Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,583
- 1,189
UVCCM MOROGORO WAHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA WA SERIKALI ZA MITAA
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Mkoa wa Morogoro (UVCCM) wametembelea Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro kwa lengo kubwa la kuhamasisha Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa ambapo zoezi hili limeanza tarehe 11 - 20 Oktoba, 2024 nchini kote.
Ziara ya Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Morogoro iliongozwa na Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Morogoro, Ndugu Mwinshehe Adam Yange; Katibu wa UVCCM Mkoa wa Morogoro, Ndugu Violeth Emmanuel Soka; Wajumbe wa Baraza, Wenyeviti na Makatibu wa Wilaya husika; Wenyeviti na Makatibu wa UVCCM wa Kata husika.
Viongozi wa UVCCM Mkoa wa Morogoro walitembelea na Kuhamasisha wananchi wote Mkoa wa Morogoro kujiandikisha katika Wilaya ya Mvomero, Wilaya ya Gairo, Wilaya ya Kilosa - Mikumi, Wilaya ya Ulanga - Lupilo, Wilaya ya Malinyi, Wilaya ya Morogoro Vijijini na Wilaya ya Morogoro Mjini.
Aidha, ziara ya Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Morogoro ilihitimishwa Wilaya ya Morogoro Mjini kwa kutembelea maeneo mbalimbali na kuzungumza na makundi mbalimbali ili kutumia siku moja iliyobaki kwenda kujiandikisha ili wapate haki ya kikatiba ya kupiga kura kuchagua viongozi wanawaotaka ifikapo tarehe 27 Novemba, 2024.
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-10-19 at 23.31.51(1).jpeg162.5 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2024-10-19 at 23.31.52(2).jpeg138 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2024-10-19 at 23.31.52(3).jpeg192.7 KB · Views: 2
-
Screenshot 2024-10-20 at 00-35-08 Violeth Emmanuel Soka (@violetsoka) • Instagram photos and v...png793.8 KB · Views: 2
-
Screenshot 2024-10-20 at 00-35-28 Violeth Emmanuel Soka (@violetsoka) • Instagram photos and v...png989.3 KB · Views: 2
-
Screenshot 2024-10-20 at 00-36-14 Violeth Emmanuel Soka (@violetsoka) • Instagram photos and v...png928.5 KB · Views: 2
-
Screenshot 2024-10-20 at 00-37-39 Violeth Emmanuel Soka (@violetsoka) • Instagram photos and v...png924.6 KB · Views: 2
-
Screenshot 2024-10-20 at 00-40-21 Violeth Emmanuel Soka (@violetsoka) • Instagram photos and v...png761.7 KB · Views: 2
-
Screenshot 2024-10-20 at 00-41-30 Violeth Emmanuel Soka (@violetsoka) • Instagram photos and v...png1 MB · Views: 2
-
Screenshot 2024-10-20 at 00-43-17 Violeth Emmanuel Soka (@violetsoka) • Instagram photos and v...png1.1 MB · Views: 2
-
Screenshot 2024-10-20 at 00-43-17 Violeth Emmanuel Soka (@violetsoka) • Instagram photos and v...png1.1 MB · Views: 2
-
Screenshot 2024-10-20 at 00-43-45 Violeth Emmanuel Soka (@violetsoka) • Instagram photos and v...png1 MB · Views: 2
-
Screenshot 2024-10-20 at 00-46-44 Violeth Emmanuel Soka (@violetsoka) • Instagram photos and v...png558.5 KB · Views: 2