Unamfahamu fundi gani mkali wa magari kwa uzoefu wako? Share na Jamii hapa.
Ukijaribu kuangalia kwa kina utabaini kuwa magari mengi yanaharibiwa zaidi na mafundi. Fundi hafahamu kuhusu gari lakini analifanyia trials and errors na mwishowe huharibu gari zaidi.
Mafundi ambao hawafahamu kuhusu gari fulani mara nyingi unakuta wanaponda gari ile na kufanya gari ionekane haifai kabisa kumbe ufundi wake ndio mdogo kwa gari ile. Mfano gari kama Nissan X-trail ni gari nzuri lakini kwa kuwa mafundi hawaifahamu vizuri basi gari hii imefanya ionekane ni gari moja ya hovyo sana.
Nachojaribu kuwaza: Hivi haiwezekani hapa bongo mafundi wakabobea kwenye aina fulani ya magari (yaani specialization).
Mfano: Anakuwepo fundi specialist wa Toyota ist; ama anakuwepo fundi specialist wa Subaru Forester, n.k. badala ya kila gari fundi kuweka ufundi wake.
Ndio kwa upande wa kipato inaweza kuwa changamoto kiasi chake, lakini kwa misingi ya kibiashara wanaweza kuwa na kitu kama 'Joint venture' ambapo kila fundi na specialization yake kiasi kwamba wataangalia uwiano wa kugawana mapato yao ili kila mmoja apate.
Hata kwa wale waliopo kwenye biashara ya magari wanaweza wakaanzisha biashara kama hii na wanaweza kufanikiwa sana.
Ni rahisi zaidi mwenye gari kupeleka gari lake kwa fundi specialist wa ile gari badala ya kupeleka kwa fundi general wa magari yote. Zama zimebadilika sana.
Kimsingi, mafundi wa magari ni sawa na madaktari tu kwa namna ya utendaji wao wa kazi. Daktari anatibu magonjwa ya binadamu na fundi anatibu magonjwa ya gari.
Tupe uzoefu wako wa fundi unayemkubali kwa utengenezaji wa magari ili tuweze kuwasaidia wahitaji wengine.
Karibuni tuendelee......