UTARATIBU WA MAZISHI YA KIKATOLIKI
• Taratibu za Mazishi ya Kikristo Kisheria
Sheria ya Kanisa Katoliki ( 1177 – 1185) inasema kuwa ni haki ya kila muumini mkatoliki kufanyiwa Ibada ya mazishi ya Kikristo isipokuwa kama amepoteza haki hiyo kwa ukaidi wake mwenyewe.
Haki hiyo inaambatana na wajibu wa Mkristo husika kwa mamlaka ya Kanisa na jumuiya nzima ya Kikristo. Wajibu wa mamlaka ya kanisa ni kuhakikisha kuwa wajibu wa mkristo unatimizwa.
Kwa wakristo waliojitahidi kuishi vizuri maisha yao ya Kikristo wanapaswa kupatiwa huduma ya mazishi ya Kikristo katika parokia yake na mazishi hayo yanapaswa kuongozwa na Paroko au Paroko msaidizi au Katekista au muumini mwingine aliyeidhinishwa na paroko kutekeleza wajibu huo.
Wanaonyimwa mazishi ya kikristo
Ibada ya mazishi ya Kikatoliki kama tendo lolote la Kiliturujia ni alama na ishara wazi ya mshikamano wa kikristo. Hivyo ibada ya Mazishi inapotolewa lazima umoja wa Kanisa uonekane wazi. Wanaopokea mazishi hayo ni lazima wawe wameonyesha umoja wa Kanisa kwa maisha yao. Hivyo wafuatao wananyimwa mazishi ya Kikristo kwa mujibu wa sheria ya Kanisa Katoliki:-
1. Yeyote aliyejitenga na mshikamano wa Kikristo anapoteza haki zake katika kanisa ikiwa ni pamoja na haki ya kupata mazishi ya Kikristo. Hao ni pamoja na hawa wafuatao: (Sheria ya Kanisa Namba 751 na 1184)
a. Wale walioasi kanisa – kwa kufuata mafundisho ya dini nyingine,(waliohamia dini nyingine wakifa wasizikwe kikatoliki)
b. Wale waliojitenga na kanisa – kwa kutosali siku za jumapili na sikukuu za amri. (Amri ya tatu ya Mungu na Amri ya kwanza ya Kanisa, wakifa wasizikwe kwa sala wala kwa ibada yoyote ya Kikatoliki)
c. Wazushi katika mafundisho ya imani – wanaojiita wakristo wakatoliki lakini wanafundisha kinyume na kanisa katoliki linavyofundisha.
d. Wanaokataa utaratibu sahihi ulioanzishwa na kanisa – mfano utaratibu sahihi wa Jumuiya ndogondogo ulioanzishwa na kanisa, wanaokataa kabisa kusali Jumuiyani na kanisani siku za Dominika kwa makusudi yote.
2. Wakristo waliojitenga na kanisa. Hawa ni wale wanaokataa ukweli unaofunuliwa na Mungu, au kwa makusudi wanakataa kukubali ukweli uliotangazwa na kanisa. Hao ni pamoja na hawa wafuatao:-
a. Waliobatizwa lakini wanakataa kwa ukaidi ukweli ambao ni lazima kuusadiki kwa imani ya kanisa katoliki (Dhambi hii inaitwa heresia)
b. Wale wanao kana dini Katoliki mbele za watu (Dhambi hii inaitwa Apostasia)
c. Wale wanaokataa mamlaka ya Kanisa, yaani kumkiri Baba Mtakatifu, kuwaamini Maaskofu, Mapadre na Mashemasi (Dhambi hii inaitwa Skisma).
3. Wakristo wanaohusishwa na dhambi za waziwazi. Yaani wakristo wenye tabia inayowakwaza wakristo wengine. Hao ni pamoja na hawa wafuatao:
a. Wakristo wenye ndoa za mitara (Wake wengi au waume wengi wahawapaswi kupewa mazishi ya Kikatoliki. Wanapaswa kubaki na mme mmoja na mke mmoja)
b. Majambazi wanaotishia maisha ya watu kwa kutumia silaha.
c. Wale wanaofuata mila zenye upotofu mkubwa unapingana na kanisa kwa mfano: Kurithi wajane, kukubali kurithiwa kama mjane, kutambika mizimu, vitendo vya ushoga (Kujaribu kufanya ndoa ya jinsia moja)
d. Wale wenye imani za ushirikina; mfano mganga wa kienyeji, mchawi anayefahamika, kuagua (kupiga ramri), kumkaribisha mganga wa kienyeji nyumbani mwako.
