Usioe/kuolewa na mnyanyasaji wa Wanyama wa majumbani

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
4,023
14,177
Baada ya kuandika uzi nikiiomba serikali yetu itunge sheria kali kuwalinda wanyama wa majumbani eg. Paka, Mbwa n.k. Nimeona sio vibaya tukalijumuisha hili suala kwenye uwanja wa mapenzi/Mahusiano.

Mimi Mjanja M1 ni kati ya watu ambao nathamini sana Uhai wa kiumbe chochote na ni moja kati ya watu ambao ninachukizwa sana na watu makatili wasiokuwa na ubinadamu ndani yao.

Ewe Kaka/Dada ambae hujaingia bado kwenye Ndoa ningependa kukutahadharisha sana kwamba isitokee ukaingia kwenye Ndoa na mtu mwenye ukatili kwa Wanyama, ukimuona mpenzi wako anafanya ukatili kwa kiumbe chochote bila ya sababu/kisheria basi tambua kuwa huyo hakufai na anaweza kukudhuru au kukufanyia ukatili kwenye maisha yenu ya Ndoa.

Ukimuona mtu anatesa wanyama tambua kuwa mtu huyo ana roho mbaya na ana ushetani ndani yake, usimruhusu mtu wa aina hiyo awe Mume/Mke maana anaweza kukufanyia anayowafanyia wanyama (Unyanyasaji/Mateso).

Binadamu tumeumbwa kwa upendo unapoona binadamu mwenzako anawatesa wanyama basi tambua kuwa huyo sio mtu sahihi kwako (MKIMBIE HARAKA SANA).

✍️ Mjanja_M1
 
100% naunga mkono uzi.
Sawasawa.Unajua idadi ya sisimizi(na wadudu wadogo wengine wasioweza hata kuonekana kwa macho)uliokwisha wauwa hadi umri huo kwa kuwakanyaga ardhini?
 
Kuna kitu kinaitwa dhamira, kama umedhamiria kuangamiza kiumbe ambacho sio kitisho kwako wewe ni mkatili.

Wewe unamuelewa mtu anayemtegea sumu mbwa au paka ili afe? Au anamsogelea na gari ili amgonge au anamkata mapanga kisa kapita karibu na bucha lake.

Kuna kisa kimoja jamaa alikuwa na bucha sasa kulikuwa na mbwa wanazagaa zagaa wanakula mifupa ile na vinyama siku moja jamaa akatoka na panga akamkata mmoja panga.

Bahati mbaya yule mbwa alikuwa na mimba kakimbia na kilio huku vitoto vinadondoka tumboni, yule mbwa akafa.

Balaa likahamia kwa jamaa kila mke wake akipata mimba inakuwa kidogo miezi minne tano inatoka, hadi leo hajawahi kubahatika kulea ujauzito wake akazaliwa kiumbe.

Hii ni tukio la kweli kabisa, so watch out Mkuu.
 
Simulizi yako ni nzuri.Turudi Rau madukani;-
-Ulianza kuelewa lini kwamba ardhini,iwe juu au ndani ya ardhi kuna wadudu unaoweza kuwakanyaga au kuwadhuru kwa aina yoyote hata kuwaua?
-Ulipojua kuwa unaweza kuwaua na wewe una "huruma" kwao,ulifanya nini?
-kitu umeshajua na bado unakifanya(wadudu wapo ardhini na unawaua) kwa nini tusikuite una dhamira mbaya/evil intentions ya kuwaua?
-umetubu kwa kuwadhuru?
-hatua gani umejipendekezea ili mambo hayo yasijirudie?
 
Baada ya kuandika uzi nikiiomba serikali yetu itunge sheria kali kuwalinda wanyama wa majumbani eg. Paka, Mbwa n.k. Nimeona sio vibaya tukalijumuisha hili suala kwenye uwanja wa mapenzi/Mahusiano.

Mimi Mjanja M1 ni kati ya watu ambao nathamini sana Uhai wa kiumbe chochote na ni moja kati ya watu ambao ninachukizwa sana na watu makatili wasiokuwa na ubinadamu ndani yao.

Ewe Kaka/Dada ambae hujaingia bado kwenye Ndoa ningependa kukutahadharisha sana kwamba isitokee ukaingia kwenye Ndoa na mtu mwenye ukatili kwa Wanyama, ukimuona mpenzi wako anafanya ukatili kwa kiumbe chochote bila ya sababu/kisheria basi tambua kuwa huyo hakufai na anaweza kukudhuru au kukufanyia ukatili kwenye maisha yenu ya Ndoa.

Ukimuona mtu anatesa wanyama tambua kuwa mtu huyo ana roho mbaya na ana ushetani ndani yake, usimruhusu mtu wa aina hiyo awe Mume/Mke maana anaweza kukufanyia anayowafanyia wanyama (Unyanyasaji/Mateso).

Binadamu tumeumbwa kwa upendo unapoona binadamu mwenzako anawatesa wanyama basi tambua kuwa huyo sio mtu sahihi kwako (MKIMBIE HARAKA SANA).

✍️ Mjanja_M1
Mkuu kwani Dini ya kiislam inanimate kuhusu mnyama Mbwa?
Kuna Muislam tena kafunfa Ramadhani anatabia ya kumpiga Mbwa na kumfukuza tena akimkuta kalala anq mpiga kwa jiwe kubwa na kumwaga maji pale alipokuwa kalala Mbwa na kupasafisha. Je hii ni sawa Kiimani?
 
Back
Top Bottom