Utata wa wanawake kupewa basi lao peke yao

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Uzinduzi wa basi la wanawake pekee katika mji mmoja wa China umewakasirisha wanaume wa taifa hilo na kuzua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii.

Huduma hiyo mpya itatolewa wakati wa asubuhi na wakati wa shughuli nyingi katika mji wa mashariki wa Zhengzhou katika juhudi za kupunguza visa vya wanawake kusumbuliwa na wanaume kulingana na gazeti la Dahe daily.

Kampuni hiyo ya basi itawalinda wanawake dhidi ya kunyanyaswa wakati wanapovaa nguo nyepesi huku wanawake wanaonyonyesha wakihisi wapo salama.

Treni za wanawake na mabasi yameanzishwa katika mataifa mengi na kuonyesha ufanisi mkubwa, lakini magari ya uchukuzi ya watu wa jinsia moja ni swala jipya nchini Uchina.

Wanawake waliohojiwa ndani ya basi hilo wanasema wanafurahishwa na huduma hiyo huku mmoja akimwambia ripota kwamba ni heshima kubwa kwa wanawake.

Lakini baadhi ya wanaume hawafurahii jambo hilo.


Basi la wanawake China
Mmoja aliliambia gazeti la Dahe Daily kwamba unyanyasaji sio jambo la kawaida katika magari ya uchukuzi.

Kampuni ya basi hilo imewakejli wanaume ikisema:Hatua hii itawafedhehesha wanaume.

Mtu mwengine amelalamika katika kituo cha redio cha Uchina:Nililazimika kungojea sana kwa basi jingine kuwasili kwa kuwa sikuruhusiwa ndani.
 
Wachina na vimiili vyao hata huwa hawavutii..Hii ingefaa ianzie hapa Bongo maana unakutana na dada jinsi Umbo lake na nguo aliyovaa ni mtihani wa shetani kabisa...Halafu unakuta mmekaa kwenye ile sit ya kwenye hiace pale mbele na yeye kaka ile sit ya wanafunzi ambayo ni lazima mpishanishe miguu...Duh hafu demu unakuta kapinda anakomaa kukuangalia usoni jinsi unavyohangaisha macho tu...Hadi ushuke chini jasho lilishakutoka..
 
wadada kunyonyesha, kushikwa shikwa, na matukio ya wadada kumwagiwa kwenye gari pia na daladala zetu bongo zilivyo hii ingefaa tatizo nchi masikini
 
bila shaka unashukaga kituo kisicho chako wewe
 
Safi sana, ije na bongo mambo ya kusafiri umesimamisha yanaleta usumbufu sana. Yaani toka ubungo hadi manzese unaona kama hufiki.
 
wadada kunyonyesha, kushikwa shikwa, na matukio ya wadada kumwagiwa kwenye gari pia na daladala zetu bongo zilivyo hii ingefaa tatizo nchi masikini
Na wadada wengine kuvaa kichokozi nakusababishia wanaume waliochomekea suruali za vitambaa kushindwa kushuka kwenye kituo chake husika maana hali imekuwa tete...Hii ingetusaidia hata sisi wanaume..
 
bila shaka unashukaga kituo kisicho chako wewe
Ni shida sana hafu dada anakuangalia machoni tu huku anatabasamu kwa mbaaaali na gari likipiga brake huna mahali pakushika zaidi ya mapaja yake..Very bad kwa kweli hii ije bongo chap chap
 
wakianza kutenga jinsia kwa mtindo huo watafika hadi mahala hairuhusiwi kusimama na jinsia nyingine,,,, matokeo ya hayo yote tunapata ndoa za jinsia 1.... mtu mnashinda mda wote jinsia 1 ata kutongozana mtatongozana saa ngapi?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…