Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,124
- 39,265
Kuna kila dalili za ubashiri kuwa, msimu huu wa 2022/23 timu ya Yanga ya Tanzania itafanikiwa kunyanyua makombe matatu (ligi kuu, Kombe la FA (Azam confederation) na Shirikisho CAF), na hali hiyo hiyo itatokea kwa timu ya Man City ya Uingereza ambayo nayo itabeba makombe matatu (Ligi kuu, Kombe la FA na klabu bingwa UEFA).
Haya yatakuwa ni mafanikio makubwa na mafanikio ya juu zaidi kufikiwa na hivi vilabu tangu kuanzishwa kwake.
Sababu kubwa za huu Ubashiri wangu zimejikita kwenye vigezo vitano tu:
1. Nafasi walizonazo kwenye mashindano yote hayo kwa sasa.
2. Kiu ya hali ya juu iliyopo ndani ya hizo klabu kufikia hayo mafanikio.
3. Uwezo wa makocha wake kimbinu dhidi ya wapinzani wao.
4. Akiba ya wachezaji wa kutosha kuweza kufanikisha hayo.
5. Uwezo wa juu wa wafungaji wake wakuu kwenye mashindano makubwa au mechi muhimu.
MUHIMU
Hayo nimeyaandika huku nikiwa mshabiki wa kawaida wa Man City na mshabiki halisi wa Simba. Pia nimeandika hayo nikiwa na uzoefu mzuri wa kubashiri matokeo ya kiujumla ya timu katika mashindano mbalimbali. Mara ya mwisho nilibashiri humu JF kuhusu Argentina kutwaa kombe la dunia kule Qatar, niliandika ubashiri huo siku chache kabla ya mashindano ya kombe la dunia 2022 kuanza, na mwisho wa siku ikatokea kweli.