Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,363
Kumekuwa na wimbi kubwa sana la watu kujinadi kwamba wanaweza kutengeneza pesa mitandaoni na wapo tayari kuwaelekeza wengine kwa ada ya kiasi flani (mtonyo).
Njia wanazotumia kupata Wateja
1. Social media bure - hapa wengi hujitangaza kwenye social media kuanzia Instagram, fb, magroup ya WhatsApp hata humu Jamii forums kwa kuanzisha post, kwa insta na fb wengi wanakomenti kwenye page za watu maarufu, hawana utofauti na wale wanaokoment dawa za nguvu za kiume
2.social media kwa malipo - hapa nao wanalipa kwa page zenye followers wengi, haya malipo yanajulikana kama shout outs, inaweza ikawa mtu unampa Masanja laki 1 ili apostiwe tangazo, kuna Dogo moja pia niliona kamwita millard akijinadi kaacha chuo saizi anapiga forex kapata mamilioni na vitu kibao vya kutamanisha, akachomekea na maada ya darasa lake la kufundisha forex nikaona huyu nae wale wale tu.
3.kuishi maisha feki - labda nikushangaze tu, binadamu tunaamini sana tunachokiona, mtu anaweza kwenda airport na kutoa laki tu apige picha kibao ndani ya private jet na akiandika biashara flani inamfanya aishi vizuri, wengi sana watashawishika na kuwa tayari kulipia darasa, kuna watu wamepaki range rovers pesa zimewaishia huwa hawaoni shida kuzikodisha hata kwa laki kwa siku ukiwa na connections nao na hapa wengi sana wanawehuka na kuwa tayari kuuza hata mali zao ili wapate elimu.
Hawa watu Mara nyingi kitu wanachodanganya kinawaingizia pesa huwa wanakijua kwa juu juu tu na wengi wanakuwa hata hawajawahi kukijaribu kwa vitendo.
Mimi binafsi nimeshuhudia kuna jamaa aliwahi kufundiha watu 130 katika nyakati tofauti tofauti ndani UA miezi miwili kwa ada ya laki 1 na nusu kuwafundisha forex, Huyu bwana alikua anaijua forex kwa juu juu sana na hakuwahi kutengeneza hata faida ya dola 5, alikusanya pesa nyungi kwa kuwafundisha hao wanafunzi kwa juu juu tu nikabaki namshangaa kanunua gari yake mpya na wanafunzi wake wakiwa njiapanda.
Ndicho kinachofanyika hata kwenye fursa nyingi za online, leo mtu wanaweza kujinadi anaweza kutengeneza pesa kwa blogging, affiliate marketing, site flipping, forex, freelancing, n.k ila kumbe yeye anajua kwa juu juu tu hivi vitu, na ndio kitu kinachomfanya ajiamini anapofundisha watu wasiojua kabisa.
Nawasihi sana kabla hujalipia kupata elimu hizi hakikisheni kwamba Mwalimu ndio anawatumikia, sio nyinyi ndio mumtumikie Mwalimu, mteja ndie mfalme.
Hakikisha huyo Mwalimu anatoa ushahidi wakutosha kuhusu kampuni anayofanyia kazi mtandaoni, kwa mfano kama ni blogging kuna makampuni yanayolipa bloggers kama AdSense, propeller ads, medianet, admaven,n.k Kitu cha pili ombeni ushahidi wa mapato anayoingiza na ushahidi wa miamala ya kutoa pesa. Inapendeza zaidi mnapochakata huo ushahidi wake muwe na mtu mzoefu kidogo anaeweza kutambua kama kuna madudu yaliyochakachuliwa.
Akiwa mkali au kuleta kiswahili kingi basi namna haja ya kulipia, mkithubutu kulipia imekula kwenu,
Hali ndivyo ilivyo, kuna baadhi ya fursa ukiitwa jijue wewe ndiye fursa