ngungo
New Member
- Aug 28, 2020
- 4
- 7
Kama ilivyo mifumo mbalimbali duniani katika nchi au taifa lolote lenye uchu na nia ya kupiga hatua kila kukicha, kwa kuwekwa imara kulingana na matakwa ya uzingatiaji wa uimara wa vizazi vijavyo na iwe ni faida endelevu ya kufanya watu katika taifa kuendelea kuneemeka kwa sababu ya kuwepo miundombinu thabiti na yenye nguvu ya muda mrefu yenye ushindani kimataifa na yenye matakwa na mahitaji yote ya ulimwengu wa Sasa.
Ni kweli usiopongika Tanzania tuitakayo inawezekana kwa kujitoa na uwekaji thabiti mifumo yenye tija na endelevu bila utegemezi wowote kwa sababu lengo kuu ni kupiga hatua, hauwezi kupiga hatua kwa kutumia uwezo wa fedha wa mtu mwingine lasivyo utaendelea kuwa mtumwa muda wote na hulka ya kuitafuta nchi yenye asali na maziwa inaishiria na kubaki kuwa ndoto.
Falsafa ya maisha huwa ni kazi, kwenye kuchapa kazi ndio maana ya maisha, lakini hapo tunapata mazingira ya uzalishaji kwenye sekita zote ziwe za kilimo, biashara elimu, uvuvi na ufugaji, nchi yetu ya Tanzania ina mazingira mazuri ya kuwezesha uzalishaji wa hali ya juu wenye ubora wa juu kwa kuwajibika, binafsi nashauri na hili naliweka kipaumbele endapo kila wizara ikiwa na uwezo wa kujiendesha tunapiga hatua kwa asilimia kubwa, maana ni uwezo wa kila wizara kujitegemea kutokana na mapato basi, wizara husika iweze kujiendesha na wataalamu katika sekita husika wafundishwe uzalendo, waipende kazi, wajengwe kuwa wabunifu wa kubuni mwendelezo wa kuisitawisha sekita yao katika kuleta maboresho ya kimukakati na yenye tija kwa taifa letu hatimaye tutafikia ile asali na maziwa iliyojificha upande wa pili, lakini pia wizara husika inatakiwa ijikite na kufanya kazi bega kwa bega na wananchi ili kufikia malengo, kwa sababu walengwa ni wananchi, kutatua kero za wananchi katika eneo husika, kubuni miundombinu ya kisasa na yenye tija katika ulimwengu wa Sasa na kufufua miundombinu ya zamani na kuikarabati upya hapo maana ni kurejesha mwonekano wa uharibifu wowote uliotokea katika miundombinu hatimae kuneemesha wananchi na taifa kiujumla katika kuwawekea mazingira salama ya uzalishaji.
Tukiwa tumejidhatiti na utekelezaji, imani, ubora wa kazi na ukataaji wa rushwa Kama nilivyoeleza hapo awali, wasilisho langu linajikita katika nyanja zifuatazo Elimu,Maji,Nishati na Kilimo endapo tukizalisha fedha za kutosha bila utegemezi wowote sekita hizi zinatakiwa kuboreshwa kama ifuatavyo.
Elimu, binafsi hoja yangu kwenye elimu ni kuchochea upatikanaji wa elimu ya kujitegemea, isiyokuwa na utegemezi ndani yake tuliyonayo ni mfumo ambao hauendani na usasa, kuanzia msingi, sekondary, mpaka vyuo tujikite zaidi kwenye stadi za kazi na ujuzi, ni aibu kijana muhitimu wa darasa la Saba anashindwa kutatua changamoto zinazomzunguka katika mazingira yake ya nyumbani mfano anakosa uwezo wa kuzalisha nyanya na mbogamboga ili kutatua na kumaliza changamoto ya uhitaji wa vitu hivi katika mazingira ya nyumbani, anafundishwa kabisa njia ya kutokomeza uzalianaji wa mbu ili kujikinga na ugonjwa wa malaria lakini anashindwa kufukia madimbwi na kufyeka majani, na kupunguza matawi ya miti kuzunguka makazi anayoishi, maana halisi ya elimu tunayoitaka ni ile inayomuhitaji kijana au mwanafunzi kufanyia kazi kwa vitendo kile anachoelekezwa kila siku, hii itamjenga na kuwa tayari kukabiriana na changamoto za maisha baada ya masomo.
