Kommando muuza madafu
JF-Expert Member
- Aug 30, 2022
- 3,161
- 7,199
Habari za jioni wana JF.
Katika kutafuta fursa za kimaisha baada ya kustaafishwa rasmi na Trump ππππ.
Niliwasiliana na jamaa yangu mmoja ambaye naye amestaafishwa na Trump ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye shirika moja la Kilimo huko Iringa. Jamaa alinieleza fursa za Kilimo kwenye Kulima, kununua, kuchakata lakini pia kwenye uuzaji wa pembejeo za kilimo Mkoani Iringa.
Nikapanga safari ya kwenda Iringa ili nijionee mwenyewe fursa hizo kwenye mazao ya Mboga na Matunda pia na mazao ya Nafaka hususani Mahindi. Jamaa yangu akaniunganisha na maafisa Kilimo wa Serikali kwenye Wilaya za Kilolo, Mufindi na Iringa DC.
Nilianza safari ya kutoka Dar hadi Iringa. Tukapita Morogoro nika enjoy pale Mikumi kwa kuona wanyama angalau nipunguze mawazo ya Trump na kile alichotufanyia. Nikafurahia zaidi Iyovi na yale makona na namna kuna mito inapita karibu na barabara.
Safari ikaendelea hadi Ruahambuyuni na barabarani naona vitunguu vingi vikiwa vimepandwa mashambani lakini pia vijana wakiuza vitunguu barabarani wakiweka kwenye vindoo.
Kituo changu cha Kwanza.
Kituo changu cha kwanza kilikuwa Ruahambuyuni. Nilitafuta sehemu ya kulala kisha nikawasiliana na BWANA SHAMBA FARM. Yule Bwana Shamba wa Ruahambuyuni anayejishughulisha na uzalishaji wa miche ya mboga na matunda, uuzaji wa pembejeo za Kilimo pamoja na uzalishaji wa mazao ya mboga na matunda.
Itaendelea ikiambatana na picha.
====
Sehemu ya pili

Inaendelea sehemu 2.
Nilipolelewa na yule Bwana Shamba na akaanza kunipeleka kwenye eneo lake la Uzalishaji wa Miche.
View attachment 3236486
Ni kweli yule jamaa anaitendea haki taaluma yake ya Kilimo. Anazalisha miche ya mazao ya Mboga mboga kama Nyanya, Hoho, Pilipili mwendokasi n.k. Amekuwa msaada kwa wakulima wa eneo husika na binafsi nilijifunza kuwa uuzaji wa miche ya mboga na matunda ni fursa kubwa sana kwenye maeneo ya Ruahambuyuni na Iringa kwa ujumla. Mtaalamu yule ana duka lake la Pembejeo na anauzia wakulima wanotiririka mamia kwa mamia madawa na mbegu bora za mazao lakini pia anauza na mbolea.
Tunatoka hapo na kwenda shambani kwake ambapo analima mazao mbalimbali kama kitunguu, Hoho, Nyanya na Pilipili mwendokasi.
Pale Ruahambuyuni watu wanamaanisha na unaweza juta kwanini nilikuwa nangangania kuishi Dar huku nikifanya kazi badala ya kujiajiri kwenye Kilimo. Jamaa wana skimu yao ya umwagiliaji ambayo hutumia kumwagilia mashamba yao. Nimeona aina mbalimbali za pumpu mbalimbali zilizofungwa mtoni ambazo humwagilia maji umbali wa zaidi ya Kilomita 6 hadi 10.
View attachment 3236493
Mkulima aliyevuna Pilipili Mwendokasi akiwa na noti zake.πππ