Uwanja wa Ndege wa Mwanza utabeba Abiria wa Kigeni 200

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,561
1,590
Nimefuatilia kwa umakini hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa jengo la abiria Mwanza linalokusudia kuifanya Mwanza Airport kuwa International ifikapo desemba 2024 by ICAO standards.

Kwenye maelezo ya Bw Mbura DG jengo hili litabeba watu 200 kutoka nje ya nchi(international pax)kwa mkupuo, uwanja utakapokuwa wa kimataifa.

Hii ni danganya toto, iwapo kweli serikali imekusudia uwanja huu kuufanya kuwa na vigezo vya kimataifa pamoja na miundo na mifumo itakayowekwa idadi ya wageni wanaohudumiwa kwa mkupuo waingiapo kuwa 200 tu ni kuupunguza hadhi uwanja unaolengwa kuwa wa kimataifa.

Iongezwe hadi 300. Tumetembea viwanja vingi ndege moja ya dreamliner ikitua baadhi ya wageni lazima wabaki nje wanyeshewe mvua hii si haki, ndege mbili zikiingia zenye abiria 200 kila moja ndege nyingine itashindwa kutelemsha abiria.hili liangalieni na ikiwezekana wekeni variation ili upanuzi ufanyike.

mliahidi kufanya re-design ya jengo, kulikoni? kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa na mlikiri kuwa lilikosewa, sasa mnarudi mlemle mwa wahandisi wa halmashauri !

Kumbukeni wananchi wanafuatilia kwa karibu suala la viwango nashauri bora mpunguze fedha za landscaping mpanue jengo.

Jengo la KIA na Songwe Airport pax capacity yake ikoje?Kwa hilo mmechemka. Ninawatakia ujenzi mwema.
 
Sasa hivi vimiradi vya hovyo vimeanza kurudi.

Uwanja wa mpira wa watu elfu 30 kwa gharama kubwa.

Uwanja wa ndege wa watu 200 kwa gharama kubwa
 
Je uwanja huu utapata kibali cha ICAO/IATA international codes kweli kuwa cha kimataifa. Tuache siasa kwenye uwanja huu. Mbona mnawapotezea wabunge na wananchi muda wao.DG Mbura tengeneza kitu kitakachoacha legacy na chenye kuakisi taaluma yako.
 
Mwanza kutua ndege ya watu 300 si leo, wageni weengi Mwanza kutafuta Nini? hayo majengo mengine yatajengwa baadae kwasasa hilo linawafaa.
Waskuma msipende makuu yasiyo na tija
 
Ule uwanja wa ndege chato ulitakiwa kujengwa Mwanza, na ule wa Mwanza wa awali kujengwa Bukoba, yule muuza furu na maziwa akaenda kujenga uwanja wa ndege kwenye mashamba ya baba yake
 
Dreamliner inabeba abiria wangapi?
Sina hakika ya takwimu ila nakumbuka niliwahi kushuka hapo Mwanza na ile Airbus zile kubwa, nadhani tulikuwa abiria zaidi ya 180 kama sijakosea


Maana ilikuwa upande wa Kulia tulikuwa tunakaa abiria 3 watatu wakati upande wa kushoto ilikuwa wanakaa abiria wawili wawili
 
Sina hakika ya takwimu ila nakumbuka niliwahi kushuka hapo Mwanza na ile Airbus zile kubwa, nadhani tulikuwa abiria zaidi ya 180 kama sijakosea


Maana ilikuwa upande wa Kulia tulikuwa tunakaa abiria 3 watatu wakati upande wa kushoto ilikuwa wanakaa abiria wawili wawili

Sasa kwa nini wajenge uwanja wa abiria 200?
 
Back
Top Bottom