Usipokuwa mwanaume wa maana mkeo hawezi kubali kuitwa kwa Majina yako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
25,654
61,561
USIPOKUWA MWANAUME WA MAANA MKEO HAWEZI KUBALI KUITWA KWA MAJINA YAKO.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Moja ya dalili kuwa wewe sio mwanaume aliyefanikiwa ni pamoja na kuangalia kama mkeo anatumia majina yako na anayafurahia.
Ukiwa mwanaume uliyeshindwa, usiye na hadhi, mwanaume usiye wa maana hakuna Mwanamke ambaye atapenda aitwe kwa majina yako.

Mfano, mkeo anaitwa Aneth Alfonse kadobe. Hilo ndilo jina ulilomkuta nalo.
Alafu wewe unaitwa Sadick Aidan Njiwa.
Mkeo hawezi kukubali kuitwa Mama Njiwa au Aneth Njiwa. Atajitambulisha kwa majina ya ukoo wake.

Ni vizuri kuelewa saikolojia ya mahusiano hasa kwa Wanawake jinsi inavyofanya kazi.

Ukiona Mkeo anakataa kujiita kwa majina yako ujue kuwa hadhi yako ipo chini ukilinganisha na hadhi ya kwao. Yaani hujafika pale alipokuwa anataka ufike.

Wanawake wakiolewa na wanaume wa ndoto zao. Hawaoni shida kubadilisha chochote kwaajili ya waume zao. Ikiwemo jina lao.

Hapo utakuta Kina Misheli Obama, Salma Kikwete, Janeth Magufuli, Maria Nyerere n.k.

Mwanamke Kutumia jina lako kuna tafsiri nyingi mno. Mojawapo ni anajivunia wewe, pili anakuheshimu na kukuona wewe ni mtu wa maana.

Elewa kuwa ni uamuzi wa Mkeo kuamua kuchukua majina yako au kutoyachukua. Hivyo sio umlazimishe mkeo kuchukua majina yako ikiwa yeye anakuona huna la maana, huna hadhi na heshima hiyo.
Muache Mwanamke atumie majina yako kwa hiyari yake mwenyewe.

Elewa kuwa, Wanawake pia kama hueleweki hawapendi hata jina lako litumike kwa watoto wao. Kwao huona aibu na kujishushia thamani.

Mwanamke kiasili kaumbwa kwa uzuri wa nje na kupenda kuona vitu vizuri. Iwe ni uzuri wa kimaumbile, kifedha au urembo.

Hakikisha familia yako, inatambulika kwa jina lako(wewe mwanaume). Sio kwa Mama Fulani, bali kwa mzee Fulani.
Hakikisha Mkeo akijitambulisha ajivunie kina lako. Mfano, mimi ni Mama fulani(jina lako).

Elewa kuwa Mwanamke asipoheshimu na kuthamini jina lako basi mpaka watoto na wajukuu zako hawatalithamini wala kuliheshimu.
Yaani utakuwa mzee uliyeshindwa na kudharaulika.

Usije ukaleta ukoloni wako wa kibwege au mfumo dume wa kijinga ukidhani ndio utajenga heshima ya jina lako. Ubabe wa kijinga utazidi kukuharibia.
Taikon najua Ubaba ni Ubabe, hata mimi natumia hiyo. Lakini ubabe wa haki, maarifa, akili, ujuzi, na mambo memba.
Sio ubabe wa kipuuzi na kijinga. Wewe utakuwa Mpumbavu tuu.

Hakikisha unajua mambo mengi kiasi kwamba kwenye mambo ambayo mkeo atakuuliza basi 80% uwe na majibu ya maswali yake.
Mwanaume ni multichoice, multiplayer, na multipurpose.

Mwanamke anataka umsikilize lakini usimsikilize kwa kila kitu. Kumsikiliza inamaanisha kuheshimu maamuzi yake. Na kama utafanya tofauti uwe na maelezo toshelevu yenye hoja shawishi akuelewe.
Mwanamke usitumie nguvu kudili naye. Atakushinda mapema sana. Na wewe hutojua amekushinda mpaka siku ukianza kuona amebadilika jua ameshayazoea Maguvu yako.

Njia pekee ambayo Mwanamke atakuheshimu ni kumzidi Akili na maarifa. Kwa sababu wanawake wengi ni Watu wakutumia Trick nyuma ya hisia zao kuzubaisha wanaume wajinga na wanaotumia nguvu.

