Uzi maalum kwa waliokosea kuoa na kuolewa au kuwa kwenye mahusiano

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
2,518
7,327
Ndugu zangu salaam

Huu ni uzi maalum kwa wale waliokosea kuoa na kuolewa pia kw wale waliokosea kuwa kwenye mahusiano.

Tuambieni ni nini ulikiona kwa mwanamke wako au mwanaume wako ukagundua hapa ulikosea kuoa au kuolewa nae.

Pia kwa wale wengine tuambieni ni nini mlikiona kwa wapenzi wenu mkagundua mlikosea kuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi

Mimi mwenyewe kabla sijaoa enzi hizo

1: Baada ya kuwa na mwanamke kimapenzi niligundua nilikosea kua nae kutokana na alikua na chuki sana na baba yake kiasi cha kumuita nguruwe, ila alikua na mama yeke ambae ni single mama na alikua akimjaza sana sumu kuhusu wanaume na kumfunza kuchuna wanaume

2: mwanamke wapili baada ya kuniomba sana hela pasi na huruma au hata nikitafuta sababu yeyote ili tuu nisimpe hela ila zinashindikana na kuzua ugomvi mkali nikajua hapa ninauziwa

3: Nilishawahi kukaa na demu gheto sogea tuishi ila yule demu alikua na mimi kwa sababu kulikua na jambo lake anataka ni msaidie avuke na alipovuka tukawa hatusikilizani tena mpaka pale macho yangu yalipofunguliwa

4: Niligundua demu huyu mwingine alikua mkosi na nilikuwa nafatiliwa sana na shetani ili aniangamize na hakuna kitu nilifanya nikafanikiwa kipindi nipo nae

5: Huyu mwingine wakati na taka mtoto alinambia ukinipa mimba utaniharibia future yangu nikajua hapa sina mtu

6: Huyu mwingine alikua na marafiki wa kiume sana na alikua akiona wanaume anaweweseka sana

7: Huyu mwingine alikua ni mzigo sana hata kunipa akili ya kununua godoro hakua nayo

8: Huyu mwingine alikua anaitaka sana ndoa na alikua analazimisha sana kunibebea ujauzito

9 : huyu mwingine alikua anaforce ni mchukue tukaishi nae hata uchumba sugu kumbe lengo lake ilikua tuu atoke kwao ili apate uhuru

10. Hakua na time na mimi na muda mwingi simu yake ilikua anasema anaweka silent ila ukiwa nae anakua romantic sana mpaka nafsi inakuambia hapa unaibiwa..

11:...... Hawa wengine niligundua nilikosea kudate nao ila bado ni wengi sana nitasema siku nyingine, je wewe ndugu yangu ni nini ulikiona kwa mwanamke / mwanaume wako ukagundua kabisa hapa sina mtu ulikosea kuwa nae kwenye maisha yako?
 
Angekuwa ni mwanamke ndio ametaja idadi hiyo ya wanaume, angeshaitwa malaya hata kama ni hao wanaume ndio waliomuacha, kumbe uhalisia wa haya mahusiano mnaujua ila huwa mnajitoa ufahamu tu
Mwanaume au dume lolote halikuumbiwa mwanamke au jike mmoja.. na ndiyo maana hata duniani wanawake ni wengi na sisi wanaume ni wachache na pia ulishawahikujiuliza wanaume tukasema tuwe na mwanamke mmoja mmoja hao wengine watadinywa na nani ili wakae sawa na je, hiyo dhambi sisi tutaenda kuisemea wapi?
 
Mwanaume au dume lolote halikuumbiwa mwanamke au jike mmoja.. na ndiyo maana hata duniani wanawake ni wengi na sisi wanaume ni wachache na pia ulishawahikujiuliza wanaume tukasema tuwe na mwanamke mmoja mmoja hao wengine watadinywa na nani ili wakae sawa na je, hiyo dhambi sisi tutaenda kuisemea wapi?
Kwanza kabisa hizo takwimu za wanawake kuwa wengi kuliko wanaume ni za dunia gani hebu ziweke hapa ili tuanzie hapo kwanza, halafu kumbuka kwenye haya mahusiano mtu akiamua kukuacha huwezi kumlazimisha abaki, sasa mnataka wanawake watumie mbinu gani ili waepuke kuachwaachwa na kujikuta wamedate na idadi kubwa ya wanaume hebu toa mawazo yako hapo
 
Back
Top Bottom