Uwindaji wa kuua wanyamapori upigwe marufuku

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
Namshauri Meja Generali Gaudence Milanzi katibu mkuu wizara ya mali asili na utalii aanze kupiga vita ujangili kwa kupiga marufuku uwindaji wa kitalii wa kuua wanyamapori na badala yake ahamasishe upigaji wa picha tu. Kampuni moja kubwa ya Arusha TGT imeanza kupiga picha badala ya kuua wanyamapori na inatengeneza faida kubwa kwa kuuza hizo picha. Mamlaka mpya ya wanyamapori inaweza kufanya kazi ya Upunguzaji (cropping) wanyamapori wanaozidi maeneo ya malisho. Kazi hii ilikuwa ikifanywa na TAWICO ambayo ilibinafsishwa kifisadi.
 
Japo unajifanya mtoto wa mama,katibu mkuu ni mtendaji tu,hata bungeni hasimami wala hatakuwepo kujibu maswali.
 
Unachosema ni sawa itaisaidia sana wildlife conservation. Lakini vile vile idadi ya watu imeongezeka kwenye maeneo ya mbugani na kusababisha huwaribifu mkubwa wa mazingira ambayo wananyama wanategemea. Ukataji wa miti kwa ajili ya mikaa na mbao,uvamizi wa arthi za mbugani.
 

Daaaah! Nimemisi nyama za porini kavu za TAWICO.
 
Japo unajifanya mtoto wa mama,katibu mkuu ni mtendaji tu,hata bungeni hasimami wala hatakuwepo kujibu maswali.

Wewe vipi? Hujui kuwa wataalamu (wakurugenzi) wote wa wizara wako chini ya katibu mkuu? Akifanya kikao cha tathmini nao kwa nia ya kumshauri rais ili muswada upelekwe bungeni ni jambo linalowezekana na bunge litafanya mabadiliko ya sheria haraka sana.
 

Vitu vingine havipo tu kwakuwa vipo mkuu, kinachofanyika ni wildlife curling, ambayo inaruhusiwa ki ecologia na kihifadhi, uhifadhi maana yake ni kutumia kwa maendeleo endelevu........... na sio kuacha rasili mali hizo intact, ukiruhusu uwindaji, unapata fedha kwa ajili ya kuendesha mbuga na kuimarisha ujirani mwema, na uhifadhi .

Hata hivyo kuna wanyama ambao wako listed kwenye SITES appendix 1 ambao utalii wowote wa ku wa consume umekatazwa, kuna wanyama inabidi wawindwe sana kwa msimu ili kuimarisha ecologia ya maeneo husika..... baada ya mbuga kuwa na wanyama wachache sana inatunzwa na uwindaji unasimamishwa kabisa na inafanywa kuwa NP na hii ni kama ina sifa za kipekee au rasilimali za kipekee... mfano wake ni Saadani NP au Mkomazi NP......
 
Uwindaji uendelee ili kuongeza pato la taifa ila big five wasiuwawe mpaka watapoongezeka na kuanza kuharibu misitu.
Ni lazima kuwe na balance wasizaliane wengi sana.

Ila gharama za uwindaji uongezeke mara mbili na muda wa uwindaji upunguzwe. Hunting season ipo duniani kote na wakati wa breeding period iwe marufuku. Pia wawe specific kwa wanyama gani wa kuwindwa.

Waziri atoe mwongozo na tujue ni idadi ngapi ya wanyama tunao na wanaongezeka kwa asilimia ngapi
 
Wale faru weupe wa mkomazi sijui khabari zake au nao waliisha?kama kumbukumbu zangu zipo sahihi waliletwa kupandikizwa pale mwenye uelewa zaidi anijuze.
 

Kwa taarifa yako fedha zinazolipwa na professional hunters ni kidogo sana na uthibiti ni mgumu kwani ufisadi umetamalaki huko. Game rangers wanarubuniwa na idadi ya wanyama iliyoko kwenye vibali haithibitiwi! Curling inaweza kufanywa na mamlaka mpya ya wanyamapori. Hao wanaua wanyamapori wapewe leseni za kupiga picha na kama hawataki wabunge virago. Huko unakusema hunting iko duniani kote wanyama wamepungua sana ndiyo maana wataliI wameongezeka sana kwetu.
 

