Utafiti: Wanaosafiri wana raha sana kuliko shopping

PureView zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
10,281
34,333
Utafiti mpya umeonesha kwamba Watu ambao wanatumia pesa zao kwa mambo kama vile kusafiri na kuhudhuria matukio ya burudani wana furaha zaidi kuliko wale wanaozingatia kuwekeza kwenye mavazi, kununua simu kali na vitu vingine kama hivyo ‘material goods’.

Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la saikolojia ya kijamii umeeleza kuwa kuwekeza kwenye safari huleta furaha kubwa, ukumbusho na starehe ya wakati huo kuliko shopping ya vitu kama simu na nguo.

Matokeo ya utafiti huo yalikuja baada ya kuhojiwa kwa kundi kubwa la Watu wazima waliowekeza kwenye safari ambapo walielezea uzoefu wao kama vile kula nje au kuhudhuria matukio mbalimbali ya burudani kitendo ambacho kiliwapa kiwango cha juu cha furaha kuliko wale ambao walikuwa wamenunua vitu...

Huu UTAFITI hata Mimi nakubaliana nao Kwa asilimia 100 %. Ebu vuta picha mfukoni uko vizuri alafu upo na familia mnaenda zenu mkoani kuna Hali Fulani hiviii inakuja moyoni yenye furaha Sana hasa ukiwa na chuma yenye uhakika na comfortable.
Tukutane December Huko barabarani huku unamwaga Moto
IMG_20240801_153053~2.jpg
 
Attachments

  • 20240805_150617.jpg
    20240805_150617.jpg
    426.4 KB · Views: 5
Mimi ni Traveller, huo ndio ukweli Kwa mfano nchi hii mikoa yote na makao makuu ya wilaya yote na vijiji vingi nimefika, anzia kule kigoma, lushoto, tarime, moshi, kila eneo sijui kondoa, dodoma kul mpwayungu, mpanda, yote na kuanzia nakonde hadi south, kenya to eriteia, mozambique, tswana land, wanaoijua landrover custom ya kijani defender tyre kubwa habari wanayo hadi Kwa wala nyani mbinga, Kwa wala panya newala, vindege vile vya warangi, bukavu, gisenyi, afrika ya kati, huko kusafiri ni shule kuliko kusoma degree hizi za afrika, na kila sehemu niliandika mambo mbalimbali ya huko hadi swaziland niliwahi kufika kwenye familia moja usiku naletewa binti mzuri eti nilalale nae ndio ukarimu Kwa wageni eti aniondolee uchovu na baridi
 
Hata Mimi natamani kuimaliza Tanzania nzima kabla ya kwenda nje ya nchi
 
NAAM HII NDIO JAMIIFORUMS! TUTASHUHUDIA UONGO WA KILA AINA KWENYE HII NYUZI
CC: ephen_
 
Uliza swali ujibiwe, ambacho sina ni degree tu lakini kutembea jifunze mrangi njoo umsikia huyu kijana wa mabibo sijui shamba umkumishe strong room tulikua tunafanya nini, umueleze rabamtoni ni nini ajifunze ashaanza ubishi
Kimya wewe! Unamkoromea nani?? Tupia picha acha rongorongo kijana wa tandahima kwenye magimbi!! Usikute hata nje ya kijiji chenu hujatoka
 
Umeshinda mkuu, wewe ni mtu muhimu sana tunakutegemea mno utupatie exposure, sie wa kibondo, tandahimba, nanjilinji, ilagara, ifenkenya, mlimba, litembo, majita, kifanya, himo, zerozero, murusagamba, kibirashi, mafyeko, chali isanga, iguguno, maluga, makunda, kiabakari, wale wa mitaa ya tandamti, aggrey, masasi, Mombasa, uhuru, mnazi, gerezani, kidongochekundu, popobawa, hao mko nao level moja,
 
Maneno mengi kama demu! Umeshindwa kutoa ushahidi endelea kiwadanganya wajinga
 
Umeshinda mkuu, wewe ni mtu muhimu sana tunakutegemea mno utupatie exposure, sie wa kibondo, tandahimba, nanjilinji, ilagara, ifenkenya, mlimba, litembo, majita, kifanya, himo, zerozero, murusagamba, kibirashi, mafyeko, chali isanga, iguguno, maluga, makunda, kiabakari, wale wa mitaa ya tandamti, aggrey, masasi, Mombasa, uhuru, mnazi, gerezani, kidongochekundu, popobawa, hao mko nao level moja,
Kusafiri ni zaidi ya shule. Hongera sana chief. Kuna moja naipigia mahesabu. Dar-Lindi-Mtwara-Masasi-Tunduru-songea-Sumbawanga-Katavi-Kigoma....

If you know anything here..share your experience. Tuendelee kujifunza.
 
Hii route yako bonge moja la adventure , Dar utapata chai nangurukuru, then utazuga mnazi mmoja pale kiaina unywe maji kidogo, hapo utajiandaa kuingia mtwara, utasimama na kushangaa kidogo Dangote cement, ukifika mtwara utaanzia magomeni, utaenda stand ya zamani pale ule supu ya pweza, ukitembea hapo uiwaze ndanda, then masasi, ukitoka masasi utaenda kusimama mangaka, kidogo utagonga pori hapo maeneo ya majimaji hadi kiuma hadi kilimasera pale kuna down moja matata kote huko utapita then ukifuka tunduru utanunua korosho bei nafuu kidogo ili unywe na maji hapo utapata story kiasi za mpunga, mbao pori, kitu na mziki hapo unaisaka namtumbo, songea mjini utalala iwe matarawe au bombambili, pale utapiga story za nyasa, mbambabey, utapata samaki aina ya mberere na mbufu na ugali wa muhogo sijui utalala appleline au utakua na tent najua utatamani ufike ziwa nyasa au manda huko lakini utadamka kwenda mliyayiyo uiage songea ulenge madaraja hadi lilondo upate kuku wa kukaanga na ndizi mbivu hapo utakua ushapita madaba, mkongotema umebeba tangawizi kidogo, then utapata kuiona kifanya, hapo unaitafuta njombe milima panda shuka, njombe baridi kali utapata chai ya rangi na majani ya asili, ukitoka hapo uiangalie makambako pale utapita Kwa mama anita upate dona na mbogamboga kama tisa hapo unapishana na akina mwendamseke, another G , utaacha kwenda iringa wewe unaanzia mbeya road sasa hapo uitafute halali, igawa, chimara, igurusi, itewe mara kidogo mlima nyoka, unapita dampo uyole hiyo hapo utaamua ukale supu Kwa wasomali au utajua ufanye nini halafu ukifika uyole useme tuanzie uyole kwenda mitaa ya nane nane, ilomba, mwanjelwa, simike nzovwe, unatokomea iwambi kuiona mbalizi hapo ukivuka mbali kama unaumwa utapita pale ifisi Kwa dokta rena au upate tiba kidogo halafu utajua uelekee senjele, upige mpaka mlowo, vwawa, mpemba, tunduma pale sasa utulie kidogo ndio uanze route yako kufika laela, sumbawanga, piga barabara hadi namanyere, hapo kidogo lyazumbi hiyo hapo kula supu na mbuzi choma then ianze hifadhi ya katavi utaona twiga, viboko pale mtoni, tembo kiasi hadi unaibukia stalike, hapo sasa utakua unaitafuta mpanda, ukifika mpanda wape salamu zao halafu kigoma nitakujuza up nafikaje,
 
Back
Top Bottom