Usiogope kuoa kwa sababu ya gharama za kuoa, hizi ni njia rahisi nimekuwekea hapa, chagua itakayokufaa

Llio 002

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,633
2,040
USIOGOPE KUOA KWA SABABU YA GHARAMA ZA KUOA, HIZI NI NJIA RAHISI NIMEKUWEKEA HAPA, CHAGUA ITAKAYOKUFAA

GHARAMA ZA KUOA NI HIZI

(1) nauli ya kwenda ukweni na kurudi watu wazima wawili mfn 45000 x 4 = 180,000
(2) kishika uchumba ya kwenye bahasha 30,000
(3) nauli yako na mtu mmoja ya kwenda ukweni na kurudi 45,000 x 4 = 180,000
(4) mahari andaa 400,000 hata ukitajiwa milion 10 ww toa 400,000
(5) ela ya pete 2 za 5,000=10000
(6) ela ya vyeti viwili vya ndoa 40,000
(7) ela ya kula njiani wakati wa izo movements ni 50,000

Jumla kuu kabisa hadi unaoa kwa mchanganuo huo hapo juu ni 890,000

PLAN B
(1) MAHARI 360,000
(2) PETE 2 = 10,000
(3) ELA YA VOCHA 15,000
(4) ELA YA VYETI 40,000
(5) NAULI YA KUMTOA MCHUMBA WAKO HUKO ALIPO KAMA HAISHI KARIBU NA WW KWA WAKATI HUO 60,000.
JUMLA NI 485,000
#NB 15,000 YA VOCHA ni kwaajili ya kuwasiliana na ukweni hadi mchakato unakamilika bila kwenda kwao, atakayetaka kuishuhudia ndoa yako basi aje kwa gharama zake mwenyewe

PLAN C
(1) ELA YA PETE 2 za 1000=2000
(2) ELA YA VYETI VYA NDOA 40,000
(3) ASANTE/MAHARI KWA WAZAZI WA MCHUMBA WAKO 150,000
(4) VOCHA 5000 YA KUWASILIANA NA UKWENI
JUMLA NI 197,000

PLAN D NA YA MWISHO

(1) ELA YA PETE 2 za 500 = 1000
(2) ELA YA VYETI VYA NDOA 40,000
(3) 1,500 KIFURUSHI CHA CHUO CHA KUWASILIANA NA UKWENI
(4) 20,000 YA KUTUMA UKWENI KAMA JUST KUSEMA ASANTENI WAZAZI WETU KWA KUMLEA BINTI YENU, NAOMBA MSINITAJIE MAHARI WALA NINI, NAWAOMBA MNIPE BINTI YENU NIJENGE NAYE FAMILIA.

JUMLA NI 62,500

Kama utakuwa na swali zaidi karibu PM
 
Kuoa ni kuamua tu na kuamua ni kuwa tayari kuoa size yako maana size yako ni yule utakayeweza kumlipia gharama kama vile mahari, n.k
 
Harusi za kiislamu kiasili hapa Tanzania ni gharama nafuu sana unless kama
1/Unataka ifanane na zile za kikristo au kimagharibi. (Huko ndio swaga za Ufahari wa Harusi zilipoanzia na kujikita kwa karne nyingi sana)

2/Wanandoa wana uasili wowote wa Kiarabu, Maarufu sana, Viongozi wa juu wa kisiasa nk. (Inalazimisha kumantain Status ya Nafasi yako kwenye jamii hususani aina ya marafiki na watu wenye uwezo wanakuzunguka)

3/Suala la dini(Uislamu) sio Agenda ya muhimu (Hapo idea za Kibagani za matumizi ya Anasa zinajiingiza)

4/Umeunda kamati ya Harusi na kukusanya pesa za Michango ya Harusi(Hapo unawajibika kuwaridhisha waliokuchangia na pia utaliwa pesa na wanakamati)

USHAURI WANGU.
*Kama wewe ni muislamu basi fanya harusi isiyo na fahari au gharama kubwa ili kupata swawabu na kulinda utamaduni wa harusi za kiislamu.

*Kama unao uwezo wowote wa kipesa, kwepa kabisa suala la kuunda kamati ya kukusanya michango na kufanikisha harusi yako.

*Kaa na ndugu zako wa karibu sana kuona namna unaweza kufanya harusi yako kiislamu na kinyumbani zaidi.

*Budget ya harusi inategemea, ila kiufupi, kiislamu mambo muhimu ni haya tu.
1/Chakula(Ubwabwa)
2/Vinywaji(Soda).
3/Burudani(Kaswida)
4/Mavazi(Kanzu, Kofia, Kiremba, Gauni, ina)
FROM Zanzibar-ASP
 
Back
Top Bottom