Usijipe umuhimu kwa mtu ambaye haoni umuhimu wako

RIGHT MARKER

Senior Member
Apr 30, 2018
118
413
Siku hizi watu wanapokea simu ambazo zina umuhimu, zina faida, zinawapa furaha, au zina wito maalum kwenye mambo yao. Ukiona simu zako hazipokelewi jiongeze!

Wakati mwingine unaweza kumpigia mtu simu zaidi ya mara tano lakini hupokelewi. Unatuma jumbe nyingi lakini hujibiwi. Tangu ulipomtafuta kwenye simu (hakupokea na hakujibu jumbe zako), sasa yamepita masaa kumi na nne (14); kimya!

Swali la kujiuliza; Je, uliyempigia simu hakushika simu yake kwa saa (masaa) kumi na nne toka ulipomtafuta?

Ukweli ni kwamba amekuta "Missed Calls na SMS" zako, lakini wewe huna umuhimu kwake, huna faida kwake, humpi furaha ya aina yoyote, hivyo ameuchuna.

Hutoamini kwasababu unamwamini, unampenda, na unajipa urafiki wa karibu kwake lakini ukweli ni kwamba yeye si rafiki yako - humjui. Hakupokea simu zako ulizompigia saa 14 zilizopita lakini katika hizo saa 14 ameshapost mambo yake huko Whatsapp Status.

Ndugu yangu, sikuhizi mwisho ni MISSED CALLS MBILI (02) tu, kama wewe ni mtu muhimu sana kwake atapokea/atakupigia, atakubeep/au atakutumia tafadhali nipigie.

RIGHT MARKER
Dar es salaam.
 
Back
Top Bottom