Hamduni
Senior Member
- Apr 25, 2020
- 169
- 117
🗓️ 26 Machi, 2024
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu. Mary Chatanda kwa pamoja wametimiza ahadi yao kwa kumpatia Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kiasi cha Tsh Milioni 2,000,000/= kwaajili ya kuchukulia fomu ya kugombea nafasi ya Urais ifikapo mwaka 2025.
UWT wamefanya hivyo ikiwa ni ishara ya kukubali na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025 kwa kishindo kikubwa katika miaka 3 ya uongozi wake tangu mwaka 2021 - 2024.
Fedha hizo wamezikabidhi kwa Ndugu. Issa Haji Gavu ambaye ni Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni wa CCM Taifa, aliyekuwa Mgeni rasmi katika Kongamano la Kumshukuru Rais Samia lililofanyika katika Ukumbi wa Mkuki House Jijini Dar es salaam.