Mtandao wa habari wa Uingereza “Middle East Eye” hivi karibuni ulitoa makala iliyopewa jina la “Jinsi Majeshi ya Marekani Yanavyoongeza Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi Duniani”, ikisema jeshi la Marekani ni moja ya vyanzo vikubwa vya utoaji wa hewa chafu duniani, na kama vikosi vya jeshi hilo ni vya nchi kavu, vitazidi zaidi ya nchi 130 duniani kwa utoaji wa hewa chafu.
Vita vinatoa uhai, na utoaji wa hewa chafu kwenye vita pia ni muuaji asiyeonekana, ambaye huzidisha mabadiliko ya hali ya hewa na kuharibu ikolojia ya dunia. Ikiwa nchi inayoongoza kwa kuanzisha vita duniani, Marekani imefanya operesheni 251 za kijeshi duniani katika miaka 30 iliyopita. Kwa mujibu wa takwimu za utafiti zilizotolewa na Taasisi ya Watson ya Chuo Kikuu cha Brown nchini Marekani, operesheni za kijeshi za Marekani nchini Afghanistan, Iraq na Syria pekee zimetoa zaidi ya tani milioni 400 za hewa chafu, ambayo ni kama utoaji wa hewa hiyo wa nchi 116 kwa mwaka. Zaidi ya hayo, Kwa mujibu wa ripoti ya “Afghanistan: Tathmini ya Mazingira Baada ya Vita” iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, vita vilivyoanzishwa na Marekani viliteketeza asilimia 40 hadi 70 ya misitu nchini Afghanistan. Katika Vita vya Ghuba, visima 788 vya mafuta vilichomwa moto, na mapipa milioni 800 ya mafuta yaliendelea kuwaka kwa miezi 9.
Mbali na mapigano vitani, kama nguvu kubwa zaidi ya kijeshi duniani, utoaji wa hewa chafu katika siku za kawaida wa jeshi la Marekani pia unatisha sana. Vifaru vyake aina ya M1 hutumia lita 1,600 za mafuta kwa kila kilomita 100 katika mafunzo ya kila siku, na ndege moja ya kurusha makombora ya masafa marefu aina ya “B-52” inatumia lita 12,000 za mafuta kwa saa. Miundombinu ya kijeshi ya Marekani pia inatoa kiasi kikubwa cha hewa chafu. Jeshi la Marekani lina miundombinu zaidi ya 560,000 duniani kote, ikiwa ni pamoja na zaidi ya majengo 275,000 katika vituo vyake 800 vya kijeshi. Katika mwaka wa fedha wa 2017 pekee, Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitumia dola bilioni 3.5 kwa umeme.
Kutokana na takwimu, mafuta yanayotumiwa na jeshi la Marekani yanachukua robo ya jumla ya matumizi ya mafuta ya Marekani, na matumizi ya mafuta ya Marekani pia yanachukua robo ya jumla ya matumizi ya mafuta duniani kote, ikimaanisha kwamba, jeshi la Marekani linatumia moja ya kumi na sita ya mafuta duniani.
Hata hivyo jeshi hilo limepewa madaraka maalum ya kuepusha jukumu la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Marekani imekuwa ikijaribu kimakusudi kushawishi jamii ya kimataifa kuzingatia utoaji wa hewa chafu wa viwandani na majumbani, na kuficha utoaji wa hewa chafu wa jeshi lake. Wanaharakati wa hali ya hewa kwa muda mrefu wametaka Marekani kuweka utoaji wa hewa chafu wa jeshi lake katika Ripoti ya Kitaifa ya Uzalishaji wa Hewa Chafu, lakini serikali ya Marekani haijafanya hivyo. Hata mwaka 1997, wakati jumuiya ya kimataifa ilipobuni Makubaliano ya Kyoto kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, ambayo inataka nchi 37 zilizoendelea kupunguza utoaji wa hewa chafu, Marekani ilidai msamaha wa kufichua utoaji wa hewa chafu wa jeshi lake kwa kisingizio cha “usalama wa taifa”.
Marekani husema itajiwajibika ipasavyo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, lakini ikiwa kweli inataka kufanya hivyo, inafaa kuacha kuanzisha vita mara kwa mara na kudumisha nguvu kubwa ya kijeshi, ili kupunguza utoaji wa hewa chafu.