umeshawahi kukutana nayo dunia hii kwenye kuishi kwako, mimi binafsi sitosahau siku moja nilikua kijijini kwetu then ilikua usiku wa saa mbili ninakwenda dukani nikakutana na mtu mrefu kweli amevaa nguo nyeupe ila sura sikuweza kuona, ile nimefika mbele na kugeuka sikumwona tena, hizo mbio zilizofata ni noma nilivyofika dukani nikaomba escort ya kurudi hom
.
.
.
Nawakaribisha tuje kushare experience zetu , pls kama hujawahi kumbwa usicomment mambo yasiyo na busara pia MSILETE SIASA ,maana najua baadhi wataanza sema ,Lissu kupigwa risasi, sijui makinikia mara bombadia..etc so tuchill kwa hayo kwani jukwaa la siasa lipo .

Nawakilisha
 
Me nakumbuka nikiwa moja Kati ya mbuga za wanyama kaskazini asubui ya saa10 tukiwa patrol (ndo tunarudi) Kumbe tunapita njia ya viboko (hippopotamus) kulikuwa na Giza kumbuka kwaiyo hatukuwaona mapema Wewe kuja kustukuka hao hapo!! Tulikuwa group na mm ndo nlikuwa mdogo na jinsia tofauti nikamshika mmoja wetu shati asee nilisukumwa nikadondoka chini nikakanyagwa kama ardhi Yaani nilihisi ndo siku yangu mwisho nikabaki Pekee Yang nimeumia natetemeka siwezi hata kunyanyua mguu nikicheki viboko (group) wenyewe wako jirani kabisa wanakuja taratibu ,,Yaani nilibiringita mpaka pembeni na Huku nasali sala zote hata maumivu sikusikia tena wakapita bila hata kunigusa ni mungu tuu,,baadae etii ndo wanakuja kunitafuta baada ya kujua sionekani
 
Me nakumbuka nikiwa moja Kati ya mbuga za wanyama kaskazini asubui ya saa10 tukiwa patrol (ndo tunarudi) Kumbe tunapita njia ya viboko (hippopotamus) kulikuwa na Giza kumbuka kwaiyo hatukuwaona mapema looh! kuja kustuka hao hapo!! Tulikuwa group na mm ndo nlikuwa mdogo na jinsia tofauti nikamshika mmoja wetu shati asee nilisukumwa nikadondoka chini nikakanyagwa kama ardhi Yaani nilihisi ndo siku yangu mwisho nikabaki Pekee Yang nimeumia natetemeka siwezi hata kunyanyua mguu nikicheki viboko (group) wenyewe wako jirani kabisa wanakuja taratibu ,,Yaani nilibiringita mpaka pembeni na Huku nasali sala zote hata maumivu sikusikia tena wakapita bila hata kunigusa ni mungu tuu,,baadae etii ndo wanakuja kunitafuta baada ya kujua sionekani
 
Me nakumbuka nikiwa moja Kati ya mbuga za wanyama kaskazini asubui ya saa10 tukiwa patrol (ndo tunarudi) Kumbe tunapita njia ya viboko (hippopotamus) kulikuwa na Giza kumbuka kwaiyo hatukuwaona mapema Wewe kuja kustukuka hao hapo!! Tulikuwa group na mm ndo nlikuwa mdogo na jinsia tofauti nikamshika mmoja wetu shati asee nilisukumwa nikadondoka chini nikakanyagwa kama ardhi Yaani nilihisi ndo siku yangu mwisho nikabaki Pekee Yang nimeumia natetemeka siwezi hata kunyanyua mguu nikicheki viboko (group) wenyewe wako jirani kabisa wanakuja taratibu ,,Yaani nilibiringita mpaka pembeni na Huku nasali sala zote hata maumivu sikusikia tena wakapita bila hata kunigusa ni mungu tuu,,baadae etii ndo wanakuja kunitafuta baada ya kujua sionekani
Hahaa dah kweli we ganja gal, ashukuriwe mungu, kwani viboko wanakula watu?
 
