Uzalendo kwa taifa lako sio kusifu tuu na kusifia, hakika najivunia kuwa mzalendo katika taifa langu

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
520
2,929
Matukio 10, niliyoyafanya 2017 yakaleta athari (impact 2017) katika jamii yangu

1.Ni juu ya madawa ya kulevya siku ,nakumbuka tarehe 4 na tare 5 mwezi wa kwanza nilitenga siku hizi 2,kufanya uchunguzi mdogo juu ya athari za madawa ya kulevya katika maeneo ya mwananyamala.nilivaa nguo kama teja(mtumiaji),nilipata taarifa nyingi na kujua hao wanaouza kwa reja reja wanatoa wapi!,nilifika hadi kituo cha polisi,nilifika hadi kwa wakazi na wazazi kuwasikia.

Siku 2 baadaye nilipata muda wa kuongea ITV Malumbano ya hoja,niliyoyaona Mwananyamala kuwa hali ni mbaya Tanzania, hatua stahiki zichukuliwe.MATOKEO YAKE Mh.Mkuu wa mkoa Paul Makonda akaanza kutangaza vita juu ya Madawa ya kulevya.

2.Tukio lingine ni kupata taarifa juu ya Hospital ya MOI wagonjwa kuteseka kutofanyiwa surgery (upasuaji wa Mgongo)sababu ya ubovu wa kitanda cha upasuaji Mgongo,niliandika taarifa hiyo nikaisambaza,MATOKEO YAKE,Mh.Naibu wazir wa Afya aliona ujumbe wangu na akanijibu akanipigia kuwa analifanyia kazi siku ya pili akanifahamisha kitanda tayari kimetengezwa tayari,hivyo wagonjwa wakaendelea fanyiwa upasuaji na kupata huduma.

3.Wanafunzi wa stashahada wa CBE ambao kwa Muda walikuwa wanasumbuliwa kutopewa AVN ,ili kuomba chuo,niliandika taarifa ,Mh.waziri Mama Ndalichako alinipigia akasema amepata ujumbe na akanikabidhi kwa Naibu katibu wa elimu tuwe tunawasiliana,Mh.Ave Marie Semakafu.MATOKEO YAKE wanafunzi walipata AVN wote.

4.Tukio lingine ni Dereva wa Daladala ya kariakoo alitaka sababisha ajali alipokuwa anavaa sare zao kipindi gari likiwa kasi,nilipomwambia kama abiria kunitukana saana nisimfundishe kazi,na kuniambia kuwa Mimi nafanana na machinga,gari lilifika mawasiliano nikachukua plate number ya Gari ,nikapeleka kituoni ,Askari waliporudi hawakulikuta gari kesho yake SAA 12 asubuhi nikarudi,MATOKEO : likakamatwa na kutozwa faini ya elf 60,na wiki hiyo hiyo ITV katika kipindi cha Malumbano ya hoja ,mada Ajali barabarani,mbele ya ma afisa usalama barabarani Makao makuu nililishitaki tena lilegari,Dereva tuliwahi onana nae akasema ameacha Tania yake ya kuendesha gari hovyo hovyo.

5.Tukio lingine ni baada ya kupata taarifa juu ya Wanafunzi wa UMBWE High school Kilimanjaro, kulipishwa fedha laki 1.sababu ya kuchafua mazingira walipomaliza shule kidato cha sita ndio wapewe Vyeti vyao,MATOKEO ,niliandika taarifa juu ya suala hili nilipigiwa simu na kiongozi akijitambulisha anatoka TAMISEMI kuwa suala hilo linafanyiwa kazi ,pia uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro wakanifahamisha suala langu limefanyiwa kazi,tayari wameagiza wakaguzi na Wanafunzi hawatalipa chochote watapewa vyeti hivyo free.

6.Tukio jingine ,ni kuwa niliwahi pata wazo la kufungua ONLINE LIBRARY (E-library) ,MAKTABA YA MTANDAONI,ambapo niliunda group la whaatsp ,nikaweka sheria nikaadi watu ,MATOKEO,nilifanikiwa 100%kwani hadi sasa watu huongeza maarifa kupitia group hilo la maktaba ,kuna watu aina mbalimbali Mawaziri,Wanafunzi, wabunge,ma lecturer, maprofessor,wanasheria,wafanya biashara,waandishi wa habari,waandishi wa vitabu.Nafarijika saana.

7.Tukio lingine ni hili linalohusu Udahili wa Wanafunzi wa chuo Cha MWECAU,karibuni wana 800 walitakiwa kusitishiwa udahili program ya BED,MATOKEO niliwasiliana na wizara ya Elimu ,Mh.Naibu waziri wa Elimu Ole Nash.alinisaidia na kutoa maagizo Wanafunzi waendelee kusoma. Kwani ni makosa ya chuo.hivyo Wanafunzi wengi walirudi chuo.

