Utitiri Wa Mabenki,Rushwa ya Mikopo na Athari kwa Taifa

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,172
1,074
Tanzania kwa sasa ina mabenki zaidi ya Hamsini..Ni mengi sana ukilinganisha na hali halisi ya afya ya kiuchumi.Mengine zaidi yapo katika mchakato wa kupata leseni..Mengi ya mabenki yaliopo hayasaidii kuwezesha wananchi zaidi ya kuwanyonya wananchi na kuwa chanzo cha kuwafukarisha kupitia bidhaa zisizo na tija au suruhu ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kipato ..Benki nyingi zimekuwa na urasimu sana sana katika kuwawezesha watanzania {wafanyabiashara,wakulima,wafanyakazi n.k} kupitia mikopo ya riba kubwa na makato makubwa ya wazi na ya siri ya huduma zitolewazo kila mara.

Baadhi ya benki kadhaa zina undugu wa karibu kiumiriki hivyo kusababisha mgongano wa maslahi ya nchi hasa katika masuala ya ulipaji kodi,udhibiti na uwajibikaji kimaadiri {kibiashara},baadhi ya mifano ya benki ndugu ni Barclays&NBC, and FNB&Stanbic..

Pia kuna Benki zenye kutuhumiwa kuhujumu uchumi hasa kwa kuruhusu mihamala ya mabilioni kufanyika kwa fedha taslimu kinyume na sheria za nchi pasipo uthibiti wenye umakini {Mfano Stanbic-Tegeta Esrcow,Egma etc}..lakini baadhi kutuhumiwa kuwa na mrengo wa kusaidia utoroshaji wa rasilimali fedha kwenda nje ya nchi {hasa benki toka nje ya Tanzania zenye kulenga mahitaji ya wananchi wa nchi zao kama experts,wafanyabiashara toka ktk mataifa zitokako-mfano Bank of India,Bank of Baroda,China Commercial Bank, etc }kama ambavyo baadhi ni tuhumiwa katika utakatishaji fedha haramu,kutuhumiwa kutumika kuwafikishia fedha watuhumiwa wa ugaidi mfano FBME etc...

Nadhani serikali yapaswa kufanya udhibiti makini na wa kina katika Bank zote kubaini ukiukwaji wa sheria na yamkini udhibiti makini na wakina.Uchumi wa nchi hauwezi kuimalika kwa mwendo huu,sarafu ya nchi haiwezi kuimarika kwa mianya ya udhoofishaji kuendelea kushamiri..Hatua madhubuti sana zapaswa kuchukuliwa hasa ukizingatia nchi iendako....

Mwisho ,Kuna mizizi ya utoaji huduma za msingi kwa rushwa hasa mikopo,na hili limekuwa likiwahusisha sana wafanyakazi wa mabenki katika vitengo vya mikopo,mameneja matawi,Maafisa mahusiano,maafisa biashara ,maafisa mauzo,wakuu wa vitengo vya mikopo {ukopaji}..Rushwa za asilimia 2,3,4,5,6,7,10 zimekuwa zikiombwa kufanikisha utoaji mikopo husika hivyo kuwabebesha mizigo mikubwa wakopaji na kusababisha wengi kushindwa kutimiza malengo yao ya msingi hivyo kushindwa kulipa mikopo husika.
 
Kuna mizizi ya utoaji huduma za msingi kwa rushwa hasa mikopo,na hili limekuwa likiwahusisha sana wafanyakazi wa mabenki katika vitengo vya mikopo,mameneja matawi,Maafisa mahusiano,maafisa biashara ,maafisa mauzo,wakuu wa vitengo vya mikopo {ukopaji}..Rushwa za asilimia 2,3,4,5,6,7,10 zimekuwa zikiombwa kufanikisha utoaji mikopo husika hivyo kuwabebesha mizigo mikubwa wakopaji na kusababisha wengi kushindwa kutimiza malengo yao ya msingi hivyo kushindwa kulipa mikopo husika.
 
kuna bank kama nmb tawi la mbeya. yaani jiji lote kitengo cha mikopo kipo tawi moja tu. huku si kutafuta rushwa kwa wateja?? ukienda pale asubuhi mpaka jioni hujafanikiwa hata kumuona huyo afisa mikopo.
hivi wanajua kuwa watu wana kazi nyingi za ujenzi wa taifa??
kwa nini wasiweke kitengo hicho na matawi mengine??
 
Huu uzi utasaidia sana kuanika ukweli, wito wangu kwa watu wote waliopata kufanyiwa ndivyo sivyo na hizi bank waweke mambo hadharani ili JPM raisi wetu mpendwa atumbue.
Ila Benno Ndulu kazi imemshinda, kuna benki wanakupa interest ya 3% kwa amana yako lakini wanakutoza 30% kwa mkopo, je interest rate Tanzania ni asilimia ngapi? Najua JPM hawezi kumtumbua Benno Ndulu kwa vile ni Ssebo wake na Likwelile lakini they have to put country first
 
Ni kweli baadhi ya wafanyakazi wa baadhi ya bank huomba rushwa ili kutoa mikopo. Suala hili suluhisho lake ni
1.Kutoa ripoti TAKUKURU
2. Kuhama benki huku ukishawishi na wengine kuhama
3. Kununua hisa kwenye benki za wananchi kama Mwalimu Benki n.k ili kuzisaidia kukusanya mtaji na kutoa huduma nzuri na bora.
 
Hata katika jiji la Mwanza utaratibu ni kama huu huu, mikopo yote hutolewa tawi la NMB Kenyatta Road na rushwa ni kama kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…