Utaratibu wa Manispaa Hadi Kulipishwa Faini ya Kujenga Bila Kibali

ComputersDAR

JF-Expert Member
Jan 21, 2013
213
242
Wakuu heshima kwenu

Nahitaji msaada kuhusu utaratibu wa Manispaa pale ambapo mhusika amegundulika kuwa ameanza ujenzi wa nyumba ya makazi ya kawaida isiyo ghorofa kwenye kiwanja chake halali kisicho na mgogoro wowote lakini bila ya kuwa na kibali cha ujenzi kuoka manispaa.

Jee, ni sawa kama mtu ameanza ujenzi bila kibali na baadaye kwa hiyari yake kuamua kwenda manispaa na kuwasilisha maombi ya kibali cha ujenzi na hadi kulipia ada ya kibali, kulazimishwa kulipa fine ya 2% ya thamani ya jengo lake?

Au kuna sababu nyingine za msingi pamoja na hatua ambazo zinatakiwa kufuatwa awali kabisa na manispaa kama kupewa notisi ya kusimamisha ujenzi na muda wa kuanza utaratibu wa maombi ya kibali cha ujenzi kabla ya uamuzi wa kutoza fine ya kujenga bila kibali ilhali hujakamatwa na ulienda mwenyewe manispaa kupeleka maombi ya kibali cha ujenzi?

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom