Usipendelee kupaki gari chini ya miti mathalani gari za Mzungu

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,381
9,726
Huu uzi nmebase kwenye gari zote ambazo ECU (Control box) ipo upande wa engine ambapo zaidi ya asilimia 90 ya gari za Ulaya na Marekani zinaingia hapo.

Ingawa zipo gari nyingi tu za Asia ambazo control box imefungwa upande wa engine mfano kuna nissan moja nimesahau tu model yake ila ina engine ya mr20de nilikuta na yenyewe ina control box upande wa engine.

Na kwa gari za Asia nyingi wameanza kuweka baada ya miaka ya 2005.

Gari za Mzungu mathalani Audi, Volkswagen, Mercedes Benz na BMW, Control box yake imewekwa karibu sana yanapopita maji ambayo yanashuka chini kutoka kwenye kioo cha mbele.

audi-a5-ecu-location-1.jpg



Hapo walipoweka siyo pabaya ila shida kama kama njia ya maji itaziba, na sababu kubwa ambayo nimeiona kwanye gari nyingi ni sehemu hiyo kujaa majani ya miti.

Nina mfano wa gari (Audi A4 2.0) ambayo hiyo sehemu yanapopita maji yamejaa majani ya miti na hivyo ilipekekea maji kuingia kwenye sehemu inapokaa control box

Kilichotokea ni kama hiki. 👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾

View attachment IMG_20210930_112629.jpg

View attachment IMG_20210930_112659.jpg


Kwa kifupi maji yaliingia kwenye hiyo connector, pins zikawa corroded gari ikatrigger codes kibao.

Hiyo gari niliwahi kuiongelea kwenye uzi huu👇🏾unaweza kuupitia,

Thread 'Gari za Ulaya/Marekani hazitaki ubabaishaji kabisa' Gari za Ulaya/Marekani hazitaki ubabaishaji kabisa

Hii gari ilikuwa na error codes 15 kwenye engine tu na hata uxifuta halafu ukaendesha zinarudi zote kama zilivyo






Screenshot_2021-10-03-15-34-26-566_com.us.thinkdiag.plus.jpg

bxhd

Sasa baada ya kuwa maji yameingia pale kwenye connector na pins zimecorrode, kuna wire pia zilipiga shoti na zikawa zimekatika... Na hiyo ni ndani ya control box.

Mojawapo ya huo waya ni huu nitakaoweka hapa chini kwenye picha na video hizi.

View attachment IMG_20211003_154510.jpg




Anyway nilisafisha hiyo connector nikapima control box na kwenda kuunga sehemu zilizokuwa zimekatika.

Kuja kufunga ECU, engine ikawa mpya yaani jino moja tu, ishu zilizokuwa zimebaki ni

1. Cooling fan control module ambayo kuna nyaya zilikatika so gari ikawa inachemsha, so tuliziweka sawa,

2. Camshaft position sensor, hii mafundi waliwahi kuikata wakati wanaichomoa, Connectors nyingi za Audi na VW ni rahisi kuzikata kama hujui kuzichomoa, so tulinunua nyingine tukafunga.

3. Thermostat, Hii tumeiacha pending kwanza maana bei yake tu ikiwa mpya ni Tsh. 274000/=

So far engine iko fresh sasa hivi, check engine inezima, nimerekebisha na ishu zingine kama taa, airbag n.k, somehow gari imekaa fresh, ishu nyingi zilizobaki ni mechanical.

Kama una tatizo na gari yako au unahitaji Computer Diagnosis nicheck.

Iwe gari yoyote ndogo ya Ulaya, Asia au Marekani tunapima na kusolve matatizo.

Nipo Dar.

0621 221 606.
 


Video ambayo nilirekodi. Hapo unaoonekana mojawapo ya wire ambao uliwaka moto mpaka ukaktika mpaka rangi yake imebadilika.
 
Back
Top Bottom