Wadau, amani iwe kwenu.
Ni dhahiri sasa kuwa CHADEMA wameshikwa pabaya. Wamekamatwa na wamekamatika. Sijawahi kuona nyeti ya jogoo ila kwa hapa walipofika CHADEMA hakika wanalazimika kuomba pooo.
Tuliwaambia kuwa dawa ya CHADEMA ni kwa CCM kuwa na kiongozi shupavu, anayejua mahitaji ya wananchi, mwenye ari ya kufanya kazi, mzalendo, asiye mnafiki na asiyevumilia madudu. Haya ni mambo ambayo kwa hakika yalikuwa yanakiangusha chama chetu kiasi ambacho wafuasi wake humu mitandaoni tulipata taabu kujieleza.
Sasa tunaye Rais Magufuli. Kwa hakika Mwenyezi Mungu amesikia dua zetu kwani katuletea mtu sahihi na kwa wakati muafaka.
Tulipoanza mapambano haya, ilikuwa ni taabu sana kwa mwana CCM kujitambulisha hadharani. Ila kwa sasa hali imebadilika. Makamanda wengi wamevua magwanda yao. Ijapokuwa hawajatangaza hadharani, ila ukweli ni kwamba Lowasa kawaangusha na Magufuli kawafurahisha. Baadhi ya wadau waliopotea humu ni pamoja na
- Dr Slaa
- Mungi
- Crashwise
- John Mnyika
- Michael Aweda
- Henry Kilewo
- Godbless Lema
- Ben Saanane
- Yeriko Nyerere
- Jason Bourne na wengineo wengi
Mtashangaa kwa nini nimewataja baadhi hapo ambao mnaamini kuwa wapo humu. Ijapokuwa wapo na wanaendelea kuchangia ama kuanzisha mada, wengi wao wamebadili aina ya uchangiaji na mada wanazoweka. Sisi tunaowajua hakika tunaelewa nini kinachoendelea.
Huko Mtaani, hakika Makamanda wamepotea kabisa. Huwezi kuona sare za CHADEMA zikiranda mitaani. Wananchi wa kawaida nao huwezi kuwasikia wakisema kuhusu CHADEMA. Ile kazi waliyopewa ya kuzungusha mikono imeshawashinda. Hapa Kazi Tu ndio habari ya Mujini