Uzi maalum wa kuelezea stress zako na njia unazotumia kukabiliana nazo

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
4,356
11,083
Picha linaanza daktari anakusomea majibu ya vipimo vyako bila kutarajia anakwambia una UKIMWI , ile hali na mshutuko utakaoupata baada ya hapo ndio STRESS zenyewe.

Just imagine umesota sana mpaka ukapata kazi mambo yako yapo vizuri, mke wako kajifungua mtoto mzuri wa kike. Bila kutarajia boss wako anakupa taarifa kuwa umefukuzwa kazi na ukiangalia hali ilivyo huna pa kupata kazi sehemu nyingine, ile hali itakayokupata ndio STRESS zenyewe.

Wewe ni mfanya biashara mkubwa unaheshimikabmtaani na mbali, ghafla umefilisika magari yote umeuza nyumba imepigwa mnada na benki umerudi ground zero, watu wanaanza kukucheka na kukutolea mfano kila unapopita, ile hali itakayokupata ndio STRESS zenyewe.

Umesambaza kadi watu wametoa michango na kuunda kamati ya harusi, ukumbi kila kitu kimeandaliwa siku ya ndoa bwana harusi anagoma kukuoa kisa kapata faili lako, watu wapo ukumbini wengine nyumbani, bwana harusi anaingia mitini, ile haki itakayokupata ndio STRESS zenyewe.

Sihitaji kukuambia stress ni nini, naamini umenielewa na umebaini kuwa ukishawahi kupata stress na pia bado unazo.

Kila mtu ana stress, waswahili wanakwambia wewe unashida zako na sisi tunashida zetu.

Kuna stress ndogo ndogo na stress kubwa kubwa.
Hizo hapo juu ni stress kubwa kubwa ambazo zinaweza kumfanya mtu apoteze hamu ya kuishi hata kuchukua maamuzi mabaya ya kujiua.

Stress ndogo ndogo ni kama vile kukosa pesq ya kula na hujui utazipata wapi hiyo siku

Watu wa mikopo kuja kukudai pesa mbele ya wapangaji wenzako.

Umepata mchumba mrembo unaibgia naye geto ile unaanza kupiga mambo mashine inalala na mitambo inazima jumla.

Umejiona unanguvu ukaamua kumpiga mkeo bahati mbaya anakuzidi nguvu na kukutandika vibaya mno tena mbele ya kadamnasi na story inasambaa vijiwe vyote.

Hali utakayoipata ndio stress zenyewe.

Mtu akikuambia niache nimevurugwa, leo sina mood, leo sina mzuka. Basi jua huyo ana stress zake wewe pambana na stress zako

Je, unatumia njia gani kukabiliana na stress zako?
 
Nitaanza mimi kueleza njia nnazotumia katika post hii namba mbili

Binafsi kuna kipindi stress zilinizidi, nikatafuta njia ya kuzichepusha/ku divert/kuzitoa kwenye reli.

Nilianza kuangalia mpira na kuufuatilia vilivyo, kabla ya hapo sikuwa nikiupa kipaumbele, timu yangu ikawa ni Yanga.

Kwa sasa ninajua mambo mengibkuhusu mpira na nina ufuatilia vilivyo

Kiukweli nilianza kuzisahau stress kidogo kidogo.

Mpira ulinisaidia sana mpaka nikawa siwazi mambo mengine ya hovyo hovyo ikiwemo yale ya ujana.

Uzuri wa mpira unapendwa na wengi pia unakupa nafasi ya kuchangamana na watu kwa haraka

Kwangu mpira ni mkombozi
 
Binafsi nikiwa na stress zangu huwa natafuta aidha Movie kali ninayoikubali naangalia au Katuni (Tom & Jerry)
:CATLUL: :CATLUL: :CATLUL:
Movies ni njia ya pili ya kukabiliana na stress.

Hakuna korean drama kali ambayo siijui. Baada ya kazi kama hamna mpira huwa naangalia series mdogo mdogo

Kiukweli stress huwa hazinisumbui kabisa kuzidivert au kuzi control.

Pia hii imenisaidia sana kufocus na mambo machache na kuacha yale ya hovyo hovyo


Baada ya kazi akili inawaza familia, movie au mpira


Kwa sasa nipo naangalia ADAMAS series kali ya kikorea
Screenshot_20240930-213339.png
 
Back
Top Bottom