Utumishi leo wamenizuia kufanya online written interview

Ujuja

Member
Jul 15, 2024
23
21
Habari wakuu, mimi ni mtanzania mwenye miaka 29. Leo nimeenda kufanya interview ya forest officer II chini ya TFS kituo kikiwa chuo cha TIA.

Jambo la kushangaza watu wa utumishi wamenizuia kufanya kwa sababu wanasema mpaka mda ambao nitaitwa kazini (Ikitokea nimepata) nitakuwa na miaka 30, kikomo cha umri ambao TFS waliandika kwenye tangazo lao la kazi ("applicants should be not above 30).

Wakuu hii imekaaje? maana naona kama ni uonevu hivi kwa sababu kuanzia Written hadi kufanya oral (26/03) bado nitakuwa na miaka 29 bado.

Naombeni wakuu wangu, kaka zangu, dada zangu, mama zangu na baba zangu mnisaidie. Najua humu watakuwepo watu wakubwa tu wenye uwezo wa kuingilia kati hili swala. Kama kuna mwenye uwezo naomba nimfate PM maana hii ndio ilikuwa interview yangu ya kwanza na ya mwisho kwa TFS maana nimesoma bachelor of science in forestry 🙏.
 
Ni sahihi, hukutakiwa kufanya, kwasababu miaka 29 uliitimiza mwaka jana 8/May/2024 baada ya hio hutokuwa na miaka 29. Refer watu wenye miaka 59 wanapofikisha 60 ni immediately wanastaafu, maana siku moja baada ya kutimiza miaka 60 hatohesabika kama ana 60 tena
 
Jambo la kushangaza watu wa utumishi wamenizuia kufanya kwa sababu wanasema mpaka mda ambao nitaitwa kazini (Ikitokea nimepata),,,,Sasa Utaitwaje Kazini Kama Walikuzuia Kufanya Hiyo Intavyuu?
 
Pole aisee fanya tu mambo mengine sio lazima uwe serikalini. Hiyo field yenu sasa hv ina hela sana ukijua jinsi ya kucheza na taasisi za kimataifa
 
Jambo la kushangaza watu wa utumishi wamenizuia kufanya kwa sababu wanasema mpaka mda ambao nitaitwa kazini (Ikitokea nimepata),,,,Sasa Utaitwaje Kazini Kama Walikuzuia Kufanya Hiyo Intavyuu?
Hapo hata mimi nilikuwa nawabana kwa kusema kwamba, mna uhakika gani kuwa nitafaulu huu mtihani? nikifeli je... nia yangu ilikuwa nifanye written tu ila wakakaza
Jambo la kushangaza watu wa utumishi wamenizuia kufanya kwa sababu wanasema mpaka mda ambao nitaitwa kazini (Ikitokea nimepata),,,,Sasa Utaitwaje Kazini Kama Walikuzuia Kufanya Hiyo Intavyuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…