Usioane na mbadala, eti utampenda mbele ya safari

Magical power

JF-Expert Member
Sep 27, 2022
1,723
4,696
Usioane na mbadala, eti utampenda mbele ya safari, kujifunza kumpenda mtu ukiwa naye ni changamoto sana kwasababu matarajio yako yasipokuwa vile utamanivyo huku ukiendelea kuzaa naye, kupoteza muda wako ni mateso 😢

Mungu ataendelea kukutanisha na wale watu wa aina yako kila leo wakiwa single au yule mtu aliyekuwa naye ukamwacha ukaoana na huyo utakapoendelea kukutawala moyoni na akilini

Wakati mwingine atakuwa anakupigia simu kukusalia au utakapoendelea kusikia habari zake njema ama za mafanikio yale aliyokuahidi anatamani siku moja awe hivyo, ukamtia moyo na sasa amekuwa vile alivyotamani ila wewe haupo kwenye maisha yake ya mafanikio hayo

Wapo watu wanaishi na watu kimwili ila hisia zao zipo kwa watu wao wa zamani au wale wa ndoto zao waliwatamani wawe nao walioana na wale walionao kwasababu ya wazazi wao walitaka, upweke, haraka zao za kuwa ndoani

Walipo hawana AMANI moyoni ingawa kwa nje wanaoneka wameyapatia MAISHA ila hawana AMANI ya moyo kwasababu wanaishi na watu wasiopenda au wasio na hisia hao watu kabisa.
 
Back
Top Bottom