CUF Habari
JF-Expert Member
- Dec 12, 2019
- 239
- 234
USIYOYAJUA KUHUSU PROFESA LIPUMBA KATIKA SAFARI YAKE YA KISIASA NCHINI TANZANIA.
Posti hii tunaiandika mahsusi kwa ajili ya wale ambao huenda kwa miaka mingi walikuwa wakiishi nchi za nje, kiasi cha kutoyajua matukio muhimu ya kisiasa nchini, tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mnamo mwaka 1992.
Wengine watakaofaidika na posti hii ni wale ambao umri wao ni miaka 30 au chini ya hapo. Hawa umri wao unakaribiana na umri wa uwepo wa awamu ya pili ya mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa nchini, na kwa sababu hiyo yapo mengi ambayo yamewapita. Mwaka 1992 wakati mfumo wa vyama vingi vya siasa unarejeshwa wengi bado walikuwa hawajazaliwa; na wachache waliobaki walikuwa watoto.
Umuhimu wa posti hii ni mkubwa ukizingatia kuwa ni wachache wanaoijua historia halisi ya mchango wa mwanasiasa nguli, Fullbright Professor Ibrahim Haruna Lipumba, katika kupigania mageuzi ya kisiasa hapa nchini.
#Mwaka 1995 Professor Lipumba alifunga akaunti yake ya benki ili kupata fedha za kampeni. Hatua hii ilikuja baada ya kugundua kwamba viongozi wa CUF wa wakati huo walikuwa wamemdanganya akatangaza azma ya kugombea urais wakati kimsingi hawakuwa na maandalizi yoyote. Kwa kuchelea kuharibu heshima yake mbele ya jamii Professor Lipumba aliamua kuwa bora atumie gharama zake mwenyewe, japo kwa uhakika alijua kuwa hawezi kushinda.
#Mwaka 1998, Professor Lipumba akiwa hana cheo chochote ndani ya CUF, alianzisha operesheni kubwa ya kuijenga CUF upande wa bara, baada ya kurejea kutoka Ulaya alipokuwa amekwenda kufanya kazi ya kufundisha kwa muda. Ni katika kipindi hicho matawi maarufu ya Kosovo, Chechnya, Kandahar, Sadam Hussein, Mashujaa wa Mwembechai, nakadhalika yalifunguliwa.
#Mwaka 2,000 mwishoni, kama ilivyo sasa, rais Mkapa alijaribu kuzuia shughuli za vyama vya siasa. Hivi aliyemzuia ni nani kama siyo Professor Lipumba, pale wakati huo ukiwa ni Mwenyekiti wa chama, alipotangaza maandamano makubwa January 27 mwaka 2001?
#Kuanzia mwaka 2,000 kulikuwa na kampeni kubwa dhidi ya UFISADI wa kitaasisi uliokuwa unaendelea nchini.
Hivi ni nani, kama siyo Professor Lipumba, aliyetoa tahadhari kwa mara ya kwanza kwamba Taifa lilikuwa linaibiwa kwenye mikataba ya dhahabu kwa sababu Tanzania ilikuwa inaambulia mrabaha wa 3% tu, na baada ya kuilipa kampuni ya ukaguzi, ikikuwa inaambulia alibaki ya 1.9% tu?!
Hivi nani, kama siyo Professor Lipumba, aliyetahadharisha kuwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA ulikuwa umekodishwa kwa dola 800 tu kwa mwaka?!
Hivi ni nani, kama siyo Professor Lipumba, aliyeasisi msamiati wa MAPAPA NA MASANGARA ya UFISADI?!
#Misamaha ya madeni kwa nchi masikini sana duniani.
Wale waliokuwa na akili za kuweza kupambanua mambo enzi ya urais wa Mkapa, bila shaka wanakumbuka jinsi serikali yake ilivyojisifu kwa Tanzania kupewa msamaha wa madeni, wakati ule.
Hata hivyo ni wachache sana wanaojua kiini cha msamaha ule.