Sikiliza ndugu nimefanya kazi Selous muda mrefu sana.... uwindaji ndio unaoingizia fedha nyingi sana serikali, pesa inayolipwa na Ph ni kwa ajili ya permit ila gharama za kuwinda mtalii analipa moja kwa moja na anakuja na kibali porini..........
Kuhusu wanyama kupungua sio issue hata kidogo ikizingatiwa tu kuwa hao wanyama sio endangered...... mfano ma buffalo... hata uwinde vipi hayaish tena ni bora yawindwe, gazelles, zebras, Kudus.... hata Leopards, Lions, Elephants wanaowindwa hunting season ni wachache sana ukizngatia na hao wanaouwawa kwa ujangili...............

Unatakiwa pia uelewe kuwa wanyama hawakai mahali pamoja milele... wanahama kwa ajili ya malisho, makazi na mambo mengine kwa kutumia wildlife corridors...... sasa nyie msipowinda.. Zambia watawinda, Botswana watawinda, Kenya watawinda etc.... ndio maana biashara ya wanyama duniani ipo controlled na CITES maana wanyama hawana geographical boundaries...
 

Acha uwongo, Kenya banned professional hunting in 1977, Uganda in 2010, Botswana in 2013. Just Google and search national geographic. Tanzania tu ndiyo tumebaki na wanyama wengi na tusipochukua hatua sasa utalii kwa heri. Wanaotetea professional hunting ni mafisadi uchwara wa hapa kwetu na mafisadi papa waliomaliza wanyamapori huko kwao. Majangiri nao wanatumia huo mwanya wa vibali. Tukiendelea kuwasikiliza mnaojifanya wataalam hata utalii utakufa kwani hatutakuwa na vivutio. Pia nimesema TAWA wafanye curling nasi tule nyama pori kama enzi za TAWICO.
 
Last edited:
Hivi huyu Meja Generali Gaudence Milanzi katibu mkuu wizara ya mali asili na utalii ana uelewa wo wote wa mambo ya wanyamapori kweli? au kawekwa tu basi
 
Una uhakika na ulichokiandika ?
 
8
Una uhakika na ulichokiandika ?[/

QUOTE
Una uhakika na ulichokiandika ?

Uhakika wa kuwa katika Afrika uwindaji umebaki Afrika kusini, Zimbabwe na Tanzania ninao. Pia kama hao wawindaji halali wanapiga vita ujangili mbona hawajamkamata hata jangili papa mmoja? Jibu ni kuwa majangili nao wanawinda katika miezi ile iliyoruhusiwa kwa hiyo ukisikia mlio wa bunduki huwezi kutofautisha wa jangili na wa professional hunter. Dawa ni kuondoa kabisa milio ya bunduki kwenye mbuga zetu.
 

Uwindaji wa kitalii sio kichocheo cha ujangali kama usimamizi wa wanyamapori ni madhubuti. Kenya ilipiga marufuku aina yoyote ya uwinbdaji mwaka 1975 hadi sasa lakini idadi ya wanyama inazidi kupungua hasa "The big five" yaani Tembo, faru, simba, chui na nyati kutokana na ujangili. Kuna wakati Zambia na Zimbabwe walifunga uwindaji lakini baadaye wakafungua. Ada ya uwindaji wa kitalii kwa mnyama moja katika the big five ukiacha faru ni kama ifuatavyo Tembo $ 15,000, Simba $ 4,900, Chui $ 3,500 na Nyati $ 2,375. Uwindaji wa kitalii huingiza mapato sawa au zaidi ya utalii wa picha ambao una adhari kubwa ya mazingira na usumbufu kwa wanyama. Utakuta simba au faru amezungukwa na magari mengi mpaka anashindwa kula au kupumzika. Changamoto iliyopo kwenye uhifadhi wa wanyamapori ni ujangili unaofanywa bila kujali ni hifadhi ya taifa au pori tengefu. Changamoto ingine ni takwimu hafifu kuhusu idadi ya wanyama wa kuwindwa katika kitalu husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…