Gift mzalendo
JF-Expert Member
- Dec 13, 2019
- 1,759
- 2,271
Habari watanzania wenzangu
Nianze kwa kusema kitu chochote unachokipenda utakilinda ,utakithaminisha na kukitetea kwa gharama kubwa pale unapoona kinaweza kuchukuliwa.
Inasemekana baba wa Taifa akiwa mgonjwa Sana akisubiri ndege aende kwenye matibabu uingereza ,
Alitoa wosia kwamba
"waambie watanzania waipende nchi yao Kama wanavyopenda mama zao maana hawana nchi "
Haya yalikuwa maneno mazito sana ya kizalendo kwamba Kama vile binadamu anavyokuwa na mama mmoja tu mzazi ndivyo alivyo na nchi moja tu aliyozaliwa
Hivyo thamani ya upendo wa nchi yako inabidi ulingane na kiwango Cha upendo wa mama maana ukipoteza hakuna mbadala.
Ndugu zangu kumekuwapo na wimbi la vijana ambao wanaona uzalendo ni kutetea maslahi ya vyama vyao viongozi wao bila kujali hayo maslahi yaathiri vipi maslahi ya nchi na Taifa kwa ujumla
Hili silisemei Kwa chama kimoja tu hata vyama vya upinzani wameshindwa kuandaa vijana wazalendo ambao wako tayari kutetea maslahi ya vyama na viongozi wao bila kujali maslahi ya taifa
Moja ya sababu kubwa Sana ya matatizo na Changamoto nyingi ya nchi yetu ufisadi ,Rushwa , huduma mbovu ni
Kukosekana kwa uzalendo NDANI ya wananchi
Hatari ni kwamba tunaanda kundi lingine la watu wanaitwa machawa ambao wanachoangalia ni maslahi yao binafsi wanayoyapata KUTOKA kwa Viongozi husika,
Watu wa namna hii wako tayari kuuza nchi wakishirikiana na viongozi bila kujali
Nimekuwa nikifiri ni namna gani tuandae Taifa la wazalendo kwenye kizazi chetu hiki na baadae Ila bado naona Kuna kazi kubwa Sana
Baada ya kuona hata vijana wanaotoka JKT bado hawajaonyesha uzalendo unafikiri nini kifanyike kuandaa kizazi Cha wazalendo