Utawala uliofitinika unajivua nguo mbele ya wananchi Na hakuna litakalositirika tena:
~ Watanzania hawakuwahi kukifahamu chama cha mawakili Tanganyika (TLS), sasa wamekifahamu vema na Rais wake wamemfahamu kwamba ni Mhe. Tundu Lissu (Mb).
~ Watanzania hawakuwahi kufahamu kwamba kuna Bunge la Afrika mashariki (EALA), na kwamba Uchaguzi wake unafanyikia kwenye Bunge la JMT na wapiga kura ni wabunge wetu, sasa wamefahamu na wameona namna CCM bungeni inavyotumia nguvu kubwa kuukandamiza upinzani Kwa maslahi ya chama chao na sio Taifa.
~ Watanzania hawakuwahi kufahamu Kwa undani kuhusu Idara ya Usalama wa Taifa nchini (TISS) pamoja na majukumu yake na shughuli zake na mpaka sasa idara hiyo ipo katika hali ipi, lakini sasa wana shauku kubwa kutaka kufahamu hayo, na Kwa uchache wamefahamu kwamba ipo idara hiyo, na katika matukio kadhaa imehusika.
Ni nini wananchi wanasubiri zaidi? Ni ufafanuzi na uchambuzi wa kina kuhusu hayo yote na mengine yaliyositirika, ni wakati sasa wa kuuangazia Umma wa watanzania utoke kizani... Kazi hiyo nitaifanya.
.