KERO Utaratibu wa kufukuzwa Wodini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Makuke

New Member
Jul 19, 2015
4
27
Habarini ndugu zangu,

Kwa masikitiko makubwa naomba kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa huduma za afya nchini kwetu hasa kwa wagonjwa waliolazwa ambao hali zao sio nzuri.

Ni wiki sasa nimempoteza mama yangu mdogo na mtu wangu wa karibu sana hapo Hospitali ya Mloganzila, kwa kile ninachohisi ni utaratibu usio rafiki wa kuhudumia wapendwa wetu.

Kumekua na utaratibu wa kufukuzwa ndani ya wodi na kuwaacha wagonjwa wetu wauguzwe na manesi pekee usiku kucha, hii inatumalizia ndugu zetu kwasababu Nesi hawezi kuangalia wagonjwa zaidi ya mmoja kwa ufanisi uleule ambao ndugu anaweza kumuangalia mgonjwa wake pekeake na kunotice kwa haraka hali ya mgonjwa wake imebadilika.

Inauma sana umetoka jioni umemuacha mgonjwa wako halafu asubuhi unakuja kumuona unakuta amefungwa ameshafariki, hii inauma sana, wengi tunatamani kuagana na wapendwa wetu na kuskia maneno yao ya mwisho ama kutoa msaada wowote unapohitajika na kama sio hivyo bas angalau kujionea ilikuaje mpaka hali ikabadilika na kuondoka.

Manesi wanajitahidi sana kwa nafasi yao lakini amini usiamini Nesi hawezi kuwa na uangalizi sawa kwa mgonjwa kama ndugu,
lakini pia Usiku huo kuna wagonjwa wanabadilika ghafla hali zao na wanahitaji msaada wa haraka na muda huo Nesi anakua yupo Nursing Station au anakua yupo kwa wagonjwa wengine, kwa situation kama hii mgonjwa anaaga dunia akiwa anajiona lakini anashindwa kuomba msaada kwakua hajiwezi(mfano wagonjwa wa sukari au presha)

Tunaomba mturuhusu kuwa na wagonjwa wetu pembeni yao wakati wa usiku na sio kuwaacha usiku wakiwa hawajiwezi na kurudi asubuhi na kusimliwa walifariki usiku, inauma sana.

Tunaomba sana Serikali iliangalie hili.

REST IN PEACE MAMDOGO
 
Una hoja mkuu,

Ni vyema ndugu muuguzaji awepo, hii itapunguza mzigo kwa nurse sababu mgonjwa anaweza hitaji maji ya kunywa ila sababu nurse yuko mbali basi inakua shida ila akiwepo ndugu jirani anakua anasaidia mambo madogo yasiohitaji utaalamu.
 
Una hoja mkuu,

Ni vyema ndugu muuguzaji awepo, hii itapunguza mzigo kwa nurse sababu mgonjwa anaweza hitaji maji ya kunywa ila sababu nurse yuko mbali basi inakua shida ila akiwepo ndugu jirani anakua anasaidia mambo madogo yasiohitaji utaalamu.
Najiuliza tu mle wodini kila mgonjwa awe na ndugu yake.
BTW hata mimi ningependa kuwa pembeni ya mpendwa wangu.
 
Najiuliza tu mle wodini kila mgonjwa awe na ndugu yake.
BTW hata mimi ningependa kuwa pembeni ya mpendwa wangu.
Kuna UBAYA Gani tena ndo vizuri,mnawafariji wagonjwa.huku mnapiga stories.
Wanajiona wapo nyumbani.
Mule Kuna Tisha ukiwa peke yako asikwambie mtu,
Kila mgonjwa aruhusiwe ndugu mmoja
 
Back
Top Bottom