Kuna kipindi tulisha wahi kukutana na nyoka, kwenye msitu wa Ml.Kilimanjaro bonge la nyoka, tulikuwa 3 wawili wa kiume na mmoja wa kike wote tukajikuta tumelengea hatujui la kufanya, baada nzuri alikuwa anakatisha kwenye uchochoro

Siku nyingine tukiwa Mitaa flani ya Moshi na bonge la jini jitu moja la mtu limeenda hewani limevaa nguo nyeupe, tulisepa si mchezo yaani tulipotezana wote, wote tukaja kukutana hom
 
Dah nyoka ni ugonjwa naweza anguka apo apo pole sana mkuu
 
Ilikuwa usiku, sikumbuki ilikuwa saa ngapi. Tulikuwa watatu kitandani. Mimi, Dada yangu na binti wa jirani alikuja kutupa kampani ya kulala sababu tulikuwa wadogo na ni wageni katika eneo moja daslam, baadae nilikuja kufahamu kuwa kunaitwa makuburi.
Tulikuwa tumelala mzungu wa nne, Dada na mwenzie wamelala upande wa miguuni huku wanapiga stori, mimi nililala upande wa kichwani nilikuwa kimya. Na ndio niko hivyo hadi sasa.
Pamoja na usiku kuwa mkubwa siku hiyo tulichelewa kupata usingizi. Kwahiyo wakati wenzangu wanapiga stori, mi nilikuwa zangu nimetulia kimya!
Lakini ghafla kilitokea kitu ambacho kilinishtua! Niliona mtu mweupe amesimama pembeni ya kitanda upande wa ukutani! Kilichonishangaza, kitanda kimegusa hadi ukutani, yule mtu amewezaje kusimama?!
Lakini cha ajabu sikuogopa kabisa! Nikabaki kimya namuangalia, huku wenzangu wanaendelea na stori.
Mara akaanza kukizunguka kitanda, nilikuwa namcheki tu ila nilikuwa makini kumfuatilia! Alizunguuka kama mara tatu kisha akasimama na kuanza kuninyooshea mkono. Nikashtuka! Basi ikawa kama mchezo, kadri anavyosogeza mkono na mimi nasogea. Nilisogea hadi kitanda nikakimaliza. Kilichobaki ni kuporomoka tu! Nikaona hapa ni kuwaeleza wenzangu tu! Wanawake bwana! Nilivyowaeleza tu "jamani mtu huyo ukutani!" Ikawa hekaheka humo chumbani, wote wakakurupuka kitandani huku wakipiga kelele! "Mamaaa mtuuuuu!!" Dingi na maza walikurupuka chumbani kwao panga mkononi!! Yule mtu katoweka! Tangu siku hiyo tukawa tunalala na wazee chumbani kwao, na yule binti karudi kwao. Ila baada ya wiki tukaswagwa kwa bibi. Ila baadae wazee walihama kabisà.
Hii ishu ilinitokea mwaka 1984 au 85 juu ya godoro la Sufi. Sitaweza kuisahau huu mkasa!
 
