Alfredi julius
New Member
- May 2, 2024
- 1
- 2
Soya ni zao jamii ya mboga mboga ambayo ni jamii ya mikunde, maaragwe.Hii ni nafaka ambayo hulimwa baadhi ya mikoa nchini Tanzania na hata nje ya nchi pia, mfano baadhi ya mikoa ni Tabora na Singida. Soya ni miongoni mwa mazao ya biashara ambayo kwa sasa yanafanya vzr sokoni kutokana na ongezeko la mahitaji na faida nyingi ya zao hili nchini na nje ya nchi.
Faida ambazo zipo katika zao la soya ni mafuta ya kupikia hii moja ya zao la soya kupata mafuta ya kupikia ambayo ni Bora kwa matumizi ya mwanadamu lakini pia hata kwa wanyama pia huweza kuwapa mafuta haya kwa kuchanganya kwenye chakula chao wakati wa kula.
Faida nyingine ni zile pumba baada ya kukamuliwa mafuta hutumika kutengenezea chakula Cha mifugo mfano,kuku,ngurue,mbuzi na ng'ombe na kina vitamini Sana kwa wanyama kwani wanyama hukua haraka na kuzaliana kwa haraka Sana.
Tanzania tuitakayo ni ombi kwa serikali, kuna viwanda vingi ambavyo vinahitaji hii nafaka kwa ajiri ya uzalishaji wa mafuta cha chakula cha mifugo, na hii nafaka mara nyingi hutoka zambia,malawi kutokana na Tanzania kutolipa kipaumbele zao hili ni lazima serikali iandae mikakati maalumu kwa ajiri ya kuweza kuendeleza zao hili ili kuweza kuongeza kipato kwa wananchi na pato la serikali kutokana na ongezeko la uhitaji hapa nchini,mfano baadhi ya viwanda ambvyo wanahitjai sana hili zao katika uzalishaji wao ni INTERNATIONAL TANFEEDS mkoani morogoro mjini,SILVERLAND FEEDS na SHAFA mkoani Iringa hivi ni baadhi ya viwanda ambvyo vinahitaji Sana soya katika uzalishaji wake wa bidhaa.
Ombi kwa serikali hasa wizara ya kilimo pia kutenga bajeti ya kilimo na kutenga ardhi na miundombinu ili iweze kufikika ili kuweza kukuza zao nchini, lakini pia kuunda makundi ya vijana na kuwapa ardhi na mikopo pia yenye masharti nafuu ili kuweza kulikuza zao la soya hap nchini.
Upatikanaji wa mbegu za kisasa na zenye ubora hii pia itachangia ongezeko la uzalishaji kua mkubwa na kuongezeka kwa kipato kwani kama uzalishaji utakua mkubwa pato litakua kubwa na kupunguza lalamiko la ajira kwa wananchi hasa vijana ambao wanamaliza elimu zao za juu na kukosa ajira.
Ijengwe miundombinu ya umwagiliaji hii itafanya uwepo wa uhakika wa hili zao la soya kwani kama kutakua na uhakika wa hili zao basi kutaongeza kasi ya uzalishaji na pesa nyingi itabaki ndani ya nchi tofauti na Sasa ambapo pesa nyingi inakwenda nje ya nchi kutokana na uzalishaji wake kua mdogo sana.
Soya ni miongoni mwa mazao ambayo bei yake mara nyingi huwa juu kufika hadi kilo moja kuuzwa hadi shilingi elfu mbili ya kitanzania hivyo ni fursa kwa serikali kuona kuna haja ya kuwekeza hapa katika zao la soya hapa nchini na ukiangalia jamii nyingi kwa sasa watu wameingia katika ufugaji hivyo ni lazima kuwe na uhakika wa kupata chakula kwa ajiri ya mifugo yao na kuendeleza kutengeneza mnyororo wa thamani na kuongezeka kwa ajira nchini.
Lakini pia serikali inaweza kuwekeza yenyewe kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaweza kukuza hili zao kwa haraka kwani itakua na uwezo wa kusimamia kwani tumeona serikali imeweza kusimamia zao la chikichi,mkonge,tumbaku,basi wanaweza pia kuanzisha hata vyama vya ushirika ili kuweza kukuza zao hili kwani lina manufaa mengi Sana nchini na duniani.
Serikali iandae wataalamu maalumu wa hili zao la soya; kama serikali inaweza kuaandaa wataalamu wa hili zao ili kuweza kupeleka elimu kwa wakulima namna ya ulimaji wa kisasa ili kuongeza kipato, serikali inaweza kutoa hata kozi za muda mfupi kwa maafisa kilimo ili wakawasidie wakulima vijijini na huo uwezo upo sababu tumeona kuna chuo Kama Sokoine University of Agriculture (SUA) mkoani morogoro wanatoa elimu ya kilimo na ufugaji pia na wanatoa wataalamu wengi ambao wanasaidia hili taifa la Tanzania hivyo ni vizuri serikali iandae wataalamu maalumu wa zao la soya hii itasaidia kukuza zao la soya nchini Tanzania.
Kwa hiyo ili tuweze fanya mabadiliko nchini na Tanzania tuitakayo serikali inaweza kuyatazama mawazo yangu kwani yamelenga kusaidia jamii ya watanzania wote kwa upande wa zao la soya na kwa wakulima ili kuweza kukuza maisha ya watu wote na kulipa nafasi hili zao kwani linaweza kua mkombozi kwa Tanzania na wananchi wake kwa ujumla, lakini pia kuna faida kwa wafugaji kwani chakula kitapatikana kwa urahisi na bei nzuri lakini pia hata mafuta ya kupikia pia yatapatkana kwa urahisi tofauti na Sasa yamekua kama ni mafuta ya watu wenye uwezo wa maisha kwa mtu mwenye hali ngumu ya maisha anashindwa kutumia kutokana na bei yake kua juu