Usipate tabu, Anza kujipenda

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Jipende kwanza wewe kabla hujajitoa Kimasomaso
na Kimuhemuhe chako cha Mahaba na kujibeba
mzobemzobe na kuubwaga moyo wako mwaaaaaaaah chini kwa mtu mwingine kwa Mahaba shantashanta halafu huyo unayedhani
anastahili kupendwa kuliko unavyojipenda anaishia kuumwagia moyo wako Tindikali mchana wa Jua kali!

Wengi tunaumizwa kwa sababu tunawapa watu
wengine nafasi kuuuubwaaaaa kwenye mioyo
yetu tukidhani wana miujiza na watatibu maradhi
yetu ya moyo kwa Mwarobaini...Jamaa wakizingua tunaumia nusura kukata roho.JIPENDE KWANZA

Ujue wazi kujisumbua kumfurahisha mtu mwingine
zaidi ya unavyojifurahisha nafsi yako ni kujikosea
adabu na kujinyima kusiko na akili...Bila yeye pia
unaweza kuishi, unaweza kuenjoy maisha, unaweza
kusmile..

Furaha yako haiko kwenye Remote ya Mwanaume/Mwanamke mwingine
Kutegemea mtu mwingine akupe Furaha utasubiri
sana, Dunia imejaa Heart Breakers tu, wako kila
kona, kila unayempa moyo ana gudulia la
Tindikali, ananyunyizia tu kama anamwagilizia
mbolea ya DDT kwenye Mahindi..

UTALIA KILA SIKU Kujipenda ni Rahisi sana,Jipe Raha, Ukisubiri
Kupendwa dunia ya leo ni ngumu kama
kumfikisha kileleni Changudoa wa Corner
Bar, labda utumie mwiko...Love Yourself
First, Ukipendwa iwe BONUS tu.
Kwa Hisani ya Wanaume wote Tulio Dimbwini bila Vigudulia vya Tindikali mkononi!
 


Wewe kijana usilete upuuzi wako hapa....unataka nijipende nikikamatwa na Kigwangala na kupelekwa central, je?
 
ha haaa haaaa sirudii tena mkuu
Mimi yalinikuta, so take care, hata ile kukomenti bila kusoma thread skuizi hawataki...
Zile
''SIJAISOMA LAKINI NAJUA TU FLANI NI NOMA''
AU
''NGOJA NIKOMENTI ALAFU NITASOMA BAADAE''
 
Wewe kijana usilete upuuzi wako hapa....unataka nijipende nikikamatwa na Kigwangala na kupelekwa central, je?
Hahahah... Sijasema uwapende watu wa jinsia yako, NO!
Unatakiwa ujipende wewe mwenyewe, hii itakuepusha kumkabidhi moyo wako mtu ambaye haeleweki
 
Hahahah... Sijasema uwapende watu wa jinsia yako, NO!
Unatakiwa ujipende wewe mwenyewe, hii itakuepusha kumkabidhi moyo wako mtu ambaye haeleweki


Kwa sasa hali ni mbaya hapa nchini hizi si zile zama za Kikwete yaani kila kitu magumashi. Kwa sasa viongozi wetu wanataka Tanzania ya ukweli na yenye heshima.....nikijipenda ninaweza kuwekewa mashaka kwa nini najipenda na ninajipara kwa sababu gani? Wataniomba kuangalia profile yangu Insta na fesibuku kuona kama nina mapozi ya kitatanishi. Toka Kigwangala atangaze vita na watu wanaojipenda, nimeacha kuoga na situmii tena deodorant. Kazi kwao wapanda daladala wenzangu.
 
Kigwangala alitangaza vita dhidi ya Yule mchele mchele James delicious.....
Acha kupotosha
 
Hahahahaha Wewe kweli ni Mbongo halisi, manake sifa zote unazo hahaha
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…