Utekaji wa watoto: Gari yadaiwa kukamatwa ikiwa na watoto wawili waliotekwa

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,235
4,615
Salaam wakuu,

Kuna video nimekutana nayo ikimuonesha Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwa Zoka, Vigwaza akielezea tukio la utekaji lililotokea Mlandizi.

Mwenyekiti huyo amesikika akimpa maelekezo Mwalimu Mkuu ambaye hajafahamika jina akimtaka kuitisha kikao na wazazi kwa ajili ya kuwaeleza kinachoendelea kuhusu matukio ya utekaji. . Mwenyekiti huyo amesema kuanzia kesho wanafunzi watasitisha kusoma mpaka hapo utaratibu mwingine utakapopatikana.

Inadaiwa tukio hilo limetokea Kijiji cha Vigwaza kwa Zoka, Kidongozero na kambini ambapo inadaiwa Noah ilikuwa inazunguka ambapo mgambo aliweza kuistukia na kuwakurupusha ambapo pia alienda kuripoti kituo cha polisi. Inadaiwa ndani ya gari kulikuwa na mwanaume aliyekuwa amevaa Hijab.

Mwenyekiti huyo amesema leo Julai 23, watekaji wamekurupushwa Kambini, wakaenda Kidongozelo ambako wamekamatwa wakiwa wamechukua watoto wawili.


**Hapa kijana wangu katoka shule kaja na taarifa walizopewa na shule kuhusu utekaji.

Pia soma


Your browser is not able to display this video.
 
Watoto wana bahati sana hao, afadhali wakamatwe hao wahuni wataje mtandao wao hali imekuwa mbaya mtaani, sasa wazazi ni kupeleka watoto shule na kwenda kuwachukua kila siku.
 
Watoto wana bahati sana hao, afadhali wakamatwe hao wahuni wataje mtandao wao hali imekuwa mbaya mtaani, sasa wazazi ni kupeleka watoto shule na kwenda kuwachukua kila siku.
Wakiutaja mtandao huo nitajua kweli serikali tunayo.
Hizo biashara wanazijua vizuri sana.
 
Hao wakahojiwe kikatili sana ile tu salam ya kwanza umetoka na kidole akiwa anajibu tarayibu unaondoka na sikio huku mwenzake anaangalia yaan kwa jinsi navyo hangaika na wanangu hapa ndo uje uwateke mamaaaee nikikukamata nakupika supu ya mchemsho.Kwanza hao kuwafunga jela ni uharibifu wa hela zetu wale ndo wa kupelekwa huko kwenye mamba
 
dah itafkia kipind kua na noa tu nyeus kisanga hiii nchi jaman gar aitek watu watu ndo wanateka watu ila serkal ingefany uchunguz hawa wenye viti weng uwaga waswqhil tu wa kweny vjiwe vya kahawa habar za kjiwen anaipublish ndo kipnd kile temek habar za popobawa mwenye kiti anatoa ushuhuda kbsa wa temek watu tunalala nje majuz nyumba ile aliwatembelea popobaw yn katengelez taharuk then mwish wa siku kumbe ni habar za kuzua tu kwann ao wazaz waliotekew watoto wasitoe taharif polis thn polis walopew ripot za kutekwa watoto wazthbtshe wao wakihoj na hao wazaz il kutoa sintofaham
 
Yani tunaogopa hata kwenda mishe mishe na kuacha familia pekee nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…