Utabiri wa Mechi ya Simba SC vs Al Masry SC, Japo Mchezo utakuwa Wenye ushindani ,Lawama kwa Refa kuwabeba na Penalty Simba atafuzu Nusu Fainali!

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
11,996
27,016
Nakuletea Utabiri Ambao Nitauchambua kwa kutumia number vibration (Numerology) na Pia Some of the astrological Effects Za siku hiyo..

Ambavyo Vyote vinaonyesha Simba Anaweza Kufuzu Aidha kwa Matuta au Atafunga ns Kusawazisha Agg.. kuwa 2:2

Haya Tuangalie..

Numerology Analysis

Tarehe ya Mechi: 09/04/2025
Jumatano – siku ya sayari Mercury (Zebaki)
Muda: Saa 10:00 Jioni (16:00)
Uwanja: Benjamin Mkapa Stadium, Dar es Salaam

Step 1: Namba ya Tarehe ya Mechi

09 + 04 + 2025 = 2038
2 + 0 + 3 + 8 = 13 → 1 + 3 = 4

Namba ya siku hiyo ni: 4

Namba 4 inaongozwa na sayari Rahu (North node/Node ya Kaskazini) ambayo inahusiana na mabadiliko(Changing), surprise (mshangao), na inahusiana pia na matokeo yasiyotabirika Kwa Urahisi..

Kwa hiyo Siku kitarehe ni siku inayongozwa na Siku ya Action zilizotabirika..


Step 2: Namba za Timu

Simba SC:
S + I + M + B + A = 1 + 9 + 4 + 2 + 1 = 17 → 1 + 7 = 8

Al Masry SC:
A + L + M + A + S + R + Y = 1 + 3 + 4 + 1 + 1 + 9 + 7 = 26 → 2 + 6 = 8

Wote Wana Jumla Numerological Value ya Nane!
Kitu kinachoongoza Ugumu zaidi kwa Timu zote Mbili..

Kwakuwa timu zote zina vibration ya 8, ambayo ni namba ya Saturn namba ya nidhamu yaani Karma ,ushindani mkali, na ukakamavu,
(Timu yoyote Itakayoonyesha Nidhamu kwenye Mpira Bila Kupanick itashinda mechi hiyo na Hapa ndo Ugumu wa Utabiri ulipoanza kwangu)

sasa Primary Conclusion ya Numerology, siku ya namba 4 (Rahu) inapokutana na namba 8 (Saturn), kuna tension na vita ya nguvu. Hii huashiria mechi kuwa ngumu sana, yenye penalti nyingi, au changamoto za waamuzi...

Japo Itakuwa na Faulo nyingi sana Na Kona Kadhaa (Wale wa Kubeti Kazi kwenu)..

Astrology Analysis

Tarehe ya Mechi: 09 Aprili 2025
Saa: 16:00 (Dar es Salaam)
Mahali: Latitude: -6.8, Longitude: 39.3
Jua liko katika Nyota ya Aries – nyota ya vita, ushindani na ujasiri.

Mwezi uko katika Nyota ya Leo (Simba) – hii inafaidisha Simba SC kwa maana ya nguvu ya kiasili na sapoti ya nyumbani.

Sayari Muhimu Wakati wa Mechi:

Mars (Sayari ya vita) iko kwenye nyumba ya 10 (nafasi ya umma, ushindi) – huashiria ushindani mkali.

Moon (Mwezi) akiwa Leo, inawapa Simba SC motisha na nguvu ya kiakili – hasa mbele ya mashabiki wao.

Mercury (sayari ya mawasiliano, kasi, na mbinu) ikiwa katika Aries – inafaidisha timu iliyo na wachezaji wenye mbinu na kasi – upande wa Simba SC.

Sasa Jibu la Mwisho na Matokeo Tarajiwa

Mechi itakuwa na matukio mengi ya kiufundi, huenda ikawa na penalti au kadi nyingi.

Simba SC wakicheza kwa nidhamu na kwa kutumia nguvu ya nyota ya Leo (na sapoti ya nyumbani), wana nafasi ya kushinda au kutoa sare yenye mabao.

Al Masry wana namba sawa ya nguvu (8) lakini hawana msaada wa nyota ya mwezi siku hiyo.

Mechi itaisha Kwa Simba 2:0 Al Masry na Wataenda Kwenye Matuta ambayo Simba Atashinda 4:2

Au Kwa hali nyingine (Japo Haitegemewi) Naona Matokeo Ambayo Sio mazuri kwa Simba Ambayo ni watafunga 2:1 Japo watashinda Ila hawatafuzu Kwenda Nusu Fainali..
Japo Pia kuna Uwezekano ikaisha kwa Penalt..

Nimewasilisha

CC: zerominus10
 
Back
Top Bottom