Usidanganyike! Sex meditation ni ibada za kishetani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,655
729,721
Nimesita kwa muda kuweka hii mada lakini usiku huu baada ya meditation nimejikuta navutika kuiweka hapa lakini vilevile nikitimiza ahadi ya mdau Ms mol

Kwanza ni lazima tutambue kuwa ngono na tahajudi ni vitu vya kihisia zaidi kiroho zaidi kupitia jumbamwili linalowaka tamaa.

Tahajudi(meditation) ni somo moja pana sana lenye mazuri mengi na mabaya mengi. Tahajudi inatumiwa na:

Matapeli
Wafanya mazingaombwe
Wanasiasa
Wafanyabiashara
Wanazuoni
Washika dini (mitume na manabii)

Waabudu sanamu na nguvu za giza kama imani za kishetani nk
Wote tunajua nguvu ya ngono na hii ndio dhambi ya asili, Adamu aliangukia hapa, Samsoni wa Delila hapa hapa, mfalme Suleimani na hekima zake alikuwa na wake mia tatu na masuria idadi hiyo hiyo (hapa King Mswati anasubiri sana)

Ngono imewaangusha wengi sana kuanzia washika dini, viongozi mbalimbali mpaka watu wa kawaida kabisa

Tahajudi inatumiwa na kutumika vibaya na watu wenye agenda za siri, agenda za kukidhi tamaa zao za mwili kwa jina la tahajudi.

Kuna wenye kumaanisha lakini ni wachache mno, wengi wanaofanya sexual meditation ni wale wa imani za kishetani bila kujitambulisha wazi, lakini pia ndani ya ibada za kishetani, ngono ni kipengele kimoja muhimu sana. Nimehudhuria nimeona.

Najua Wengi wana munkari wa kutaka kufanya meditation, lakini ni vema sana ukawa makini na kile unachotarajia ama kutaka kufanya.

Mambo mengi siku hizi yamefanyiwa kolabo. Jihadhari sana unapojifunza hizi elimu ngeni

Alamsiki

Jr.!
 
Sex meditation ni nini?
 
Hivi wale wanaume wanaokaa mahali mida ya jioni kuangalia wadada warembo wanapita na vinguo nguo vyao vya mitego huku wakiwatamani mpaka wanapata mfadhaiko wa kiutu uzima si wanakuwa wamefanya hii sexual meditation??

Vipi kwa wale wanaojichua???
Mentally pre acted state.... Maranyingi mwanaume akimwangalia mwanamke kimatamanio anakuwa ameshazini naye kihisia
 
Hivi wale wanaume wanaokaa mahali mida ya jioni kuangalia wadada warembo wanapita na vinguo nguo vyao vya mitego huku wakiwatamani mpaka wanapata mfadhaiko wa kiutu uzima si wanakuwa wamefanya hii sexual meditation??

Vipi kwa wale wanaojichua???
Kiongozi ungetuwekea nyamanyama japo kidogo kwa sie ambao hatujui kabisa, labda hata ungetuelezea kdg hizo meditation za ngono zinavokuwa' na hao wanaozitumia kwa tamaa binafsi wanazitumiaje? Wanaotumia kisahihi wanatumiaje? Kazi ya meditation ni nn?
 
Kufanya ngono kuzini etc ni lugha tu kitendo ni kilekile

No si kweli hata kdg usipotoshe watu tafadhali. Unachosema ni UONGO Adam ha kufanya hilo usemalo. Huwezi sema hivyo kua sex na mkeo ni kuzini.

Huu ni uongo mwingine shetan anatumia kupotosha km alivyodanganya Hawa kua hakika hutakufa na imezaa ibada ya mizimu. Muasisi wake ni shetani, mtu akifa hakuna jinsi ya kurudi in any form.
 

Mmh haya ila naona kama umechanganya vitu viwili kwa mpigo
Kwangu mimi kulia na kucheka zote ni kelele.

Sasa kitendo cha mwanaume kuingiliana kimwili na mwanamke kina majina mengi kama uasherati ngono kuzini kufanya tendo la ndoa nknk hizi ni mbwembwe tu za lugha kitendo ni kilekile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…