UTAFITI: Instagram si salama kwa afya ya akili hasa wanawake, Youtube mambo poa

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Instagram ni App yenye madhara zaidi kwa afya ya akili ya vijana ikifuatiwa kwa karibu na Snapchat kulingana na ripoti mpya ya Royal Society for Public Health(PSPH) yenye maskani yake Uingereza.

Utafiti wao ulijumuisha vijana 1,500 wenye umri kati ya miaka 14 hadi 24 na ulihusu jinsi gani mitandao ya kijamii inaathiri afya na ustawi wao kama wasiwasi, msongo wa mawazo, kujitambua na muonekano.

Youtube pekee ilijitokeza kinara kwa kuwa na athari chanya ilhali Instagwam, Snapchat, Facebook na Twitter zote zilionekana na athari hasi kwa ujumla kwa vijana.

Instagram ambao ni mtandao wa kusambaza picha wenye watumiaji zaidi ya milioni 700 duniani unawaathiri zaidi vijana wa kike kwa kujilinganisha na vitu visivyo halisi. Inawafaya wanawake kuona miili yao sio mizuri na kusababisha kuongeza vionjo na photoshop ya uhalisia ili kuonekana wazuri.
=======


SOURCE: Gurdian
 
Hili linaukweli ndani yake,watu wana ji edit mpaka wawavinyago
 
JF ndiyo mtandao Salama kabisa, ndiyo maana mimi huwezi kunikuta kwenye mitandao mingine ya kijamii
 
Kweli mkuu tena wadada wanataka wapendeze kila siku wapost, wakila wapost, wakilala wapost, wakioga wapost... Aiseeh too much
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…