Ili Mwanamke ajivunie jina lako na alitumie. Uwe na moja ya mambo yafuatayo;
1. Akili na ujue kuzitumia
2. Mali kulingana na wakati husika
3. Umashuhuri fulani kama kipaji kwa kiwango cha juu.
4. Cheo au Mamlaka
5. Handsome Boy.
Ukiwa na hayo Mwanamke hata uachane naye bado atajivunia Historia aliyoipitia kuwa na wewe. Hata akisimulia rafiki zake au wajukuu zake lazima kuna Sehemu lazima akutaje.

Taikon nimemaliza. Mwenye swali aweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kiukweli yule mwanaume nampenda sana ila majina yangu nitaendelea kubaki nayo.

Sio busara kubadili majina/ubini wa kwenu kufuata wa mume.
Mapenzi yetu yatabaki kuwa palepale na majina yangu yatabaki kuwa palepale.

Nikiitwa Mrs…… inatosha ila sio kubadili kabisa majina.
 
Kwanza kumbadili mkeo jina la baba yake na kuweka lako ni unyanyasaji. Sasa wewe ndo unakuwa baba yake wakati mnalala kitanda moja. Uzungu huu pyuuuuuuuuu

Unajua maana ya hiyari?

Unajua maana ya Unyanyasaji?

Mtu anaweza kujiita jina lolote lile hata na ubin wowote ule. Lakini hiyo haibadilishi damu yake.
Majina na sio naturally ni mambo ya kutunga tuu kulingana na utashi wa mtu. Hata mtoto wako anaweza kujiita jina lolote na akaondoa majina yako na isiwe kosa kisheria, kidini na kivyovyote vile.

Mke kujiita majina ya mumewe ni hiyari yake. Na wala hatakiwi kulazimishwa
 
Kwani hii dunia ni yetu.?
Aliskika yule jamaa wa Arusha anajiita majanaba.

mambo mengine tunayaacha tu yaende kama yalivyo.
 

😃
Ndio maana ya Hiyari.
Hata kumpenda ulimpenda kwa Hiyari yako.
Majina ni utashi wa mtu kulingana na hiyari yake, maamuzi yake.

Mwenye amri ya kubadilisha majina ni Wewe mwenyewe na Mungu muumbaji.

Pia inatokana na mtazamo ambao upo sehemu ya utashi wa mtu au jamii husika.
Ila jina ni hiyari ya mtu. Na unaposema hiyari unazungumzia upendo, kadiri moyo utakavyokutuma.
 
hivi hua mnabadili kabisa majina kisheria? mimi nikajua ni kama mazoea tu ila sio kitu rasmi
 
Ukiona mke anaitwa mama fulani, jua hilo jina hajajipa yeye bali wanamzunguka. Anaitwa hivyo kwa sababu majina ya ukoo wake mara nyingi huwa hayafamiki, hivyo huitwa jina la mume wake ambaye kwa wakati huo hua anafahamika kulingana na majukumu yake.
 
Sio kitu Rasmi. Ila wapo wanaobadili kisheria hawa ni wachache Sana.

Mimi najua wanajiita majina ya waume zao lakini kwenye karatasi huitwa majina ya koo walizotoka
Kuitwa majina ya waume zao ni heshima tu kwa wanawake na utambuzi, hasa hutumika kwa viongozi kama utambuzi wa moja kwa moja kwa wenza wao.
Huku uswahilini hali ni tofauti kabisa.
Kwanza kama upo normal kuanza kuhangaika na mwanamke eti aitwe kwa jina lako huo mda unaupata wapi?

Mambo ni mengi mda ni mchache sana ,mwanaume fanya mambo yako usisumbuke na kutafuta furaha ya mwanamke,hakuna mda wa kuridhisha mwanamke eti ili aitwe kwa jina lako.

Kama haridhiki achana nae ,kwani jina linaleta ugali mezani.Acha aitwe majina ya kwake,ikimpendeza aitwa vyovyote anavyo furahia yeye.
Hukumzaa wewe,jitu zina meno therathini na mbili uanze kuwaza mwanamke aitwe kwa jina lako.
Hayo mambo ya majini waachie viongozi wa serikali na wanasiasa kujikweza kwa wanachi wao na kujimwambafai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…