Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,685
- 1,235
UVCCM KUENDELEA KUENZI MAHUSIANO YA KIDUGU YA CPC YA CHINA NA CHAMA CHA MAPINDUZI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amekutana na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian, tarehe 07 Mei 2024 Ofisi za Ubalozi wa China Tanzania na kufanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali yanayohusu uhusiano na urafiki wa kidugu kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Tanzania na China, lakini pia fursa Mbalimbali za Vijana wa Tanzania nchini China.
Komredi Kawaida Amemuwakikisha Balozi wa China kuwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wataendelea kuenzi na kudumisha Mahusiano wa kidugu na ya muda Mrefu kati ya CCM na CPC lakini pia Tanzania na China.
Katika Msafara wake Komredi Kawaida aliambatana na Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa Komredi Emmanuel Martine na Mkuu wa Idara ya Uwezeshaji Uchumi na Fedha Komredi Ali Issa Pamoja na Baadhi ya Maafisa UVCCM Makao Makuu.
#Diplomasia
#CPC&CCM
#KulindaNaKujengaUjamaa
Imetolewa na
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM-Taifa