Kwa matakwa ya dunia inavyoenda kasi na usasa wa kidijitali, ikimuhitaji mtu kuwa na mtazamo tofauti wenye ubunifu na wakuvutia ili hata ukionekana uwe na faida lakini was kipekee na wakitalii, kwenye hili la elimu inatakiwa lishughulikiwe kwa kuwekwa maboresho ya vifaa na vitendea kazi vyenye ubora mfano shule zilizonyingi za kidato Cha tano na sita zinakosa miundombinu thabiti yenye ubora wa juu hasa ili kuzalisha wahitimu bora wenye tija na wanaoendana na hatua hiyo.
Kilimo na Maji, natamani kuiona Tanzania niitakayo ikijipambanua na kuchanua kwa kiwango cha hali ya juu katika kulahisisha shughuli za kilimo nchi yetu inamazingira wezeshi ya kujitengenezea miundombinu katika sekita ya kilimo kwa muda wote tukiamua tunaweza kwa sababu tunavyanzo vya maji vukubwa na vidogo karibia nchi nzima, itoshe kusema kilimo Cha umwagiliaji kinawezekana kwa sababu ya vyanzo vingi, uwepo wa maziwa, mabwawa na mito, lakini pia zao la mpunga si lakutegemea vipindi vya mvua tu, sekita husika inatakiwa ielekeze nguvu kwenye uundaji wa sikimu na mifereji mbalimbali ikilenga kuchepusha maji kupeleka sehemu pasipo na maji na kufanikisha uzalishaji wa zao la mpunga, mbogamboga na matunda kwa wingi kila mahali ndani ya nchi yetu, vilevile hoja ya kusema kwamba tunaweza kuathiri kina Cha maji ya ziwa ni hoja zisizo na mashiko kwa sababu na elimu ya kutosha kwa sababu sayansi inaelekeza kuwa maji yaliyochepushwa yanarudi ziwani kutokana na tabia ya nchi na mazingira kwa ujumla.
Uvuvi na Ufugaji nchi yetu imejaaliwa ufugaji na uvuvi katika maeneo na kila Kona, serikali kupitia wizara husika inatakiwa kuboresha miundombinu ya kisasa kunufaisha wavuvi hasa pale inapopumzisha ziwa kwa shughuli hizo, ufugaji nao unatakiwa kuendana na mahitaji ya uzalishaji wa mazao, mfano kutokana na uwekaji wa mazingira vizuri, Serikali inatakiwa ijikite katika uwekezaji wa viwanda vya ngozi, kwato, gundi utengenezaji wa kirutumbisho kitokanacho na samaki na samaki kiitwacho Omega-3-kitalamu, chenye nguvu ya kuimarisha na kurutubisha vizuri ubongo wa binadamu kwa kuzingatia hayo sekita ya uvuvi na ufugaji zinauwezo wa kuzalisha viwanda vingi sana kwa kuruhusu uwekezaji wa watu kutoka katika mataifa mbalimbali na watu wa ndani kwa kuwahakikishia usalama wa kuwekeza katika kutatua migogoro ya wafugaji na wakulima hatimaye uzalishaji mkubwa.
Nishati ni suala la msingi na linalohitaji vipaumbele na mikakati, kutokana na nchi yetu ndo kwanza inaendelea lakini pia Kama ilivyohitajika nishati mwilini, bila nishati binadamu ni mgonjwa, Tanzania inahitaji nishati endelevu yenye nguvu bila kuathiri vyanzo vingine Kama vya maji wasilisho langu linajikita katika katika kuchagua aina ya uzalishaji wa nishati usio na gharama ya uendeshaji ambao vinu vya nyukilia na mitambo inayozalisha umeme kupitia upepo, mikoa ya Singida na Dodoma ipewe kipaumbele kufanikisha hili maana ni kufunga tu mitambo na kusubiria umeme wa uhakika wa mda wote kupitia upepo.
Nawasilisha.