Watanzania wameamka kwenye utetezi wa utalii wao. Kila kurasa ya mtanzania ya facebook kuna picha za vivutio tulivyojaaliwa, naona hamasa ya kuitangaza nchi imekuja kwa kasi kubwa sana.
Wajukuu wamerudi kijijini kuliokoa shamba la bibi, ambalo kwa kweli kila mtu aliliona kama la kwake, lakini nguvu hii isiwe ni ya muda mfupi. Wizara yenye dhamana ya utalii iutumie huu mwamko walionao watanzania katika kutumia mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa sheria, katika kuhakikisha kila rasilimali yetu inajulikana kila kona ya dunia hii.
Wizara ya utalii isiwaache watanzania mmoja mmoja wakihangaika kutafuta picha mpya za vivutio vyetu na kuzipost kwenye kurasa zao. Wao wanaendesha shughuli zao kwa kutumia kodi ya wananchi. Kinachotegemewa kutoka kwao kinatakiwa kiwe ni zaidi ya nguvu na ubunifu wa kila mtu anayeipenda na kuitangaza nchi na vivutio vyake.