Utaratibu wa ukusanyaji "kodi ya parking" una walakini sana

Simbamteme

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
797
2,110
Jana wakati natoka Makongo juu naenda zangu Ubungo kufika mitaa ya Survey nikakutana na barrier,wafanyakazi wa halmashauri ya kinondoni wanasimamisha magari yanayodaiwa madeni ya parking

Bahati mbaya au nzuri kakamkebe kangu nako kakasimamishwa..naambiwa nadaiwa deni la 38500/=

Nikawaomba wanionyeshe mchanganuo wa hilo deni...wakanionyesha kuwa ni la kutoka mwaka 2022..kuna baadhi ya maeneo nilionyeshwa kuwa niliwahi ku "park" gari mpaka mwenyewe nikashangaa inakuwaje wanadai kodi ya parking maeneo ambayo hayajawekewa miundo mbinu ya parking...Kuna madeni niliandikiwa wakati nilipoegesha gari kituo cha daladala nikiwa namsubiri mtu au naenda kuchukua kitu sehemu na kurudi

Kuna barabara za ndani ndani huko mtaani una "park" gari kumbe wanakuingiza kwenye System...nilichoka kabisa

Nilichowashauri ni kuwezesha basi mtu kupata "notification" kwenye simu kuwa ana daiwa kiasi flani kila anapoandikiwa hiyo kodi...maana mimi nilikuwa sijui kabisa kama nina deni lolote!!

Ila all in all huu utaratibu wa ukusanyaji hii "kodi" haujakaa sawa kabisa...watu wanabambikiziwa kodi kiholela sana...wanachojali wao ni makusanyo tu..watengeneze miundombinu ya ku "park" magari ili wakusanye hiyo hela kihalali!!
 
Manispaa hawana pesa, wanakusanya pesa kinguvu mpaka wapate kasma yao ya bajeti mpya, wana deficit ya Billion 30.
 
😀😀😀kuna wajomba fulani wanavaa traffic coats ogopa sana wanakua na vimashine vya efd kazi yao ni kubambikiza fine kama hizo
 
Back
Top Bottom