4. Wakristo wanaopotosha mafundisho ya kanisa kwa makusudi. Hao ni pamoja na hawa wafuatao:
a. Wale wanaokufuru Ekaristi takatifu, mfano kuiba Ekaristi Takatifu, kuitupa, kuichezea au kuifanyia mamba ya kishetani.
b. Wale wanaotupilia mbali wajibu wa kutunza familia – wanaotelekeza familia zao (Wasiotimiza wajibu katika familia zao)
c. Wale wanaowatesa wanafamilia wenzao kwa ukatili mkubwa.
d. Wale wanaodharau desturi takatifu za kanisa Katoliki mfano kuiba vitu vya kanisa, kuchoma au kuharibu vitu vitakafu kwa makusudi kama vile rozari na visakramenti vingine.
e. Wale wanaochochea kuzuka kwa madhehebu potofu miongoni mwa wakatoliki.
f. Wale wanaojihusisha na vitendo vya kuua watu, mfano kwa kuwadhania kuwa ni wachawi, kuwaua walemavu wa ngozi (Albino).
5. Waamini wote wanaokufa wakiwa wamejitenga na kutengwa na kanisa hawapewi mazishi ya Kikatoliki. Sababu ya msingi ya kuwakatalia ni kwamba kwa hiari yao wenyewe au kwa ukaidi wao wenyewe wameamua kuleta makwazo makubwa kwa kanisa na jamii yote ya kanisa.
Nafasi ya Jumuiya ndogondogo katika Mazishi ya Kikatoliki
Nafasi ya Jumuiya ndogondogoza Kikristo katika mazishi ya Kikatoliki inaonekana katika swala linaloitwa “Kutoa uamuzi” Muumini mkataoliki anaishi katika Jumuiya ndogondogo za Kikristo. Ni wakristo wenzake wanaoweza kuonyesha kuwa huyu aliiishi imani yake vizuri au la. Ni wanajumuiya wanaoweza kuonyesha kuwa mkristo huyo alikuwa vizuizi vilivyotajwa hapo juu au la. Ni kazi ya wanajumuiya kumtambua mkristo anayepaswa kunyimwa mazishi ya kikristo au kupewa mazishi ya kikristo. Sababu yenyewe ni kwamba jumuiya za kikristo zinafahamu vizuri maisha ya wanajumuiya wao. Wanajumuiya ni mashaihidi wa jinsi muumini mwenzao anavyoishi. Hawa ni mashahidi kamili na ni kazi yao kushuhudia ukweli jinsi marehemu alivyoishi nao katika Jumuiya yao.
Wanajumuiya wana wajibu wa kutoa taarifa za kweli kwa viongozi halali wa kanisa. Wanapofanya hivyo wanakuwa mashahidi tu wa ukweli utakao wawezesha viongozi wa kanisa kutoa uamuzi unaotegemezwa na ukweli na haki. Wanajumuiya hawapaswi kulaumiwa kwa lolote isipokuwa wanapaswa kuwa wakweli mbele ya kanisa na mbele ya Mungu.
Je mtu a siye mwanajumuiya anaweza kunyimwa mazishi ya kikristo? Ndiyo kwa sababu mtu asiye mwanajumuiya itajulikanaje kama ana vizuizi au la? Asiye mwanajumuiya si mwenzetu maana wanajumuiya hawafahamu maisha yake. Hivyo kutoa uamuzi endapo mtu huyo amekufa kutaathiri ukweli wa maisha ya mtu. Ni katika Jumuiya mtu anapata nafasi ya kudhihirisha maisha yake na hivyo kuwapatia wanajumuiya nafasi ya kusema ukweli katika maamuzi yao baada ya kifo cha mmoja wa wanaojumuiya yao.
Sheria na taratibu za kanisa ziko wazi kabisa kuhusu nani anapaswa kupewa mazishi ya kikatoliki. Sheria hizi zinatawala wabatizwa wote pasipo kuangalia tajiri, masikini, jinsia, uraia, uanasiasa, jamaa ya viongozi wa kanisa. Hivyo katika hali ya kutatanisha jumuiya ziende ngazi ya juu kupata ushauri na maelekezo. Tukumbuke kuwa mwenyewe mamlaka na kauli ya mwisho ya kutamka kuwa marehemu Fulani apewe au anyimwe mazishi ya kikristo ni paroko wa parokia husika. Kukiwa na utata mkubwa paroko ataomba ushauri kwa mchungaji mkuu – Askofu wa Jimbo.
Viongozi wa ngazi zote: Wafundisheni watu watambue wajibu wao wa kuishi vema Imani yake. Kila mmoja atimize wajibu wake kwa kuwafundisha wanao husika ili mwisho wa siku yeyote aslilaumiwe kwa sababu ya kutekeleza majukumu yake katika kiongozi wa Kanisa. JAmbo la maana ni kuwatembelea wale wote walio katika mazingira ya kutozikwa Kikristo ili wayabadilishe maisha yao ili msije mkalaumiana baadaye.
MWONGOZO TEC - KUTOKA KITABU KILICHAANDIKWA NA ASKOFU WA MOSHI AMEDEUS MSARIKIE
Mungu atubariki sote