KERO  Usumbufu kupata vyeti vya watoto RITA

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba utusaidie nikiwakilisha watanzania wengi wanaopata changamoto kama mimi juu ya huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (RITA).

Mimi nimeomba uhakiki wa cheti cha mtoto online toka tarehe 8/7/24 online, but nimekuja kufuatilia kwenye mtandao kuna wengine wameomba mwezi wa sita wote hatujapata majibu ya vyeti vyetu.

Kitu ambacho si matarajio ya wengi, tulitegemea online service itoe huduma nzuri na ya haraka, lakini imekuwa mzigo na usumbufu kwa watanzania.

Nimekuwa nikitumia namba zao walizoweka ili wanisaidie cha kushangaza simu HAZIPOKELEWI.

Naomba utusaidie kutoa taarifa ili mamlaka husika iweze kusikia ombi letu.

Majibu ya RITA; Madai ya kuchelewesha Vyeti, RITA yasema imepokea maombi 143,157, yaliyofanyiwa kazi ni 61.2%

Asante
 
Back
Top Bottom