Uwaziri Mkuu India ni wa muda gani?

and 300

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
26,325
36,124
Niliwahi kwenda India Juni 2014 Narendra Modi akiwa Waziri Mkuu, mpaka Leo 2024 jamaa bado Ni Waziri Mkuu. Wajuvi imekaaje hii?
 
Huu muhula wake wa 3 na utakamilika 2029. Amekuwa Waziri Mkuu tangu 2014 na ni wa pili kwa kuwa madarakani muda mrefu baada ya muasisi Jawaharlal Nehru.
 
Huu muhula wake wa 3 na utakamilika 2029. Amekuwa Waziri Mkuu tangu 2014 na ni wa pili kwa kuwa madarakani muda mrefu baada ya muasisi Jawaharlal Nehru.
Hawana ukomo wa Mihula wakichoka ndio kwaheri huyu Udini hasa sera za chama chake cha BJP za kupendelea ushindi na wakulima ndio kinampa ushindi japo ameituliza India kwa sasa

USSR
 
Uwaziri Mkuu nchini India hauna muda maalum ulioelezwa kikatiba. Waziri Mkuu anahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, kulingana na muda wa Baraza la Wawakilishi (Lok Sabha), lakini anaweza kuchaguliwa tena mara nyingi kadiri chama chake kinavyoshinda uchaguzi mkuu. Kwa hivyo, Waziri Mkuu anaweza kuhudumu kwa kipindi cha miaka mingi, mradi tu chama chake kinapata idadi ya kutosha ya viti katika Lok Sabha na anaungwa mkono na wingi wa wabunge.
 
Niliwahi kwenda India Juni 2014 Narendra Modi akiwa Waziri Mkuu, mpaka Leo 2024 jamaa bado Ni Waziri Mkuu. Wajuvi imekaaje hii?
As long as you can comand majority in thelower houseof parliament known as Lokh Sabha
 
Back
Top Bottom