Utatuaji wa Mgogoro katika Sekta ya Utumishi wa Umma nchini Tanzania: Uchambuzi wa Sheria na Utaratibu

Irene Gudu

New Member
May 6, 2024
2
1
Muhtasari
Moja ya lengo muhimu la kutunga Sheria ya Utumishi wa Ummaya Mwaka 2002 ni kutoa mpango kazi wa kutatua migogoro na kutoa kazi na majukumu pamoja na kuanzisha tume ya utumishiwa umma na mambo yanayoendana na hayo. Hii inamaanishakwamba Sheria ya Utumishi wa Umma ya 2002 ilikuja kueleza na kutatua pamoja na mambo mengine taratibu za uendeshaji wa migogoro ya kazi katika sekta ya utumsishiwa umma.

Andiko hililimejikita kwenye uchambuzi wa taratibu za uendeshaji wa migogoro kwenye sekta ya utumishi wa umma; kwanza kwa kuonyesha taratibu za utatuzi wa mgogoro ndani ya sekta hii kwa ujumla pamoja na kubainisha changamoto zitokanazo na taratibuza utatuzi wa mgogoro ndani ya sekta ya utumishi wa umma kamazilivyowekwa na Sheria ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2002. Mwisho, kutoa mapendekezo ambayo yatasaidia kuhakikishaufanisi wa utatuzi wa migogoro ndani ya sekta ya ummaunafikiwa.

1.0 Utangulizi
Kwa mujibu wa Sheria nchini Tanzania, baada ya kutokeamgogoro baina ya Mtumishi wa Umma na mwajiri wake, mfanyakazi anapaswa kufuata taratibu za Watumishi wa Ummakama zilivyo katika Sheria ya Utumishi wa Umma. Mamlaka ya Rufaa kwa Mleta Maombi kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma ni Tume ya Utumishi wa Umma. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 9 (3) (e), 25 (l) (b) na 31(2) cha Sheria ya Utumishi wa Umma zikisomwa pamoja na kanuni ya 60 (2) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za 2003.

Sheria na kanuni zinaeleza kuwamaamuzi ya wakuu wa Taasisi yanakatiwa Rufaa kwenda Tume ya Utumishi wa Umma. Baada yapo, Rais anamamlaka ya kupokearufaa kutoka kwa mtumishi wa umma ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa Tume ya Utumishi wa Umma. Anaweza pia kupokearufaa kutoka kwenye kamati ya nidhamu dhidi ya uamuzi waTume ya Utumishi wa Umma, ambapo uamuzi wa Rais utakuwawa mwisho. Pale ambapo mtumishi wa Umma hataridhika na uamuzi wa Rais, uamuzi huo wa Rais unaweza kurejewa kwa njiaya Mapitio ya Mahakama katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa sababu kama vile upendeleo, Kanuni za haki zilizovunjwa wakatiwa kusikia shauri hilo.

Mwaka 2016 kulifanyika mabadiliko ya sheria ya Utumishi waUmma kupitia Sheria ya mabadiliko ya Sheria Na. 3 ya 2016ambayo iliongeza kifungu cha 32A katika Sheria ya Utumishi wa Umma. Nyongeza hii ilieleza kwamba watumishi wa Taasisi za Umma wataongozwa na Sheria zinazoongoza Utumishi wa Umma.Hivyo, Mfanyakazi anapaswa, (kabla ya kuwasilisha Shauri mbeleya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kwa lengo la kutaka kupatahaki zake chini ya sheria za kazi), kufuata taratibu za Rufaa kamakifungu cha 32A cha Sheria ya Utumishi wa Umma kinavyoelezakuwa akamilishe kwanza taratibu zilizopo ndani ya Sheria kablaya kutafuta haki yake katika vyombo vingine vya kisheria.

Mahakama Kuu ilikuwa na msimamo sawa na huo katika shauri la Faima Siraji dhidi ya Mamlaka ya maji Safi na maji Taka Mbeya,ambapo Mahakama iliamua kuwa Mtumishi wa Umma anatakiwakufuata taratibu za ndani kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma kabla ya kufuata taratibu za Sheria nyingine. Hivyo, kufuatia Mabadiliko hayo hivi sasa Sheria ya Utumishi wa Ummainataka Mtumishi kumaliza taratibu za ndani za utatuzi wa migogoro ya kazi kabla ya kufuata taratibu za sheria nyingine.