Shukurani kwa mtoa uzi

Siku ambayo sitakuja kuisahau kamwe Maishani mwangu ni kipindi nasoma shule flani kule mkoani ruvuma nikiwa kidato cha sita, nikiwa naishi bweni , ni wiki kadhaa toka nijiapize moyoni mwangu kua ulokole siutaki tena,
Tukiwa tupo bwenini purukushani za viongozi a.k.a vilanja zikiwa zinaendelea za kututaka tuondoke bwenini, nikiwa naharaka ya kubeba material yangu niende darasan Mara niliona Pete( ndio pete unayoijua wewe ya kuvaa kidoleni) iliwa kwenye kitanda flani bila ya kujiuliza na kutafakari niliichua na kuondoka nayo adi darasani, nikiwa naendelea kusoma nikakumbuka juu ya ile Pete akiri yangu ikanituma nivae, nami bila kusita nikaivaa nikaendelea kusoam , Muda wa prepo ulipo isha nilirudi bwenini! Tukiwa tunaendelea na story Mara nikasikia mtu anasema kwa sauti ya chini na akiwa anauliza majirani wake kua kuna mtu amechukua Pete yake! Nilimsikia lakini nilimpuuza na nikapanga nimpe kesho yake, kwa hiyo nililala Nayo! MUNGU wangu nikiwa nimelala sikumbuki ilikua saa ngapi ! ilikuja ndoto ya ghafla nikaona Mtu akiwa amevaa nguo Nyeusi toka juu adi chini na USO wake akiwa ameufunika mkononi akiwa ameshika fimbo flani akaja adi pembeni ya kitanda changu na kuniangalia kwa sekunde kadhaa halafu akaninyooshea fimbo yake kisha akapotea nilistuka na nliogopa sana, nilipo tazama wenzangu nlisikia sauti za kukoroma tu hakna aliejua nini kilinitokea, nililala tena ghafla niliota namuona jirani yangu anapaa juu kitandani kwake akiwa amelala vile vile hiyo ndoto ikakata,------- lakini ghafla tulishitishwa na kelele za juu sanaa kama mtu analia kwa sauti kubwa ,wote tuliamka nakuanza kumuhoji , jamaa akasema nimeona mtu ananipaisha juu ndo nmeanguka! Kumbukumbu zangu zilirejea kwenye ndoto yangu! Lakini sikumwambia mtu yeyote , amini usiamini kesho nilipata msala msala wa ajabu ambao ulisababisha nikafukuzwa shule siku hiyo hiyo, Sitokuja kusahau hii kitu
 
Ilikuwa usiku, sikumbuki ilikuwa saa ngapi. Tulikuwa watatu kitandani. Mimi, Dada yangu na binti wa jirani alikuja kutupa kampani ya kulala sababu tulikuwa wadogo na ni wageni katika eneo moja daslam, baadae nilikuja kufahamu kuwa kunaitwa makuburi.
Tulikuwa tumelala mzungu wa nne, Dada na mwenzie wamelala upande wa miguuni huku wanapiga stori, mimi nililala upande wa kichwani nilikuwa kimya. Na ndio niko hivyo hadi sasa.
Pamoja na usiku kuwa mkubwa siku hiyo tulichelewa kupata usingizi. Kwahiyo wakati wenzangu wanapiga stori, mi nilikuwa zangu nimetulia kimya!
Lakini ghafla kilitokea kitu ambacho kilinishtua! Niliona mtu mweupe amesimama pembeni ya kitanda upande wa ukutani! Kilichonishangaza, kitanda kimegusa hadi ukutani, yule mtu amewezaje kusimama?!
Lakini cha ajabu sikuogopa kabisa! Nikabaki kimya namuangalia, huku wenzangu wanaendelea na stori.
Mara akaanza kukizunguka kitanda, nilikuwa namcheki tu ila nilikuwa makini kumfuatilia! Alizunguuka kama mara tatu kisha akasimama na kuanza kuninyooshea mkono. Nikashtuka! Basi ikawa kama mchezo, kadri anavyosogeza mkono na mimi nasogea. Nilisogea hadi kitanda nikakimaliza. Kilichobaki ni kuporomoka tu! Nikaona hapa ni kuwaeleza wenzangu tu! Wanawake bwana! Nilivyowaeleza tu "jamani mtu huyo ukutani!" Ikawa hekaheka humo chumbani, wote wakakurupuka kitandani huku wakipiga kelele! "Mamaaa mtuuuuu!!" Dingi na maza walikurupuka chumbani kwao panga mkononi!! Yule mtu katoweka! Tangu siku hiyo tukawa tunalala na wazee chumbani kwao, na yule binti karudi kwao. Ila baada ya wiki tukaswagwa kwa bibi. Ila baadae wazee walihama kabisà.
Hii ishu ilinitokea mwaka 1984 au 85 juu ya godoro la Sufi. Sitaweza kuisahau huu mkasa!
Aisee nimeisoma asubuhii hii,, alikua amevaa ni i huyo mtu? Ni mvulana su msichana?
 
Back
Top Bottom