8.Suala lingine,ni kuhusu wafanya kazi wa madini,(wakaguzi wadogo wa madini na madini ujenzi)waliokuwa Wanafanya kazi katika katika wakati mgumu,saana na kusainishwa mikataba mibovu,na Rushwa kukithiri kwa maafisa madini baadhi wa kanda,nakumbuka nilitafuta taarifa nakuanza kulitafutia ufumbuzi suala hili,kesho yake asubuhi baada ya Mh.waziri Angella Kairuki kuona taarifa yangu,Alinialika ofisini kwake,nikabahatika kuonana na Kamishna wa Madini,na Naibu waziri wa madini nikampa Concerns zangu,MATOKEO alifanikisha kuyafanyia kazi malalamiko yalio kuwepo na waliokuwa na waliokuwa na shutma ya ufisadi na Rushwa baada ya uchunguzi wao walifukuzwa.

9.suala kubwa lingine ni juu ya mikopo elimu ya juu na Udahili nafurahi saana nimeshiriki kikamili,kutoa taadhari kabla ya udahili kuanza,kipindi cha udahili na baada ya Udahili wa Wanafunzi, MATOKEO mengi ambayo nilikuwa nikiyatahadharisha TCU walikuwa wakiyapokea na kuyafanyia kazi.

Mikopo,kwa kushirikiana na TSNP Nimeshiriki kikamilifu kuweka pressure kubwa kwa bodi ya mikopo elimu ya juu Mwaka huu,MATOKEO: mbali na idadi ya waliotakiwa pewa elf 30,kulikuwa na niongeza ya wanafunzi kama elf 1000 mbali na Wanafunzi elf 30,mwaka huu Rufaa zimewahi toka mapema saana,na nusu ya waliokata rufaa wamepata mkopo.nawashukuru saana *EATV*(Hotmix),East African Radio *ITV* *AZAM TV* *CHANEL TEN* *MAGIC FM* *CLOUDS TV*, *CLOUDS Radio* *MILLARD AYO* *THE CITIZEN* Na wengine ambao sijawataja mmefanikisha saana kutimiza na kusaidia sauti za Wanafunzi kusikika.

10..Suala lingine ni juu ya Wanafunzi 24 kidato cha sita wa PUGU ambao walifukuzwa shule ,kwa kile kinachodaiwa kuvunja sheria za shule ,nilianza fuatilia suala hili na kupeleleza nikapata ushahidi ambao bado hautakiwi kuwekwa wazi. MATOKEO YA AWALI., nilipata kuwasiliana na Naibu katibu wizara ya Elimu Mh.Ave Ade Maria semakafu Akaniahidi kufika pugu Sekondari ,akafika na juzi j.NNE akanipa Majibu kuwa ameongea na bodi kuwa imepunguza adhabu Wanafunzi hao wataruhusiwa kufanya mtihani tuu na sio kusomea hapo,juzi j.Tank nimekutana na wazazi wa Wanafunzi hao 24 tukaongea nao.Ni kwamba kwa upelelezi wangu kupitia idara yetu haki na wajibu wa Wanafunzi TSNP, nikuwa wizara na Tamisemi kuna taarifa nyeti za kuhusu Mkuu wa shule ya pugu hawana ,namalizia uchunguzi na nitaenda kuwakabidhi juu ya yanayoendelea pugu.lengo ni Wanafunzi hawa wote warudi shule kusoma na kufanyia mtihani.kuna uozo unaoendelea ambao wizara wala TAMISEMI hawajui ,hili ndio tukio nimepanga kumaliza nalo mwaka.

Abdul Nondo.
Mungu atupe Afya Njema sote kuona na kuanza na mwaka ungine kwa Amani na upendo,na Afya njema.

Tafadhali,Kwa ushauri na maoni zaidi: 0659366125.
0762082783.
Abdulnondo10@gmail.com

Shukrani:

Shukrani zangu za dhati ziende kwa Mungu aliyejuu kwa kunipa Afya na Uzima hadi sasa nipo hai,kwa kunilinda hadi sasa.

uongozi wangu Mzima wa TSNP Kwa support wanayonipa.

Wazazi wangu kwa ushauri wanaonipa na kunitia moyo,

Walimu wangu wa political science UDSM kwa maarifa yanayo nijaza ujasiri kila siku.

Wanafunzi wenzangu wa UDSM na marafiki zangu wa karibu kwa kunipa moyo na hamasa ya kutovunjika Moyo.

Rafiki zangu kupitia mitandao ya kijamii pia ,ambao wamekuwa mstari wa mbele kunishauri na kuwa na mahusiano mazuri.

Hakika nafarijika,Namaliza Mwaka 2017 Nikiwa na Amani Moyoni saana .Mungu aendelee kunilinda na kunipa Afya Njema.kufanya mengi zaidi 2018,kwaniaba ya jamii yangu.
 
Back
Top Bottom