Kiini cha msamaha ule ni mpango ulioratibiwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF), kuanzia mwaka 1996, wa kuzisamehe madeni nchi masikini sana, ambazo zilikuwa zimeelemewa na mzigo mkubwa wa madeni (Heavily Indebited Poor Countries, au HIPC kama zilivyojulikana kwa kifupi).
Lakini je, huu mpango ulianzia wapi? Kuzaliwa kwa mpango huu kulianzia pale mchumi nguli, Fullbright Professor Lipumba, alipowasilisha utetezi katika kamati ya Bunge la Marekani (Congress), - House - Sub Commitee on International Development, Finance, Trade & Monetary Policy; kuhusu matatizo ya madeni ya nchi za Afrika, mwezi Februari 1994.
Mwaka 2015, baada tu ya uchaguzi mkuu, rais Magufuli alizuia tena shughuli za kisiasa. Amefanikiwaje wakati Mkapa alishindwa?!
Jibu ni jepesi. Wakati zuio linatangazwa Professor Lipumba alikuwa amejiuzulu uongozi wa CUF akipinga hatua ya Maalim Seif na Freeman Mbowe kusimika pandikizi la CCM, Edward Ngoyai Lowasa, kugombea urais kwa tiketi ya upinzani.
Kuna kila sababu ya kuamini kuwa iwapo Professor Lipumba bado angekuwa kwenye hatamu za uongozi wa CUF rais Magufuli asingefanikiwa.
Kwa sababu Professor Lipumba hakuwepo, jukumu la kumzuia MAGUFULI liliangukia kwa wale wanaojitangaza kuwa wao ndio 'WAPINZANI WA KWELI'.
Sasa mbona hatukuona lolote, na badala yake tukaona foleni kubwa ya WABUNGE NA MADIWANI wa UKAWA wakirudi CCM kwa madai ya kumuunga mkono MAGUFULI?!
#Mwaka 2015 Lipumba alikataa kuunga mkono mchezo wa karata tatu uliokuwa unachezwa na MBOWE, MAALIM SEIF NA CCM.
CCM ilipanga kumsimika Lowasa kama mgombea wake namba 2 kupitia UKAWA na kwa kusaidiwa na WAPIGA DILI, MBOWE NA MAALIM SEIF, walifanikiwa.
Uchaguzi ulipokwisha Lowasa na Maalim Seif wakatumika kutuliza makundi ya mihemko na mambo yalipokaa LEVEL Lowasa akatangaza kurudi NYUMBANI!!!
Wakati Lowasa anarudi 'NYUMBANI' Mwenyekiti wake wa chama, MBOWE, alikuwa gerezani; huku mwanaharakati mkuu wa chama, TUNDU LISU, akiwa anauguza MAJERAHA ya risasi nchini UBELGIJI. Shame! Hicho ndio kipimo cha utu wa hilo pandikizi la CCM.
Mwaka 2016 kundi la wanachama wa CUF walimwomba Professor Lipumba arejee katika uongozi wa chama. Hoja mbalimbali zilimshawishi akakubali. Hakurudi kinyemela. Alimwandikia Katibu mkuu, Maalim Seif Shareef Hamad, barua ya kutengua kujiuzulu kwake. Pamoja na kwamba hakukuwa na pingamizi la kikatiba, Maalim Seif Shareef Hamad hakuridhia akaamua kwenda mahakamani kumpinga Professor Lipumba. Kitendo hiki kilizaa mgogoro uliokigawa chama katika makundi mawili.
Jitihada mbalimbali zilifanywa kuyasuluhisha haya makundi lakini ziligonga mwamba. Wakati katika kipindi chote Professor Lipumba alikuwa radhi kufanyike suluhu, Maalim Seif katika kipindi chote alikataa kata kata kusuluhishwa.
Hivi sasa CCM wako kwenye harakati za kumleta LOWASA mwingine UPINZANI.
Uwezekano mkubwa ni kwamba safari hii ataibukia ACT WAZALENDO.
Kitendo cha MAALIM SEIF baada ya kushindwa kesi kuacha kujiunga na maswahiba wake wa CHADEMA, NCCR au NLD, na badala yake akaenda ACT ndio dalili kwamba maandalizi ya kumpokea huyo mamluki wa CCM yameanza kupitia chama hicho!