Usichokijua kuhusu pande kuu nne za dunia

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,331
16,311
Nawasalimu wote mliopo humu ndani
Kitu chochote ambacho Mungu anakitumia kwa mazuri na satani naye anakitumia kwa ubaya..

Umewahi kujifunza pande kuu nne za dunia na majina yake ya Kaskazini, Kusini, Mashariki, na Magharibi?. bila shaka utaniambia ndio.

Sasa katika ulimwengu wa roho hizi pande kuu nne za dunia zinatumika ipasavyo na Mungu mwenyewe, pamoja na satani.

Umewahi kusikia nchi za Kaskazini, pia nchi za Kusini, pia nchi za Mashariki, pia nchi za Magharibi.

Sasa popote ambapo nchi yako inapatikana au upande ambao nchi yako inapatikana, ukae ukijua kuanzia leo.

Satan ana ngome zake huko na zinafanya kazi kama ifuatavyo:
Nchi za Kaskazini zinaongoza kwa kuwa na uganga mwingi.
Nchi za Kusini zinaongoza kwa kuwa na ushetani mwingi.
Nchi za Mashariki zinaongoza kwa kuamini sana kwenye mizimu.
Nchi za Mangaribi zinaongoza sana kwa uchawi.

Na sio mambo ya nchi tu hata hapo ulipo katika nchi yako, ipo hivyo hivyo kutokana na upande unaotoka.

Kazi kwako kuamini katika ubaya au mazuri.

Hizo pande pia Mungu anazilinda kupitia Malaika wanne aliowaweka kwa wale wanaofuata katika upande wa kumcha Mungu.

Hitawataja wakati mwingine.
 
Umelala umeamka ukawaza na mawazo Yako yaloshiba kiporo Cha pilau ukaamua uropoke,
Mambo ya kiroho yanahitaji maarifa na utashi sio hisia
 
Back
Top Bottom