UTEUZI: Bw. Sylvester Joseph Kainda ateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania

Last Seen

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
229
566
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:

i) Amemteua Bw. Sylvester Joseph Kainda kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kainda alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.

ii) Amemteua Bi. Eva Kiaki Nkya kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bi. Nkya alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

iii) Amemteua Bw. Chiganga Mashauri Tengwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Tengwa alikuwa Naibu Msajili

Screenshot_20240403-173619_Instagram.jpg
 
Duuh, huu URAIS ni zaidi ya UFALME,..jamani, muda wa KATIBA MPYA BORA NI SASA..Rais abaki na mambo machache MAKUBWA
 
Pongezi kwa walio teuliwa.
Tunacho taka sisi raia ni haki itendeke.
Watende haki tu hilo ndio jambo la msingi.
 
Msajili mkuu wa mahalama vs. Msajili wa mahakama kuu!
Kuna mahakama ya rufaa na mahakama kuu. Thus kuna jaji mkuu anae saidiwa kazi na msajili mkuu, pia kuna mahakama kuu ambayo inaongizwa na jaji kiongozi akisaidiwa na msajili wa mahakama kuu
 
Teuzi juu ya teuzi,why hawa hawaombi na kufanyiwa usaili wa kuwa jaji?,tunakoenda huko hata Rais atatuteulia wenza wetu!,upo right kabisa mchangiaji hapo juu,awamu ya kwanza teuzi hizi hazikuwepo,hizi nafasi zimetengenezwa lini?
 
Back
Top Bottom