Mtu anafanya madudu katika wadhifa aliopewa, na haoni kama anafanya madudu au anahisi ni haki yake. Hapo tu inaonesha jinsi asivyo na uzalendo, sasa unategemea atajiwajibisha aje ikiwa wala haoni kuwa analofanya si sahihi? Ni kweli pengine mwisho wa uongozi wa sasa tukarudi kwenye uozo tena, hapo ni sheria na uwajibikaji wa kila mtu na taasisi unahitajiwa.