KERO Utozwaji wa Nauli kinyume na Nauli zilivyoelekezwa na mamlaka (LATRA)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ma agent wa mabasi hasa yamikoani wanatoza abiria nauli ambazo ni kinyume na nauli elekezi.

Kwa mfano Nauli rasmi kutoka mkoani Gieta kwenda Kibondo (kigoma) kupitia nyakanazi ni Tshs. 17000/= Lakini makampuni ya mabasi kupitia ma agenti wao kutoka eneo hilo wanatoza nauli Tshs.22,000/= kinyume na nauli za mamlaka.

Na bado makampuni hayo yanatumia ticketi Zao za zamani (vitabu) na sio ticketi mtandao kama inavyotakiwa na mamlaka.

huku abiria wanaokaa mbele ndio wanaopatiwa ticketi za mtandao ambazo Nauli iliyoandikwa ni tofauti na nauli inayolipwa.

Mfano ni kampuni ya mabasi ya ALHAMDULLILAH (Mwanza-geita-Nyakanazi-kibondo)
 
Kula urefu kwa kamba yako mkuu bi Chura aliposema hili we hukuwepo kikaoni
 
Latra wako ofisini wanakula AC tu. Kwenye njia y vumbi au lami kufanya nn?
 
Back
Top Bottom