Ustawi wa Jamii; A Penny Saved is a Penny Earned; Serikali inaweza Kumpunguzia Mzigo wa Matumizi Mwananchi hivyo Kumwongezea Kipato cha Kutumia

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
14,872
23,471
Maadui wetu hawajawahi Kubadilika Umasikini, Ujinga na Maradhi..., Vilevile Mahitahi Muhimu ya Binadamu hayabadilika (Chakula Malazi na Mavazi); Karne ya sasa ambayo sio kila mtu anaweza kuchukua Jembe na kwenda kulima mihogo na kupata kitoweo Pesa inahitajika. Hii ndio itakupatia mahitaji (ukizingatia hata zile huduma za elimu na afya zimekuwa biashara).

Hivyo tutakuwa hatumtakii mema mwananchi huyu hata kile ambacho hakitoshi bado tutakichukua kwa Matozo, na kama hio haitoshi zile huduma zote ambazo ni muhimu bado tukampa kwa gharama isiyo ya lazima.

Hivyo hapa taongelea sekta chache ambazo Serikali ina uwezo wa moja kwa moja kumpunguzia mzigo mwananchi hivyo kubakia na vijisenti vya kuweza hata kuongezea kwenye manunuzi ya unga ili mwananchi huyu angalau apate milo hata miwili kwa siku.

Mapishi / Kupikia (Tanzania Nzima)
Je kwanini tunazidi kumfanya mwananchi huyu aweze kutumia gharama ya mapishi kubwa (gesi) na kumkataza kuni (ambazo angetumia bure) wakati kwa sasa angeweza kutumia Umeme ambao gharama yake kwa unit ni Tshs. 100/= badala ya 306/= ambayo atatumia kwa hii Mitungi ya gesi tunayompa?

Je, kwanini tunatumia pesa zake za Kodi kutaka kumpa ruzuku ya kupunguza bei ya gesi wakati hizo pesa tunapeleka nje ya nchi kununua hii gesi wakati tuna umeme wa kumwaga ambao tungeweza kumshushia bei hata mpaka Tshs. 20/= kwa unit?


Kwanini katika shida ya uzalishaji wa Umeme na wananchi hawana Pesa wasiwe wawekezaji wa Kuzalisha Umeme ili mwisho wa Siku tuwe na Umeme mwingi na mwananchi kuweza kupika hata kwa gharama ya Tshs 0/= jambo ambalo wanafanya sasa hivi kwa Kuni


Kwanini badala ya kuwaambia watu wawekeze kwenye Gesi na kuuza gesi ambazo tunatoa nje watu hawa hawa wasiwekeze kwenye Majiko ya Umeme ambayo umeme huo utakuwa unazalishwa nchini ?

Je ni kwamba hatujui haya au kwanini tunafanya tunayofanya?

Usafiri Kwa Dar es Salaam / Morogoro n.k.
Kwenye Usafiri hususan Dar watu wanapoteza muda mrefu sana wakiwa barabarani na sio ajabu kwa mtu kutumia mpaka elfu kumi kwa siku (pesa ambayo angeitumia kufanya mengine) au anaweza kujikuta kwa siku anapoteza masaa hata manne akiwa amekaa kwenye gari au kusubiri gari wakati angetumia muda huo kwenye uzalishaji.

Sio hivyo tu kama kuna Treni za Mwendo kasi mtu angeweza kukaa Morogoro na kufanya kazi Dar au kuleta biashara zake Dar kila siku (iwapo gharama ya usafiri ingekuwa rafiki), ila cha ajabu tunafanya hili jambo kama ni chanzo cha mapato wakati ujenzi wake umetumia jasho la huyu huyu mlalahoi ambaye tunazidi kuchukua pesa zake za kununua chakula na kupata mlo katika usafiri.

Makazi (Tanzania Nzima)
Watu walianzisha National Housing ili kuwe na affordable housing kulingana na vipato vya wananchi, ila kinachotokea hii Kampuni imejikita kwenye Biashara ambapo cost zake ni kubwa au hazina tofauti na watu binafsi ukizingatia mtaji mkubwa ulikuwa ni wa UMMA hivyo ni kama wamechukua mali ya UMMA na bado hawana Msaada kwa UMMA.

Internet Bundle / Mitandao / Mawasiliano / Huduma za Miamala
Kuna kipindi East Afrika tulikuwa tumepiga sana hatua katika financial inclusivity ambapo hata bibi kijijini alikuwa na Benki mikononi mwake aliweza kutumiwa pesa bila shida na ndugu yake mjini, matokeo yake yakaja matozo (sijui tunakata ili tutoe huduma gani wakati kila huduma imekuwa biashara) kwahio kasi ya watu kuwa financially included ikapungua sana.

Leo hii Shule imekuwa kwenye mitandao na vijana wengi ambao tumeshindwa kuwapa ajira zenye ujira wanabangaiza kwenye mitandao ili kujiokotea vijisenti (ukizingatia dunia imekuwa kijijini) lakini yet serikali imesababisha bundle hazishikiki



Hitimisho
Kwa hayo yote hapo juu inabidi tujiulize tunafanya nini na kwa faida ya nani na kwanini ? Is it Naiveté au Malevolent
 
sawa tumesikia, ngoja tukalijadili na vyombo vyetu vichunguze kwa kina
Kwamba mlikuwa / walikuwa hawajui haya ?

Nadhani labda nachofanya ni kuwaambia wananchi wenzangu sababu wangejua haya wangekuwa wanauliza maswali zaidi ya kumeza kila wanacho / tunachotengewa...

Na kila hawa watu wakija na Hekaya zao kutafuta Kura za kwenda Kula badala ya kuwa wasikilizaji tungekuwa tunawahoji pia...
 
Back
Top Bottom