2.0 Ufanisi wa Taratibu za Utatuaji wa Mgogoro katika Sektaya Utumishi wa Umma Nchini Tanzania
Kama ilivyooneshwa hapo juu, ni matakwa ya sheria kuwa endapoMleta Maombi ni Mtumishi wa Umma kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, kifungu cha 32A cha Sheria ya Utumishi wa Umma kinamtaka Mtumishi wa Umma aliyeachishwa kazikukamilisha taratibu za kupata nafuu zilizowekwa na Sheria hiyokabla ya kutafuta nafuu katika sheria za kazi.

Hata hivyouchambuzi wa matakwa haya ya sheria yameonyesha kutokuwa na ufanisi hasa katika utatuaji wa migogoro ndani ya sekta ya utumishi wa umma. Ufanisi wa taratibu hizi ni wa kutiliwamashaka kutokana na kigezo kilichopo chini ya kifungu cha 25 (1) (c) cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya 2002. Kifungu hikikinafanya maamuzi ya Rais kuwa maamuzi ya mwisho ambayohayawezi kukatiwa rufaa. Msimamo huu wa kisheria ulirejewa na Mahakama kuu na kubainika kuwa na mapungufu katika kesi yaAsseli Shewally dhidi ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza,ambapo Jaji Mkasimongwa, alibainisha kuwa, ni matakwa ya sheria kwamba baada ya kukamilisha taratibu za kupata nafuuzilizowekwa na Sheria ya Utumishi wa Umma, Mtumishi wa umma atakuwa na haki ya kutafuta nafuu katika sheria za kazi.

Hata hivyo sheria hii inasababisha usumbufu kwa watumishi wa umma. Kwasababu, ukamilishaji wa taratibu za kutafuta haki(nafuu) chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma unakuja namaamuzi ya mwisho, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi hainamamlaka ya kupokea na kuamua Shauri ambalo limefanyiwamaamuzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

3.0 Mapendekezo
Kufuatia changamoto zilizobainishwa hapo juu, andiko hililinapendekeza kufanyika yafuatayo ili kuboresha taratibu za utatuzi wa mgogoro ndani ya sekta ya Utumishi wa Umma.

(i) Ujumuishaji wa taratibu za utatuzi wa migogoro ndani ya sheria moja.
Taratibu za utatuzi wa migogoro zinapaswa kuwa ndani ya sheria moja (sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya 2004) ili kuwafanyawatumishi katika sekta zote kuwa na uwezo wa kufikia Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ikiwa ni pamoja na kupata hakizinazopatikana chini ya sheria za kazi kama ilivyokuwa kabla ya mabadiliko ya sheria mwaka 2016.

(ii) Maboresho ya kifungu cha 32A cha Sheria ya Utumishi wa Umma.
Mbali na ujumuishaji wa taratibu za utatuzi wa migogoro katika sheria moja, ni lazima pia kifungu cha 32A cha Sheria ya Utumishi wa Umma kiboreshwe ili kutoa mwanya kwa watumishi wa ummakupata haki zao chini ya sheria za kazi bila kuwa na ugumuwowote chini ya sheria kama ilivyo sasa. Kifungu hiki kinapaswakuboreshwa ili kuondoa matakwa ya mtumishi wa umma kumalizataratibu zote zilipo chini ya sheria hiyo ndipo akatafute hakikwenye sheria za kazi.

4.0 Hitimisho
Andiko hili limeonyesha kuwa utaratibu wa utatuzi wa mgogorokatika sekta ya Utumishi wa umma unawaweka katika njiapandaya matatizo yao kutotuliwa kwa misingi ya haki. Hii inatokana namatakwa ya sharia kuwa kabla ya kwenda kutafuta haki (nafuu) kupitia sheria za kazi, mtumishi wa umma anatakiwa kuhakikisha amemaliza taratibu zote zilizowekwa ndani ya Sheria ya Utumishi wa Umma. Ni Mapendekezo ya andiko hili kwamba kuna uhitajiwa Maboresho ya kifungu cha 32A cha Sheria ya Utumishi wa Umma, pamoja na ujumuishaji wa taratibu za utatuzi wa migogoroyote (katika sekta ya umma na sekta binafsi) ndani ya sheria mojakama ilivyokuwa kabla ya mabadiliko ya sheria ya mwaka 2016.
 
Back
Top Bottom